Wednesday, April 17, 2013
MAKAMBA ASHITAKIWA KWA KINANA
WanaCCM wa Ifakara mjini ‘wamemshtaki’ Katibu Mkuu
wa zamani wa CCM, Yusuph Makamba kwa Katibu Mkuu wa sasa wa chama hicho,
Abdulrahman Kinana kwa ahadi yake aliyoitoa 2008 ya kuwapatia Sh1
milioni ambayo hajaitimiza.
Mwenyekiti wa
CCM wa tawi la Ifakara mjini, Felista Chakachaka alisema kwamba mwaka
2008, Makamba alipotembelea tawi hilo, aliwaahidi kuwapatia
Sh1 milioni
kwa ajili ya kazi za tawi hilo lakini hakuitekeleza.
Hata hivyo, Makamba aliyeko Bumbuli mkoani Tanga,
alisema jana: “Sawa, mimi nilitoa ahadi hiyo, sikuitekeleza, sasa
aliyepo si ndiyo anatoa...kwani ahadi za Mwalimu Nyerere si Mzee Ali
Hassan Mwinyi kazitekeleza, sawa na ahadi za Benjamini Mkapa ambazo Rais
Jakaya Kikwete anatekeleza.
Akijibu hoja hiyo, Kinana alisema kwa kuwa Makamba
aliahidi kiasi hicho cha fedha akiwa katibu mkuu, basi yeye atatoa fedha
hizo. “Katika kipindi cha wiki mbili fedha hizo zitakuwa zimeingia
katika akaunti yenu..nitawapatia kama alivyoahidi alisema Kinana.
Mbali na kutembelea tawi hilo, Kinana
alifungua mashina ya wakereketwa matano mjini Ifakara.Kinana yuko
ziarani mkoani humo kuangalia maendeleo ya chama hicho tawala.
SOURCE::MWANANCHI:
MILA POTOFU ZACHANGIA KUONGEZEKA KWA MAAMBUKIZO YA UGONJWA MALARIA MKOANI MBEYA
......................................................................
Na Esther Macha, Mbeya
Na Esther Macha, Mbeya
LICHA ya
Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya
vyandarua hali hiyo bado imekuwa tatizo kutokana jamii zilizo nyingi
Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kuwa na imani potofu kuhusu matumizi
ya vyandarua vyenye dawa kuwa hawapati usingizi na wengine kudai ni
njia ya uzazi wa mpango.
Hayo
yalisemwa jana Bwana afya katika Ofisi ya Wilaya ya Mbarali Bw.Yona
Msyani wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili, kuhusiana na elimu
ya ugonjwa wa maralia katika viwanja vya hospitali ya Chimala Mission
.
Alisema
kuwa suala la utumiaji wa vyandarua imekuwa changamoto kubwa kwa
katuiika utendaji kazi kwa wataalamu wa afya kutokana na wananchi
kuwa na imani potofu juu ya matumizi ya vyandarua vyenye dawa.
“Bado tuna changamoto kubwa sana hivyo inatupasa kujipanga na kuelimisha jamii kutambua umuhimu wa matumizi ya vyandarua “alisema.
Hata hivyo alisema kuwa imani hiyo potofu si kwa Wilaya ya mbarali tu kwani hali hiyo ilijitokeza wakati wa kampani ya ugawaji wa vyandarua hivyo mwaka 2010 kwa nchi nzima.
Bw.
Msyani alisema kuwa kama wataalamu wa afya bado wanaendelea kutoa
elimu ya afya kwa wananchi jinsi ya kujizuia na ugonjwa wa maralia
ikiwa ni pamoja na kuondokana na dhana potofu waliyojenga wananchi.
Akizungumzia kuhusu vifo ambavyo vinatokana na ugonjwa maralia ,Bwana afya huyo alisema kuwa maralia I ugonjwa ambao unaongoza kwa vifo hasa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
“Tatizo hili lipo kwa kiasi kikubwa kwa watoto , mwaka 2012 mwezi januari mpaka desemba waliugua watoto 1,635 chini ya umri wa miaka mitano ambapo kati ya hao waliofariki ni 100 kwa mwaka jana kutokana na ugonjwa wa maralia.
Tuesday, April 16, 2013
DIAMOND AMTOLEA NJE WEMA NA KUMPAMBANISHA NA PENNY AMREKODI NA KUSAMBAZA CLIP
Clip iliyosambaa inayomuhusisha Wema Diamond na Penny imefika ndani ya
blog yako, clip ambayo inaonekana kurecodiwa kwa maksudi na Diamond pale
alipopigiwa simu na Wema Sepetu jana usiku. Inasemekana Wema alimpigia
simu Diamond usiku, lakini baada ya Diamond kupokea alimtaka kuacha drama
na kumsisitizia kuwa sasa hivi anampenda Penny.
maongezi yako hivi
Diamond: mi sikufanyii drama na wala sitaki drama yoyote, am
inlove with penny we unajua hilo right?
