STAA
wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amesema
mwaka huu atawachanganya wanaume kama afanyavyo Nasibu Abdul ‘Diamond’
ili kwenda sawa. Akifafanua kauli yake kwa paparazi wa Stori 3, Baby Madaha aliweka bayana kuwa haoni tatizo kunaswa na Mwisho Mwampamba kama ilivyoripotiwa hivi karibuni wakati huohuo anatoka kisela na mkali wa Bongo Fleva, Juma Kassim ‘Nature’. “Watakoma mwaka huu, lazima niwachanganye sana, mbona wao wanatuchanganya sana kama Diamond vile anavyofanya!” alisema Baby. |
Monday, April 22, 2013
BABY MADAHA: NTAWACHANGANYA WANAUME KAMA DIAMOND
Sunday, April 21, 2013
WASOMI:::SPIKA ANAVURUGA BUNGE
Baada
ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kutoa mwongozo na kuunga mkono uamuzi
wa Naibu wake, Job Ndugai kuwasimamisha wabunge sita wa Chadema, wasomi,
wanasiasa na wanaharakati wamesema Kiti cha Spika ndiyo chanzo cha
mvutano bungeni kwa kuwa kinapendelea wabunge wa chama tawala (CCM).
Wamesema
licha ya Bunge kuongozwa na kanuni, wakati mwingine viongozi hao wa
Bunge wanatumia kanuni hizo kuwapendelea wabunge wa CCM, huku wakieleza
kuwa licha ya wabunge wa chama hicho kutukana, hawakupewa adhabu yoyote.
Jumatano
ya wiki hii, Ndugai aliwasimamisha Tundu Lissu (Singida Mashariki),
Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini),
Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiah Wenje (Nyamagana) na Godbless Lema wa
Arusha Mjini kutohudhuria Bunge kwa siku tano kutokana na alichokiita
kufanya vurugu ndani ya Bunge.
Uamuzi
huo wa Spika Makinda ulikuja baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kumtaka Ndugai aeleze alitumia kanuni
gani kuwasimamisha wabunge hao.
DAWA ZA KUONGEZA AKILI ZATUA NCHINI
Mtindo wa maisha, ulaji na msongo wa mawazo, vimewasababishia Watanzani wengi maradhi lukuki hata vifo.Hata hivyo, wataalamu wa afya kutoka Afrika Kusini wamekuja na dawa maalumu, zilizo na uwezo wa kurudisha kumbukumbu, kuongeza upeo darasani, kuondoa sumu mwilini na kumfanya mzee kuonekana kijana.
Dawa
hizo zinazotumia vitamini zilizomo kwenye vyakula vya kila siku, zina
uwezo wa kuongeza kiwango cha uelewa kwa mwanafunzi au mfanyakazi.
Kiwango hicho cha uelewa kitaalamu unatambulika kama ‘IQ’.
Mratibu wa dawa hizo hapa nchini, John Haule anasema kuwa dawa hizo zina uwezo wa kufanya kazi kwa haraka.
“Virutubisho hivi ni vizuri kwa wale wanaokwenda katika
mitihani au wanataka kufanya kazi inayohitaji umakini wa hali ya juu,” anasema Haule na kuongeza: “Zimetengenezwa kwa vyakula tunavyotumia na siyo kemikali.”
mitihani au wanataka kufanya kazi inayohitaji umakini wa hali ya juu,” anasema Haule na kuongeza: “Zimetengenezwa kwa vyakula tunavyotumia na siyo kemikali.”
Haule
ambaye ni mtaalamu wa tiba asili na mimea anasema kwamba mtindo wa
maisha na vyakula vinavyoliwa na watu mara kwa mara kwa sasa huufanya
mwili kuhifadhi sumu nyingi mwilini.
MUME WA MTU ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUFANYA MAPENZI NA MBUZI MWENYE MIMBA NA KUHARIBU MIMBA YA MBUZI HUYO
Marcel
ambaye ni mume wa mtu, alifunguliwa kesi namba 29/2013 katika Mahakama
ya Mwanzo ya Bashneti mkoani Babati kwa kosa la kuiingilia kimwili
mifugo, kinyume na kifungu cha 325 kanuni ya adhabu, sura ya 16 na kesi
hiyo ilisomwa hivi karibuni.
