Sunday, April 14, 2013

TAMKO LA CHADEMA KUHUSU NJAMA ZA KUKICHAFUA ZINAZOFANYWA NA GENGE LA VIONGOZI WAKUU WA CCM NA VYOMBO VYA DOLA

Ndugu waandishi wa habari; 
LEO tumewaita hapa ili kuwaomba mtufikishie ujumbe kwa Watanzania, kwamba nikiwa mwanasheria na mtu ambaye nimepata ujuzi wa kazi za ushushu, nimefanya uchunguzi matukio haya ya utekaji na utesaji na kugundua mambo mengi mno.

Uchunguzi huu nimeufanya kabla na baada ya kukamatwa kwa Mkurugenzi wetu wa Ulinzi na Usalama, Willifred Muganyizi Lwakatare, ambaye hivi sasa anashitakiwa mahakamani kwa tuhuma za kupanga ugaidi. 


Nimefanya hivyo kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa langu na chama changu. Katika uchunguzi wangu huo, nimegundua mambo mengi ikiwamo kuwapo kwa genge la watu ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaopanga mipango hii ya kishetani na kisha kuwasingizia watu wengine. 


Angalieni mfano huu: Unaoitwa na polisi na Mwigulu Nchemba, “mkanda wa Lwakatare” unadaiwa uliwasilishwa jeshi la polisi Desemba mwaka jana. Lakini jeshi hilo halikumkamata yoyote wala kumhoji, hadi pale Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, alipovamiwa na kuumizwa. 

Aidha, Nchemba amedai kumiliki video ile Desemba mwaka jana, lakini rekodi hiyo iliwekwa kwenye mitandao ya kijamii (YouTube na Jamii Forum) baada ya kutekwa kwa Kibanda. Hapa mtu makini anaweza kujiuliza, hiki kimelenga nini?

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 
14 Aprili, 2013

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) ambaye amefariki dunia tarehe 14 Aprili, 2013 saa kumi na mbili na nusu asubuhi, katika Hosptali ya TMJ.

Pamoja na nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika Jeshini na Serikalini, Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) alikuwa Mkuu wa JKT wa tano. Kama mnavyofahamu umuhimu wa JKT, yeye ni miongoni mwa Makamanda walioleta tija kubwa katika kuwalea Vijana wa Kitanzania na kuwajengea nidhamu na uzalendo.

Mpango wa Mazishi unafanywa, mtajulishwa baadae juu ya wapi na lini atazikwa Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (Mstaafu). Msiba upo nyumbani kwake Mikocheni, karibu na nyumbani kwa Hayati Mwl J.K Nyerere.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI
ROHO YA MAREHEMU
Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (MSTAAFU) AMINA.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Chadema yatishia kujitoa mchakato wa Katiba Mpya

 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kitajitoa katika mchakato wa Katiba Mpya endapo mambo muhimu mawili hayatapatiwa ufumbuzi hadi kufikia Aprili 30, mwaka huu.

Wakati Chadema wakisema hayo, Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limesema uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba uliomalizika siku tatu zilizopita katika maeneo mbalimbali nchini haukuwa huru na ni batili, huku likipendekeza urudiwe katika maeneo yote yaliyokumbwa na kasoro.


Katika hoja zake, Chadema kimesema kinataka kufutwa kwa uteuzi/uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata na badala yake wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya wachaguliwe moja kwa moja na wananchi wa Kata husika bila kuchujwa na Kamati za Maendeleo za Kata (WDC).

Msimamo huo ulitolewa na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati akisoma hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2013/14 huku akiitaka Serikali kuwasilisha muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ili maeneo kadhaa yafanyiwe marekebisho.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRIL 4

DSC 0552 0051d
DSC 0550 b42a5
DSC 0551 29f07

MWANAMKE ANUSURIKA KUUAWA NA PADRI AMBAYE NI MPENZI WAKE HUKO KIBAHA......!!

