Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh (katikati),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya
ukaguzi ya mwaka wa fedha ulioishia 30 Juni, 2012 zilizowasilishwa
bungeni jana mjini Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Rajab Mbarouk Mohammed. Picha
na Edwin Mjwahuzi
Dodoma. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ilitolewa jana ikiweka bayana madudu mbalimbali ya ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma, udhaifu katika usimamizi wa mikataba na Serikali kushindwa kutoa fedha zilizoidhinishwa na Bunge kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Moja ya matatizo yaliyojitokeza ni Wizara ya Nishati na Madini kushindwa kukusanya nyongeza ya mrabaha wa madini baada ya kuongezwa kutoka asilimia tatu hadi nne.