Mshitakiwa
aliwekewa dhamana lakini siku chache baadaye kesi ilipotakiwa
kuendelea, hakuonekana na imebainika mahakamani hapo kuwa ametoroka.
Kesi
hiyo ipo mbele ya Hakimu Julius Dagharo wa mahakama hiyo na
aliyethibitisha mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa ametoroka ni Afisa
Mtendaji wa Kijiji cha Bashneti, Omari Mwanditi.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki iliyopita, mmiliki wa mbuzi anayedaiwa kuingiliwa,
Clementina Masay alidai kuwa mtuhumiwa huyo amemsababishia hasara kwani
mbuzi wake alikuwa na mimba lakini baada ya kitendo hicho, imeharibika.
Jamii
ya wafugaji wa Kiiraq wa eneo hilo wamesikitishwa na kitendo cha
mtuhumiwa kudaiwa kuiingilia mifugo yao kimwili mara kwa mara na
wameahidi kumsaka hadi wamkamate.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Babati, ACP Akili Mpwapwa amekiri
kutokea kwa tukio hilo na ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa
wakimuona mtuhumiwa huyo ili afikishwe mahakamani.
AMA
kweli dunia imekwisha kwani mtu mmoja, Daniel Marcel (27), mkazi wa
Kijiji cha Madunga, wilayani Babati, Manyara, amekamatwa na kufikishwa
mahakamani kwa madai ya kufanya mapenzi.
WAREMBO WA XTRA BONGO WAZITWANGA NGUMI, KISA BUZI LA KIZUNGU.
Otilia Boniface kulia na Janeth Tingisha
Wanenguaji wa Bendi ya Extra Bongo, Otilia Boniface na Janeth Tingisha mwishoni mwa wiki iliyopita walitoa kali ya mwaka baada ya kutaka kutwangana makonde wakigombea kutoa namba zao za simu kwa buzi la Kizungu.
Tukio hilo lilitokea
ndani ya Ukumbi wa Meeda uliopo Sinza jijini Dar ambapo awali Mzungu
huyo alivutiwa na wadada hao hivyo kuwafuata na kuomba namba ya simu ya
mmoja wao.
Kufuatia ombi la Mtasha huyo, kila mmoja alitaka apate
nafasi hiyo ndipo wanenguaji hao waliposukumana na kufikia hatua ya
Janeth kuchukua simu ya Otilia na kuipiga chini ila kwa busara za Mzungu
huyo alichukua namba za wote.
JUMA NATURE ATIMULIWA EATV BAADA YA KUINGIA AKIWA AMEVAA KANDAMBILI.....
Msanii
mkongwe na maarufu nchini, Juma Kassin Kiroboto, aka Nature,
ameonyesha kukerwa na kitendo cha kutimuliwa jana usiku katika
kipindi cha burudani cha televishen inayotizamwa africa ya mashariki
alipokuwa akifanya nao interview.
Nature
alionekana akiwa amevaa kawosh na ndala na mara baada ya mahojiano
mafupi ya mwanzo mtangazaji alisema watarejea baada ya mapumziko
mafupi na ndipo Nature hakuonekana tena.
Kilichotokea kwa mujibu wa Nature mwenyewe, ni wakati wa mapumziko
hayo, mtangazaji wa kipindi hicho alimfuata na kumuambia kuwa
hataendelea na interview tena kwasababu ya mavazi aliyokuwa kavaa
ambayo ni ndala na kawosh. kuonyesha kukerwa kwake na ishu hiyo Nature aliamua kuandika yafuatayo kupitia ukurasa wake wa facebook....
"hivi kwa mfano angekuwepo mzungu pale na kavaa ndala wangesitisha mahojiano na kuvaa kaoshi ni tatizo....
kunywa
nimekunywa bt kuna baya nimeliongea na hivi kama kweri we nimuandishi
wa habari unaruhusiwa kuvaa vile kisheria kama yule mtangazaji
nimeboreka kinoma na ikiwezekana nasitisha kuanzia ssa kupeleka ngoma
zangu pale siitaji interview"
WABUNGE WATAKA JUMBA LA MCHUNGAJI LWAKATARE LIVUNJWE.........!!!
