Kamanda wa polisi mkoani wa Kinondoni (RPC), Charles Kenyela.
Jeshi
la Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, limelalamikiwa kwa vitendo vya
baadhi ya askari wake kuvamia vyumba vinavyodaiwa kupangwa na watu
wanaodaiwa kuwa makahaba (madanguro) na kuwapora fedha, simu na vitu
vingine vya thamani nyakati za usiku.
Aidha, askari hao wamedaiwa kuwageuza wanawake hao mashine za kutolea fedha (Atm) ambapo hufika katika vyumba vyao kila baada ya wiki moja na kuwadai fedha kati ya Sh.30,000 na 50,000 kila mmoja kama hongo ili wasiwafikishe polisi.
Malalamiko hayo yametolewa na baadhi ya akina mama wanaoishi eneo la Mwananyamala walipozungumza na NIPASHE baada ya askari hao kukamata wanawake zaidi ya 87.
Kiongozi wa wanawake hao, Judith Rugamwa alidai kuwa, askari hao kutoka vituo vya Oysterbay na Mabatini wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuwapiga, jambo ambalo ni kinyume cha haki zao binadamu.