Ngoma inaonekana kuwa bado ni nzito
kuhusiana na mirathi ya marehemu Steven Kanumba kwani taarifa
zilizopatikana hivi karibuni zinaeleza kuwa, hakuna kitu kilichofanyika
mpaka sasa kutokana na mvutano uliokuwepo ndani ya familia.
Akizungumza na Risasi Jumatano hivi karibuni, mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa alisema yeye aliamua kukaa pembeni na kumuachia baba wa marehemu, mzee Charles Kusekwa afuatilie suala hilo lakini anashangaa mwaka umepita hakuna kilichofanyika.
Akasema, alisikia mzee huyo alituma wawakilishi wake walishughulikie suala hilo lakini wakachemsha kutokana na kukosa viambatanisho muhimu.
“Mimi niliamua kusubiri upande wa baba Kanumba wafungue mirathi kwa sababu Kanumba hakuwa na mtoto kusema nina ulazima wa kuharakisha ili apate haki zake, cha ajabu hakuna kilichofanyika mpaka sasa,” alisema mama Kanumba.
Akasema, kutokana na kwamba ametoa muda mrefu kwa mzee Kusekwa kushughulikia suala hilo bila mafanikio, ameamua kuingia ‘front’ mwenyewe ili kuhakikisha haki za mwanaye zinapatikana.
Credit:Global Pubishers.