'Hekalu' linalomilikiwa na Mchungaji Getrude Lwakatare. |
Wabunge
wamemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira Terezya
Huvisa kuzivunja nyumba mbili zilizopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam
zilizojengwa katika fukwe ya bahari ya Hindi ikiwemo ya mbunge licha ya
kwamba kuna zuio la mahakama.
Bila kutaja majina ya wamiliki hao, wabunge hao walitaka hatua hizo zichukuliwe kwa haraka kwa nyumba hizo zilizojengwa kwenye fukwe kinyume cha sheria zivunjwe kwa maelezo kuwa hazina ofa wala hati.
Sambamba
na hilo wametaka watendaji wa serikali waliohusika kutoa vibali
kuruhusu ujenzi huo kwa maelezo kuwa walichukua rushwa wachukuliwe
hatua.
SHY- ROSE BHANJI APATA AIBU YA KARNE TOKA KWA ANNA KIBIRA
Aliyekuwa
mjumbe baadae katibu mkuu wa CHANETA Anna Kibira amechaguliwa tena
kuwa mwenyekiti wa chama cha mpira wa pete chaneta Katika uchaguzi
uliofanyika jioni ya leo hii Mkoani Dodoma , huku msimazi wa uchaguzi
huo akiwa mkuu wa wilaya ya bahi na aliyekuwa Mtangazaji wa zamani wa
itv Betty Mkwasa .
Anna
Kibira amemshinda mpinzani wake Shy-Rose Bhanji kwa tofauti ya la
kura arobaini katika nafasi ya uenyekiti Anna Kibira amepata kura 61
dhidi ya mpinzani wake Shy-Rose Bhanji ambaye amepata kura arobaini na
moja .
Aidha
kulikuwa na nafasi mbalimbali ambazo zilikuwa zikigombewa katika chama
hicho cha mpira wa pete ambapo kulikuwa na wajumbe wa kamati ya
utendaji ambao walikuwa wagombea tisa lakini wamepataikana wagombea
sita tu.
Grace
Khatib ambaye alikuwa hana mpinzani katika nafasi ya mweka hazina
alipata kura za ndio 66 na kura za hapana 16 kati ya kura 82
zilizopigwa.
Katika
nafasi ya makamu mwenyekiti kulikuwa na wagombea wawili Zainab Mbiro
na Agnes Madasila katika nafasi hiyo Zainabu Mbiro alipata kura hamsini
saba wakati mpinzani wake amepata kura 27
Kwa
maana hii CHANETA imepata safu mpya kabisa ya uongozi baada ya ile ya
mwanzo ile kuamua kuachia ngazi na wagombea wengine kuamua kutokugombea
kabisa uongozi katika chama hicho cha mchezo wa pete kwani safu mpya
inatakiwa kufanya kazi ya ziada kufikia malengo ya kuinua mchezo wa
mpira wa pete kwani uongozi uliopita uliiwezesha CHANETA kuifikisha
timu ya taifa ya mchezo huo katika mashindano ya dunia.
Chama
kiliweza kuaandaa michuano ya mataifa ya afrika ni wazi kabisa
wanachangamoto kubwa ya kufanya japokuwa mara baada ya ushindi kibira
amesema kuwa anataka kuupeleka mchezo huo mikoani na kwenda kuuimarisha
zaidi vijijini .
Saturday, April 20, 2013
Rais wa zamani wa Pakistan Jenerali Musharraf akamatwa akijiandaa kugombea ubunge.
Polisi nchini Pakistan wamemtia mbaroni rais wa zamani wa nchi hiyo Jenerali Mstaafu Pervez Musharraf.
Musharraf amekamatwa leo nyumbani kwake mjini Islamabad na kufikishwa mahakamani.
Kiongozi
huyo alirejea Pakistan mwezi uliopita, akitarajia kuwania ubunge katika
uchaguzi mkuu mwezi ujao, baada ya kuwa uhamishoni kwa miaka minne.
Hata
hivyo ombi lake lilikataliwa na maafisa wa uchaguzi, kwa misingi
kwamba anakabiliwa na mashitaka ya uhaini yanayohusiana na kipindi
chake cha utawala.
Hapo Jana mahakama mjini Islamabad iliamuru Musharraf akamatwe.
