Saturday, April 13, 2013

MWENYEKITI WA CHADEMA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA JELA KWA WIZI WA MIL. 1.2


Mwenyekiti wa chadema, mtaa wa Isamilo kaskazini B wilayani Nyamagana Philbert Bulinjiye amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kujipatia shs milioni 1,250,000 kwa njia ya udanganyifu.

Hukumu hiyo, imetolewa na hakimu Vaineth Mahizi wa mahakama hiyo, kufuatia kesi ya jinai namba 196/2012, iliyofunguliwa na Vedasto Mavubhi ambaye alimtuhumu mwenyekiti huyo kuchukua kwake kiasi hicho cha fedha, kwa ajili ya kumuuzia kiwanja. 

Hakimu Mahizi katika hukumu yake, alidai ameridhika na ushahidi uliotolewa na upnade wa mlalamikaji, mashahidi pamoja na wazee wa baraza hivyo kumhukumu mwenyekiti kwenda jela.
Alisema mwenyekiti huyo pamoja na Balozi Robert Byagaye wanastahili kutumikia kifungo hicho cha mwaka mmoja jela kutokana na kutiwa hatiani. 

"kitendo kilichofanywa na viongozi hawa, kuwaibia raia wanaowaongoza kiutapeli kwa kuwadanganya kuwauzia kiwanja na kisha kutafuta mtu bandia kwa madai kuwa kiwanja hicho kiko katika mtaa wanaouongoza, ni udanganyifu" Alisema hakimu na kuongeza kuwa Mwenyekiti huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa viongozi wengine matapeli.

SHAA AJILINGANISHA NA AKINA DIAMONDA & OMMY DIMPOZ

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sara Kaisi ‘Shaa’ amejinasibu kuwa kiwango alichonacho sasa hakina tofauti na wasanii wengine wakali kama Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na Nassib Abdul ‘Diamond’.
                                                     Shaa akifanya vitu vyake.
Shaa aliyabainisha hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hii aliyekuwa akitaka kufahamu kiwango cha fedha anachokipata katika shoo zake mbalimbali anazofanya.

“Hivi sasa kama mtu anaweza kumchukua Ommy ama Diamond kwa dau hilo analowapa, basi anaweza pia kunichukua mimi kwa shoo zake kwa kiwango cha nyota hao wawili, kwani uwezo ninao,” alisema.

Aliongeza kuwa ili kudumu katika fani ya muziki wa kizazi kipya, kunatakiwa kuongeza ubora wa kazi kwa kufanya kazi na wadau mbalimbali wa muziki wa ndani na nje ya nchi.
Shaa alisema kwa sasa wimbo wake wa ‘Lover Lover’ unaendelea kufanya vema katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini na Afrika Kusini, ambako video ya wimbo huo inachezwa zaidi.

MBUNGE ATAKA KILIMO CHA BANGI KIHALALISHWE TANZANIA

MBUNGE wa Nkasi,Ally Kessy (CCM) ametoa mpya bungeni baada ya kuuliza swali la kuitaka serikali ihalalishe kilimo cha bangi ili kujipatia fedha za kigeni.

Akiuliza swali la nyongeza jana, Kessy alisema kwa kuwa zao la tumbaku limekuwa likipigwa marufuku dunia nzima, lakini limendelea kulimwa na kuchangia pato la mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania, kwanini serikali isihalalishe kilimo cha bangi kama ilivyo kwa tumbaku ili kuchangia pato la taifa?
Swali hilo liliibua vicheko kwa wabunge wote, akiwemo Spika na Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula, Adam Malima.

Hata hivyo, Waziri Malima akijibu swali hilo alisema kuwa pingamizi dhidi ya zao la tumbaku duniani limepungua na zao hilo sasa ni moja ya mazao makubwa ya biashara.
Kuhusu bangi kuhalalishwa kuwa zao la biashara, Waziri Malima alisema kuwa katika nchi zingine imeruhusiwa kuwa moja ya zao la biashara na linachangia pato la taifa.