Wema: yeah your inlove with Penny and i i ...
Diamond: sipendi kwasababu sipendezewi kwasababu mwisho wa siku
itakuja kutuletea matatizo drama, nakujua kitu kidogo hukawi kukifanya
kikubwa mji mzima na nini na nini sitaki.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA SIKU MBILI WA UDHIBITI WA HUDUMA ZA KIUCHUMI BARA LA AFRIKA, JIJINI ARUSHA LEO
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma
hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano wa kimataiafa wa siku mbili
wa Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Bara la Afrika, ulioshirikisha
mataifa mbalimbali kutoka Bara la Afrika, ulioanza leo Aprili 16, 2013
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua
Kitabu cha Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Bara la Afrika, wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili wa Udhibiti wa Huduma za
Kiuchumi Bara la Afrika, ulioshirikisha mataifa mbalimbali kutoka Bara
la Afrika, ulioanza leo Aprili 16, 2013 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Kitabu hicho kimetungwa na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Prof. Mark Mwandosya. Kulia ni Waziri
wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) ni Mkurugenzi wa Ewura,
Haruna Masebu.
Baadhi ya washiriki
wa mkutano huo wakiwa ukumbini wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal
wakati akiwahutubia.
HUYU NDIYE MBUNGE ALIYEMWAMBIA SUGU 'SIONGEI NA MBWA NAONGEA NA MWENYE MBWA........!!
Mkutano wa 11 wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaendelea huko Dodoma na wabunge
wameendelea kujadili bajeti ya ofisi ya waziri Mkuu katika kikao cha 5.
Siku hizi watu wengi wamezoea kusikia malumbano ama vijembe wanavyotoleana
wabunge wetu, licha ya kuwa vinakuwa sehemu ndogo tu na
wanaendelea na hoja za kutusaidia watanzania, lakini bunge limekuwa
tofauti sana hasa kwa kuzingatia matumizi ya lugha na hata tafsiri ya
lugha hizo.Siku hizi watu wengi wamezoea kusikia malumbano ama vijembe wanavyotoleana
Leo asubuhi mbunge wa jimbo la Kondoa kusini Juma Suleiman Nkamia alimwambia mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) kuwa “kumbuka siongei na mbwa naongea na mwenye Mbwa”. Sentensi hii ilitamkwa na mbunge huyo baada ya kusikia sauti ya Sugu akijaribu kukataa kile alichokuwa anachangia bila kufuata utaratibu wa kunyoosha mkono ama kumuomba naibu spika, na ndipo alipomuomba kuwa na heshima kwanza kwa kumtaja kwa jina la ‘Sugu'
PENNY: "NIMEMSAMEHE DIAMOND INGAWA ALINISALITI KWA UWOYA....KWA SASA TUMEYAMALIZA"
Katika muda ambao kila mmoja alikuwa amejaribu kuamini kuwa Diamond Platnumz ameamua kutulia na mpenzi mmoja, mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa, hivi karibuni staa huyo ameanzisha uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa filamu Irene Uwoya.....
Magazeti ya udaku nchini yaliandika habari hiyo ikiwa na picha inazowaoenesha mastaa hao wakichukua chumba kwenye hoteli ambako walienda kufanya yao.
Kufuatia tetesi hizo, mwandishi wetu amezungumza na mpenzi wa sasa wa Diamond, Penny ambaye amesema kwa ufupi kuwa wameshayazungumza na Diamond na wako vizuri kwa sasa lakini akasisitiza kuwa asingependa kuliongelea zaidi suala hilo.
Katia hatua nyingine, Jokate Mwegelo aliyewahi kuwa na uhusiano na Diamond amekanusha taarifa iliyoandikwa na gazeti moja la udaku kuwa amemcheka Irene kwa kunaswa kwenye himaya ya Diamond.
“Mimi hivyo vitu havinihusu na wanapenda kupata quotes zangu pasipo hitajika. I don’t know why? I don’t why wanatafuta story. That’s their life kiukweli with whatever they choose to do, more power to them,” amesema Jokate.
Kutoa Taarifa za Siri Katika Mawasiliano ya Elektroniki ni Kosa la Jinai.
Jana
na leo, Serikali imeona kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya
utunzaji wa siri za taarifa za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa
huduma za simu za mkononi. Taarifa hizo zimefikia hatua ya kuchapishwa
katika vyombo vya habari kwa kutaja bila idhini yao, namba za simu,
wahusika wa namba hizo, maongezi na muda wa mawasiliano Kati yao. Jambo
hili ni Kosa la Jinai. Mfano; tamko la Chadema lililotolewa na Ndugu
Mabare Marando Mjini Dar es Salaam tarehe 14/04/2013.
Serekali inapenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha wenye makampuni ya
Simu, Vyombo vya Habari na wananchi kwa ujumla kuwa, kutoa taarifa za
mawasiliano binafsi ya simu baina ya watumiaji wa huduma hiyo, ni
uvunjaji wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Na. 3 ya
mwaka 2010 na Kanuni za Mawasiliano (Kulinda Wateja) za mwaka 2005.
