Mkutano wa 11 wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaendelea huko Dodoma na wabunge
wameendelea kujadili bajeti ya ofisi ya waziri Mkuu katika kikao cha 5.
Siku hizi watu wengi wamezoea kusikia malumbano ama vijembe wanavyotoleana
wabunge wetu, licha ya kuwa vinakuwa sehemu ndogo tu na
wanaendelea na hoja za kutusaidia watanzania, lakini bunge limekuwa
tofauti sana hasa kwa kuzingatia matumizi ya lugha na hata tafsiri ya
lugha hizo.Siku hizi watu wengi wamezoea kusikia malumbano ama vijembe wanavyotoleana
Leo asubuhi mbunge wa jimbo la Kondoa kusini Juma Suleiman Nkamia alimwambia mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) kuwa “kumbuka siongei na mbwa naongea na mwenye Mbwa”. Sentensi hii ilitamkwa na mbunge huyo baada ya kusikia sauti ya Sugu akijaribu kukataa kile alichokuwa anachangia bila kufuata utaratibu wa kunyoosha mkono ama kumuomba naibu spika, na ndipo alipomuomba kuwa na heshima kwanza kwa kumtaja kwa jina la ‘Sugu'