  ( picha na maktaba)

Bi Celestina Ananius(35) amenusurika Kuuawa na Padri   wa kanisa katoliki parokia ya Hombolo iliyoko Dodoma kwa jina la Celestine John Nyaumbana  ambaye kwa Sasa anaishi kwenye Makazi ya Katoliki Mbezi kwa ajili ya Masomo.

Dada huyo anasema amekuwa katika mapenzi  na padri huyo tangia akiwa Fratel, akawa Shemasi na sasa ni padri na suala hilo ni siri yao na wazazi wa pande mbili hadi wamezaa mtoto anaitwa Agnes (3).

Bi Celestina ambaye anaishi Dodoma alikuja Dar kumfuata Mpenzi wake huyo ili  ajue  hatima  ya  huyo  mtoto  wao....

Sasa wakati wapo Dar padri huyo alimuomba mpenzi wake huyo watoke kidogo kwenda kutembea maeneo ya Kiluvya...
Walipofika  huko wakati wapo katikati ya pori padri huyo alishuka kwenye gali na kumshambulia dada huyo  kwa madhumuni ya kumuua na kupoteza ushaidi ila hakufanikiwa kumuua .....

Taarifa za Polisi Mkoa wa Pwani zinaonyesha kuwa Mwanamke huyo aliokolewa na Wasamalia wema na kukimbizwa Hospitali ya Tumbi Kibaha kwa matibabu!!!

 source: Police Kibaha  na  Wapo radio kipindi cha Patapata

MAJID MJENGWA NAYE AKAMATWA NA POLISI AKIHUSISHWA NA SAKATA LA KIBANDA.....!!

Majid Mjengwa.
MWANDISHI wa safu katika magazeti mbalimbali nchini, Majid Mjengwa amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda.
Habari zilizoufikia mtandao huu jana mchana na baadaye kuthibitishwa na polisi zinasema Mjengwa alikamatwa muda wa asubuhi na kwamba alikuwa akihojiwa na makachero wa jeshi hilo hadi alasiri kuhusu tukio la kuteswa kwa Kibanda.

Msemaji Mkuu wa Polisi Advera Senso alisema kwamba:

“Ni kweli kwamba tunaye, tunaendelea kumhoji, tunachoomba ni kwamba mtupe nafasi ili tufanye kazi yetu na kukiwa na jambo lolote tutawajulisha.”

Saturday, April 13, 2013

ANGALIA PICHA IKIWAONYESHA ODINGA AKIWA NA KENYATTA IKULU NA WALIOKUA WAGOMBEA WENZA WAO

Picture
Picha: L-R: Uhuru, Ruto, Raila, Kalonzo katika Ikulu ya Nairobi leo, Aprili 13, 2013
RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta na na Naibu wake William Ruto, leo wamekutana na kushauriana na wakuu wa chama cha CORD Raila Odinga na Kalonzo Musyoka waliowatembelea Ikulu Nairobi kuwatakia heri.

PADRI ALIYEOA KWA SIRI AFUNGWA JELA MIEZI 6 ...!!!

KUSHOTO: Padri William akimbusu mkewe, Beverley. KULIA: Kanisa la Mt. Clara ambamo Padri huyo alibambwa akifanya uchavu wake kwa binti wa miaka 17.

Padri mmoja wa kanisa Katoliki ambaye alifunga ndoa kwa siri amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela jana kwa kumsumbua msichana mdogo kwa kile jaji alichoelezea 'uvunjifu mkubwa wa uaminifu'.


William Finnegan, akifahamika kama 'Fadha Bill', alimpapasa binti huyo mwenye miaka 17 chini na kulazimisha kumbusu kwa nguvu katika Kanisa Katoliki la Mt Clara mjini Bradford siku ya Jumapili ya Pasaka mwaka jana.

Jaji Roger Thomas alisema kwamba Padri huyo mwenye miaka 60, alikiri wakati wa kesi hiyo kwamba alifunga ndoa kwa siri miaka 14 iliyopita.