Kifungu cha 98 ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta
kinasema;
“Mtu yeyote ambaye ni mfanyakazi wa kampuni yenye leseni ya kutoa
huduma za mawasiliano, au mwakilishi wake, ana wajibu wa kutunza siri za
mawasiliano binafsi na taarifa zozote za siri za wateja kwa mujibu wa
sheria hii”. Aidha, “Mtu yeyote haruhusiwi kutoa taarifa binafsi za
mteja yeyote alizopokea au kusikia kwa mujibu wa sheria hii isipokuwa tu
mtu huyo ameruhusiwa kwa mujibu wa sheria”
Monday, April 15, 2013
JB AJITOSA KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE MWAKA 2015..!!
Akizungumza na paparazi wetu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, JB alisema ameamua kuweka wazi ndoto yake hiyo ya miaka mingi ambapo ilikuwa kuitumikia jamii ya Kitanzania.
“Nimeamua kuweka wazi kwamba mwaka 2015 nitajitosa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha ubunge. Nia ninayo, uwezo ninao na sababu pia ninayo, ni muda muafaka sasa wa kutimiza ndoto yangu ya kuitumikia jamii,” alisema JB.
Hata hivyo, ‘mheshimiwa’ huyo hakuwa tayari kuanika ni jimbo gani atagombea akisema atatangaza baadaye licha ya kudai kwamba ni jimbo moja kubwa lenye upinzani mzito kila ukifika wakati wa uchaguzi.
“Nasisitiza nitagombea, lakini siwezi kuweka wazi ni jimbo gani, hilo nitaliongelea baadaye, ila ni kubwa lenye upinzani mkubwa kila wakati wa uchaguzi,” alisema JB.
KAJALA APATA MCHUMBA MPYA, NI MFANYAKAZI WA WEMA
Kajala ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa mtayarishaji wa muziki maarufu hapa Bongo “P-Funk” na kufanikiwa kupata naye mtoto mmoja, hivi sasa inasemekana ana-roll na mchizi mmoja ambaye ni member wa kampuni ya Endless Fame ya Wema Sepetu. Solid snitch wa bongomovietz.com ambaye amezipata za chinichini na ku-notice nyendo mbili tatu za bootylicous actress Kajala Masanja kupitia BBM na mshkaji huyu. Directly unaweza kukubali kwamba yes, Jamaa na Kajala ni mtu na mpenzi wake kwa sasa. All is well, its a new life for Kajala and she deserve to love and to be loved. Best wishes kwenye kila anachokifanya hasaa kazi ya yake ya movie.
SHIBUDA AANDAA MAANDAMANO YA NG'OMBE HADI IKULU KWA KIKWETE
Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda
anatarajia kuongoza maandamano makubwa ya ng’ombe kutoka Lusumo
Nyakabanga Mkoani Kagera, hadi Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete ili kupinga
uonevu na manyanyaso wanayofanyiwa wafugaji.
“Kama watu
wanasema ni porojo za Shibuda, basi wasubiri kama hotuba ya Waziri Mkuu
haitakuwa na majibu kwa wafugaji, lazima hayo yatatokea kwa mara ya
kwanza katika historia ya nchi yetu, hawa nao ni binadamu waambiwe basi
kama hawatakiwi Tanzania,” alisisitiza.
Mbunge huyo
alitoa kauli hiyo juzi akiwa na uongozi wa wafugaji kutoka Kanda ya Ziwa
ambao wako Dodoma kwa lengo la kuonana na Mawaziri wa Maliasili na
Mawaziri wa Mifugo akiwemo Waziri Mkuu, ili kufikisha kilio cha wafugaji
ambao wanateketezewa mifugo yao na askari wa wanyama pori.
Shibuda alisema
kuwa “Katika nchi yoyote duniani hakuna mateso yanayofanywa kwa wananchi
wake kama ambavyo inafanyika Tanzania kwa upande wa wafugaji, ni heri
ya wakimbizi watakuwa na amani kuliko hawa wanaonekana kama takataka.”
JOKATE AMCHEKA UWOYA BAADA YA KUSIKIA KATOKA NA DIAMOND
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
MWANAMITINDO Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, ameangua kicheko
baada ya kusikia mwigizaji Irene Uwoya kunaswa hotelini na Nasibu Abdul
‘Diamond’.
Jokate aliangua kicheko hicho juzikati
jijini, Dar wakati alipozungumza na paparazi wetu na alipogusiwa kuhusu
suala la Uwoya kunaswa na Diamond, alicheka sana huku akimshangaa.
“Hahaha
sasa ndiyo nini tena, yeye si aliwahi kunisema mimi nakwapua mabwana?
Sasa leo imetokea kwake tena!” alisema Jokate.
Irene Uwoya.
Subscribe to:
Posts (Atom)