“Hapa nchini bado bangi haijaruhusiwa kuwa zao la biashara, lakini kama utafiti utafanyika na kubaini kama linaweza kupata soko la kuingizia pato taifa, tutaliangalia hilo,” alisema.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 13, 2013

.

.
.
.
.

Friday, April 12, 2013

MKE WA MTU ANASWA LIVE AKIFANYA MAPENZI NDANI YA GARI

KUFUATIA vitendo vya usaliti wa ndoa, uasherati, ufuska na ukiukwaji wa maadili ya Kitanzania kwa wanandoa, wiki iliyopita Ijumaa iliendelea na Operesheni Fichua Maovu kwa kuzunguka jijini Dar usiku wa manane na kunasa tukio la mke wa mtu akifanya uzinzi ndani ya gari.


Kabla ya kufanya operesheni hiyo, waandishi  walitaarifiwa kwamba Wilaya ya Kinondoni jijini Dar ndiyo inayoongoza kwa wake na waume  za watu kufanya vitendo vya ngono kwenye magari.


Maeneo yaliyodaiwa kwamba wazinzi hao hupenda kuyatumia ni Coco Beach, Leaders Club, Mlimani City na sehemu kubwa ya vitongoji vya Sinza na Mwenge, Dar.

WEMA SEPETU AMFIKISHA POLISI MAMA YAKE MZAZI


NI kivumbi! Kuna madai kwamba, staa wa Bongo asiyechuja, Wema Sepetu amemfikisha mama yake, Miriam Sepetu kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar kwa madai ya kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa samani mbalimbali....

Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilijiri usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.

Mbali na mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema aitwaye Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye inasemekana ni mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa msanii huyo.

“Wema alikuwa nyumbani kwake usiku huo, watuhumiwa hao wakamzukia na kuanza kumchapa makofi ya ‘kelbu’ ambapo katika mshikemshike huo, baadhi ya vitu vilivunjika na kumtia hasara staa huyo,” kilisema chanzo.

Haikujulikana mara moja ni kitu gani kilisababisha mama mzazi huyo, dada mtu na kijana asiyekuwa ndugu kwenda kwa Wema na kutenda kosa hilo.

Wema alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.

JULIANA SHONZA AANIKA HADHARANI MATUKIO MAZITO YA CHADEMA YANAYOFANYWA GIZANI

WANASIASA wawili vijana ambao wamekuwa katika vita ya maneno na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, kuhusu madai waliyoyatoa kuwa anawindwa kuuawa, mwishoni mwa wiki iliyopita, walijitokeza katika ofisi za Mtanzania Jumatano na kufunua siri na matukio ya utesaji raia na mauaji ya kinyama ambayo yamekuwa yakitokea kwa nyakati tofauti kwenye shughuli za kisiasa hapa nchini.

Wanasiasa hao, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba, ambao wamefanya mahojiano ya ana kwa ana na gazeti hili, walisema madai waliyoyatoa awali kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa, alitajwa na kada wa chama hicho, Ben Saanane, kuwa alimtuma amuwekee sumu Zitto kwa lengo la kumuua ni ya kweli kwa sababu walimkamata akiwa nayo na alikiri jambo hilo na kumuomba msamaha Zitto kwa kitendo hicho.

Walidai, mbali na tukio hilo ambalo baada ya kuliibua limegusa hisia za wengi na kuzua mijadala mikali, yapo matukio mengine ya mauaji na majaribio ya kuua, ambayo yamekuwa yakiratibiwa na Chadema kwa lengo la kuwagombanisha wananchi na Serikali.

Shonza na Mwampamba walisema kuwa wapo tayari kutoa ushuhuda wa matukio hayo mahali popote watakapohitajika na walipoulizwa ni kwa nini baada ya kubaini kuwepo kwa vitendo hivyo, hawakutoa taarifa kwa vyombo vya sheria au taasisi za ulinzi na usalama, walisema mlengwa mkuu katika matukio hayo ambayo yalikuwa yakisababisha madhara kwa watu wengine hakuwa tayari siri hiyo kuanikwa.