Pia alitumia maneno makali kwa wanaparokia wa Finnegan ambao walikuwa upande wake licha ya mashitaka hayo, akisema: "Pengine baadhi yao wanaweza kuamini kesho jua litachomoza magharibi kesho kama akisema hivyo."

YUSUPH MLELA AMTUNDIKA MIMBA MWANAFUNZI NA KUMLAZIMISHA AITOE....!!

STAA wa filamu za Kibongo, Yusuph Mlela amedaiwa kumtundika mimba mwanafunzi aliyefahamika kwa jina moja la Salha, mkazi wa Zanzibar ambaye anasoma katika chuo cha ITF, Tandika, jijini Dar.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja  kilichopo chuoni hapo, Mlela alidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na denti huyo kwa muda mrefu ambapo mashosti wote wa Salha, walikuwa wakimtambua kama shemeji yao hadi alipodaiwa kumpa kibendi.

 “Unajua shemeji yetu (Mlela) alikuwa anakuja sana hapa chuoni lakini baada ya kuambiwa yule Salha ana ujauzito wake, aliruka viunzi na kusema hahitaji mtoto, atoe mimba.


“Salha alipokataa ndipo Mlela alipoamua kukata mguu kabisa, tukawa hatumuoni,’’ kilisema chanzo hicho.


Alipotafutwa Mlela kuhusiana na ishu hiyo, alimkana mwanafunzi huyo na kusema hamtambui na wala chuo  anachosoma hakijui.


“Huyo msichana simjui hata hicho chuo chenyewe cha Tandika sijawahi kufika huko,  kama huyo binti ana ushahidi auweke hadharani,’’ alisema Mlela.

MWENYEKITI WA CHADEMA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA JELA KWA WIZI WA MIL. 1.2


Mwenyekiti wa chadema, mtaa wa Isamilo kaskazini B wilayani Nyamagana Philbert Bulinjiye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kujipatia shs milioni 1,250,000 kwa njia ya udanganyifu.

Hukumu hiyo, imetolewa na hakimu Vaineth Mahizi wa mahakama hiyo, kufuatia kesi ya jinai namba 196/2012, iliyofunguliwa na Vedasto Mavubhi ambaye alimtuhumu mwenyekiti huyo kuchukua kwake kiasi hicho cha fedha, kwa ajili ya kumuuzia kiwanja. 

Hakimu Mahizi katika hukumu yake, alidai ameridhika na ushahidi uliotolewa na upnade wa mlalamikaji, mashahidi pamoja na wazee wa baraza hivyo kumhukumu mwenyekiti kwenda jela.
Alisema mwenyekiti huyo pamoja na Balozi Robert Byagaye wanastahili kutumikia kifungo hicho cha mwaka mmoja jela kutokana na kutiwa hatiani. 

"kitendo kilichofanywa na viongozi hawa, kuwaibia raia wanaowaongoza kiutapeli kwa kuwadanganya kuwauzia kiwanja na kisha kutafuta mtu bandia kwa madai kuwa kiwanja hicho kiko katika mtaa wanaouongoza, ni udanganyifu" Alisema hakimu na kuongeza kuwa Mwenyekiti huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa viongozi wengine matapeli.

SHAA AJILINGANISHA NA AKINA DIAMONDA & OMMY DIMPOZ

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sara Kaisi ‘Shaa’ amejinasibu kuwa kiwango alichonacho sasa hakina tofauti na wasanii wengine wakali kama Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na Nassib Abdul ‘Diamond’.
                                                     Shaa akifanya vitu vyake.
Shaa aliyabainisha hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hii aliyekuwa akitaka kufahamu kiwango cha fedha anachokipata katika shoo zake mbalimbali anazofanya.

“Hivi sasa kama mtu anaweza kumchukua Ommy ama Diamond kwa dau hilo analowapa, basi anaweza pia kunichukua mimi kwa shoo zake kwa kiwango cha nyota hao wawili, kwani uwezo ninao,” alisema.