ROSE NDAUKA AWATEGA MADENTI WA DSJ, HIKI NDO ALICHOKIFANYA
STAA mwenye mvuto wa kipekee kwenye ‘industry’ ya filamu Bongo, Rose
Ndauka hivi karibuni alitinga kivazi kifupi ambacho kiliwachengua
madenti wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) ambao
walibaki kumkodolea macho mwanzo mwisho.
Mpango mzima ulitokea Aprili 13, mwaka huu katika Ufukwe wa Belinda, jijini Dar wakati mwanadafada huyo alipokuwa amealikwa katika sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa chuo hicho.
Mpango mzima ulitokea Aprili 13, mwaka huu katika Ufukwe wa Belinda, jijini Dar wakati mwanadafada huyo alipokuwa amealikwa katika sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa chuo hicho.
Kutokana na kivazi hicho alichokivaa na mvuto alionao staa huyo, baadhi ya madenti wakware walionekana wakipoteza usikivu wa hotuba ya mgeni rasmi na kubaki kumtazama.
“Mh! Rose ni mzuri jamani uongo dhambi, nilikuwa nikimuona katika runinga leo nimemuona live daaah!” alisikika denti mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
ANAYEMWEZESHA WEMA SEPETU KIMKWANJA AJULIKANA,
VIROBA TISHIO JIPYA LA SARATANI YA KOO KWA WANAUME
Daktari
bingwa wa uchunguzi wa magonjwa ya saratani katika Kitengo cha
Patholojia, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Henry Mwakyoma na
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani katika Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road, Dk Crispin Kahesa wameeleza hayo jijini Dar es Salaam.
Walisema
kuwa ingawa bado hakuna visababishi kamili vya saratani hiyo, asilimia
90 ya wagonjwa wa saratani ya koo wamekuwa na historia ya uvutaji
sigara, unywaji pombe kali kama viroba na kula aina za vyakula
vilivyochomwa
ikiwamo nyama na samaki, ulaji pilipili, ndimu, ‘chilisosi’ na unywaji wa vitu vya moto kupita kiasi.
“Ongezeko
ni kubwa, asilimia 90 ya wagonjwa tuliowapokea hapa wana historia ya
kutumia vilevi vikali, sigara, pilipili kwa wingi na aina nyingine na
vitu vinavyosababisha saratani hii,” anasema Dk Kahesa.
Fid Q Atoa Mauzo RBT Ya Wimbo Wake Mpya Kuweka Kumbukumbu Ya Marehemu Bi. Kidude ...
Kuna uthubutu wa kusema kuwa hili inawezekana kuwa ni wazo zuri na jema kabisa ambalo toka mwaka uanze umewahi kulisikia ...
Rapper
kutoka MWANZA CITY, Fid Q amependekeza kujengwa kwa kumbukumbu
itakayomuenzi ambayo pia itatumika kusaidia waliokuwa karibu na marehemu
Bi. Kidude aliyefariki na kuzikwa jana huko visiwani Unguja ...
Akiongea
katika radio interview na kipindi cha XXLkinnachoongozwa na BDozen,Fid Q
amependekeza kufanyika kwa jambo hilo hata kwa harambee
itakayochangisha fedha za kufanikisha kitu hicho ...
Kwa
kuanzia, Fid Q ambae alipata nafasi ya kurekodi wimbo pamoja na
marehemu,"JUHUDI ZA WASIOJIWEZA" uliokuwa kwenye album yake ya
Propagandaametoa mauzo yote ya miito ya simu, yaani Ring Back Tones
[RBT]yatakayouzwa kwa wananchi na wapenzi wa muziki katika kusaidia
ujenzi wa museum hiyo ...
Fid Q "Sitachukua hata thumni ..."
Hiki
ni kitu cha kujivunia kuwa na mwanamuziki kama huyu ambae naweza kusema
anauona umuhimu wa wanamuziki wakubwa hapa nchini, Bi. Kidude amekuwa
mwanamuziki wa Taarabu aliyefanya vizuri sana na kuitangaza nchi hii ...
Mimi na wewe, tuanze kwa kushiriki kwenye hili ... BIG UP Fareed !!!
R.I.P Bi. Fatuma binti Baraka a.k.a Bi. Kidude
Subscribe to:
Posts (Atom)