CAG abaini ubadhirifu mkubwa


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha ulioishia 30 Juni, 2012 zilizowasilishwa bungeni jana mjini Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Rajab Mbarouk Mohammed. Picha na Edwin Mjwahuzi 

Dodoma. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ilitolewa jana ikiweka bayana madudu mbalimbali ya ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma, udhaifu katika usimamizi wa mikataba na Serikali kushindwa kutoa fedha zilizoidhinishwa na Bunge kwa ajili ya miradi ya maendeleo. 


Moja ya matatizo yaliyojitokeza ni Wizara ya Nishati na Madini kushindwa kukusanya nyongeza ya mrabaha wa madini baada ya kuongezwa kutoka asilimia tatu hadi nne.

TANZANIA YAPANDA KATIKA ORODHA YA FIFA

Na Mtandao
Kwa mujibu wa orodha ya FIFA ya ubora wa soka duniani iliyotolewa leo nchini Uswizi, zile timu zilizopo 3 Bora, Spain, Germnay na Argentina bado zimeshikilia nafasi zao.
Tanzania inayoongozwa na taifa stars chini ya kocha mkuu Kim Paulsen imepanda juu nafasi tatu na kujikita Nafasi ya 116.
Katika miezi miwili, Tanzania imepanda kwa kasi kutoka nafasi ya 127 mwezi machi na kwenda nafasi ya 119 mwezi Aprili na sasa imekalia nafasi ya 116 baada ya kushusha kipondo kwa Simba wasiofugika kutoka pwani ya magharibi mwa Afrika, timu ya taifa ya Cameroon bao 1-0 uwanja wa taifa, na baadaye kuwatungua simba wa milima ya Atlas, timu ya taifa ya Morroco mabao 3-1 katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia.
Wakati Tanzania ikipanda nafasi tatu juu, Simba watatu yaani timu ya taifa ya England imeporomoka nafasi 3 na sasa ipo nafasi ya 7 huku wazee wa Samba na waandaaji wa michuano ya kombe la dunia mwakani, timu ya taifa ya Brazil ikiporomoka nafasi 1 na sasa ipo ya 19.
Timu toka Barani Afrika ambayo iko juu sana ni Tembo wa pwani ya magharibi ya Afrika, timu ya taifa ya Ivory Coast iliyopanda nafasi 1 na sasa ipo nafasi ya 12.
Orodha nyingine ya timu bora za taifa duniani itatolewa na FIFA Mei 9 mwaka huu.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRIL 12, 2013

DSC 0082 d1df0

DSC 0080 b4ef5

HAYA NDIO MABEGI YA RIHANNA AMBAYO HUSAFIRI NALO POPOTE AENDAPO




JAY -Z KUNUNUA KISIWA KWA AJILI YA FAMILIA YAKE

Rapa nguli nchini Marekani Jay-Z amefanya kufuru baada ya kutangaza kuwa atanunua kisiwa chake binafsi katika eneo la la Bahamas, kwa ajili ya mapumziko na familia yake.

Vyanzo vya habari vilivyopo karibu na nyota huyo vilieleza juzi kuwa  ametenga pauni milioni mbili ili kununua eneo hilo lililopo kaskazini mwa wilaya ya Abaco kwa ajili ya familia yake.

Thursday, April 11, 2013

JOHARI AGOMA KUTINGISHA MAUNO YAKE MBELE YA RAY


MKONGWE kwenye ‘Industry’ ya Filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ alitoa kali ya aina yake baada ya kukataa kuzungusha nyonga mbele ya mwigizaji mwenzake, Vincent Kigos ‘Ray’ anayedaiwa ni mpenzi wake

Tukio hilo lililonaswa na mwandishi wetu juzikati, lilitokea katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar wakati wasanii hao walipojumuika pamoja kwa ajili ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kitokee kifo cha msanii mwenzao, Steven Kanumba.

Akiwa viwanjani hapo, Johari aliitwa kupanda jukwaani na wasanii wenzake kwa ajili ya kucheza sebene kidogo lakini yeye alikataa na mwandishi wetu alimsikia akijitetea kuwa hawezi kukata nyonga mbele ya wasanii wenzake hususan Ray ambaye ni bosi mwenzake kwenye kampuni yao ya RJ Company.