Aliongeza kuwa ili kudumu katika fani ya muziki wa kizazi kipya, kunatakiwa kuongeza ubora wa kazi kwa kufanya kazi na wadau mbalimbali wa muziki wa ndani na nje ya nchi.
Shaa alisema kwa sasa wimbo wake wa ‘Lover Lover’ unaendelea kufanya vema katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini na Afrika Kusini, ambako video ya wimbo huo inachezwa zaidi.

MBUNGE ATAKA KILIMO CHA BANGI KIHALALISHWE TANZANIA

MBUNGE wa Nkasi,Ally Kessy (CCM) ametoa mpya bungeni baada ya kuuliza swali la kuitaka serikali ihalalishe kilimo cha bangi ili kujipatia fedha za kigeni.

Akiuliza swali la nyongeza jana, Kessy alisema kwa kuwa zao la tumbaku limekuwa likipigwa marufuku dunia nzima, lakini limendelea kulimwa na kuchangia pato la mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania, kwanini serikali isihalalishe kilimo cha bangi kama ilivyo kwa tumbaku ili kuchangia pato la taifa?
Swali hilo liliibua vicheko kwa wabunge wote, akiwemo Spika na Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula, Adam Malima.

Hata hivyo, Waziri Malima akijibu swali hilo alisema kuwa pingamizi dhidi ya zao la tumbaku duniani limepungua na zao hilo sasa ni moja ya mazao makubwa ya biashara.
Kuhusu bangi kuhalalishwa kuwa zao la biashara, Waziri Malima alisema kuwa katika nchi zingine imeruhusiwa kuwa moja ya zao la biashara na linachangia pato la taifa.

“Hapa nchini bado bangi haijaruhusiwa kuwa zao la biashara, lakini kama utafiti utafanyika na kubaini kama linaweza kupata soko la kuingizia pato taifa, tutaliangalia hilo,” alisema.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 13, 2013

.

.
.
.
.

Friday, April 12, 2013

MKE WA MTU ANASWA LIVE AKIFANYA MAPENZI NDANI YA GARI

KUFUATIA vitendo vya usaliti wa ndoa, uasherati, ufuska na ukiukwaji wa maadili ya Kitanzania kwa wanandoa, wiki iliyopita Ijumaa iliendelea na Operesheni Fichua Maovu kwa kuzunguka jijini Dar usiku wa manane na kunasa tukio la mke wa mtu akifanya uzinzi ndani ya gari.


Kabla ya kufanya operesheni hiyo, waandishi  walitaarifiwa kwamba Wilaya ya Kinondoni jijini Dar ndiyo inayoongoza kwa wake na waume  za watu kufanya vitendo vya ngono kwenye magari.


Maeneo yaliyodaiwa kwamba wazinzi hao hupenda kuyatumia ni Coco Beach, Leaders Club, Mlimani City na sehemu kubwa ya vitongoji vya Sinza na Mwenge, Dar.

WEMA SEPETU AMFIKISHA POLISI MAMA YAKE MZAZI


NI kivumbi! Kuna madai kwamba, staa wa Bongo asiyechuja, Wema Sepetu amemfikisha mama yake, Miriam Sepetu kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar kwa madai ya kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa samani mbalimbali....

Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilijiri usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.

Mbali na mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema aitwaye Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye inasemekana ni mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa msanii huyo.

“Wema alikuwa nyumbani kwake usiku huo, watuhumiwa hao wakamzukia na kuanza kumchapa makofi ya ‘kelbu’ ambapo katika mshikemshike huo, baadhi ya vitu vilivunjika na kumtia hasara staa huyo,” kilisema chanzo.

Haikujulikana mara moja ni kitu gani kilisababisha mama mzazi huyo, dada mtu na kijana asiyekuwa ndugu kwenda kwa Wema na kutenda kosa hilo.

Wema alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...