“Siwezi kujidhalilisha mbele ya umati huo kwa kukata kiuno tena na bosi mwenzangu yupo pale, labda ningekuwa nimelewa kiasi cha kutojitambua hapo ningefanya madudu kama hayo,” alisema Johari.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, MULUGO ATANGAZA VITA NA WAZUSHI WAKE

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema atawafikisha mahakamani watu wanaodai kuwa ameghushi vyeti vya elimu ya sekondari. Mulugo alisema amechoshwa na kashfa hizo zinazosambazwa na baadhi ya watu atawafikisha mahakamani endapo wataendelea kumdhalilisha.

Mulugo alitoa kauli hiyo alipofungua mkutano wa mwaka wa Umoja wa Wamiliki wa Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania (TAMONGSCO0) jijini Mbeya.

“Wanasema eti nimeghushi vyeti, mara ooh sijui natumia jina la mtu. Nimechoshwa na maneno haya… ni kweli nimerudia darasa kama walivyorudia watu wengine, kwa nini iwe tatizo kwangu. Hata hapa tulipo wapo wengi tu waliorudia darasa.

“Kama kweli ningekuwa nimeghushi vyeti hivi leo ningekuwa naibu waziri wa elimu? Sasa nimechoshwa, nitawachukulia hatua watu hawa, siwezi kusema ni lini nitafanya hivyo ila nitakapoamua nitaanza,”alisema.

Kwa miezi kadhaa sasa Mulugo amekuwa akidaiwa kughushi vyeti na kutumia jina la mtu ili kufikia kiwango cha elimu alichonacho madai ambayo alisema yanamchafulia jina katika jamii.

Kuhusu suala la matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, Mulugo alisema matokeo hayo mabaya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mmomonyoko wa maadili miongoni mwa wanafunzi.

Naye Ruth Mnkeni kutoka Dar es Salaam anaripoti kuwa Mlugo amezindua tovuti ya elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ijulikanayo kama Shule Direct.

Muluigo alisema kuzinduliwa kwa tovuti hiyo kutawafanya wanafunzi kupata maarifa mengi ya vitabu mbalimbali na kuinua kiwango cha elimu nchini

HALI TETE KWENYE SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC

Ndani ya Taasisi ya Utangazaji Tanzania(TBC) kwa sasa kuna mgogoro mkubwa sana unafukuta chini kwa chini ukihusisha pande mbili kuu, yaani Wafanyakazi wa kawaida na Uongozi wa juu wa shirika hilo, kuhusu madai yafuatao na huku wakitaka Mkurugenzi mkuu wa sasa wa TBC afukuzwe na bodi ya shirika hilo ivunjwe;

1/Ubaguzi katika kupewa vyeo, Posho na marupurupu(Suala la Itikadi, Ukanda na Udini linatajwa sana)

2/Kuruhusu wanasiasa(Viongozi wa serikali na makada wa CCM) kuingilia wanavyotaka kazi za kitaaluma katika utoaji wa habari hususani kuhariri(Kuchuja) habari.

3/Kutokulipwa malimbikizo ya madeni ya madai ya siku za nyuma.

4/Utendaji Duni na Mbovu wa Mkurugenzi mkuu Clement Mshana hadi kufikia kumpa jina la dhihaka la 'BOYA'

5/Vitisho vya kufukuzwa kazi kwa baadhi ya watumishi wanaohoji sana mwenendo mbovu wa shirika hilo kwa sasa.

6/Mvutano wa Chini kwa chini kati ya Wakurugenzi waliowekwa na Lowassa wakati akiwa waziri mkuu na wapya walioletwa na Pinda.

*Pia kuna issue ya mkataba tata(White Elephant) kati ya TBC na Startimes(Wachina!) ambao Terms, Conditions, Investment, Dividend na Shares havijawekwa wazi na sawasawa, japokuwa Mkurugenzi mkuu na Bodi yake ya sasa wanadai wameurithi tu lakini sio 'wapishi' kamili wa hicho kilichopikwa!!

source: JF

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...