CAG
ameweka mezani taarifa yake asubuhi hii. Katika mkutano wa Kumi wa
Bunge, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Ukaguzi ya mwaka 2008
Kwa kubadilisha vifungu 38, 39 na 40 ambapo Serikali ingeleta majibu
yake sambamba na Taarifa ya CAG. Serikali haikuleta majibu hayo.
Wamevunja Sheria wakiisha nikiwa siku ya kwanza ya kuanza kutekelezwa
kwake. Spika alipowataka Serikali kutoa majibu, Mawaziri walibaki
kutazamana tu
Thursday, April 11, 2013
HATARI : WALA MAHINDI HATARINI KUDUMAA AKILI
WATAALAMU
wa masuala ya afya na kilimo kutoka mataifa mbalimbali duniani,
wamebaini mahindi, karanga na mihogo yenye sumukuvu ni moja ya vitu
vinavyochangia saratani ya ini, udumavu wa mwili na akili kwa watoto.
Ingawa takwimu sahihi hazijapatikana kuonesha madhara ya kila
Kutokana
na ukubwa wa tatizo, wataalamu hao kutoka nchi 20, wanakutana jijini
Dar es Salaam kwa siku tatu, kuanzia jana, kutafuta njia madhubuti za
kukabiliana na sumukuvu. Tanzania inatajwa kuwa miongoni mwa nchi
zilizochukua hatua za awali dhidi ya tatizo hilo.
Akizungumza jana katika ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi alisema,
“Lengo
la mkutano huu ni kuwapa fursa wataalamu kuja na mikakati
itakayoisaidia serikali na sekta binafsi kupambana na sumu ya aflatoxin
kwa kuwa hata hapa Tanzania ni tatizo kubwa.”
Dk
Mwinyi alifafanua kuwa, tatizo kubwa linaonekana kwenye mazao
yanayoathiriwa zaidi na sumukuvu ambayo ni mahindi, mihogo na karanga na
husababisha watumiaji kupata saratani ya ini na watoto hudumaa akili na
mwili.
Alisema
pamoja na serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwa na
sheria ya kudhibiti vyakula vinavyoingia nchini, lakini sheria pekee
haziwezi kumaliza tatizo hasa ikizingatiwa kuwa Watanzania wengi
wanatumia nafaka hizo wakati zikiendelea kukua shambani bila kuzipima
kiwango cha sumukuvu kinachotakiwa.
Sumukuvu
ni aina ya sumu inayosababishwa na kuvu katika mazao na ingawa
haiepukiki katika nafaka, kuna kiwango kinachopaswa kuwepo na
kinapozidi, huleta madhara hayo.
JK Atia Saini Kitabu cha Maombolezo ya Bi. Margaret Thatcher
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Jana, Jumatano, Aprili 10, 2013 ametia saini Kitabu cha Maombolezo cha
aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi. Margaret Thatcher ambaye
alifariki dunia Jumatatu wiki hii kwa ugonjwa wa kiharusi akiwa na umri
wa miaka 87.
Rais Kikwete ametia saini Kitabu hicho kwenye Ubalozi wa Uingereza katika Tanzania ulioko Jengo la Umoja mjini Dar es Salaam.
Rais
alikaribishwa kwenye Ubalozi huo na Balozi wa Uingereza katika
Tanzania, Mheshimiwa Bi. Dianna Melrose na wafanyakazi wengine wa
ubalozi huo na amekwenda moja kwa moja kutia saini kitabu hicho mara
baada ya kuwasili kwenye Ubalozi huo.
Wednesday, April 10, 2013
Irene Uwoya afunguka kuhusu skendo yake na Diamond.......!!!
Baada ya majaribio mengi ya kupiga simu yake ambayo ilikuwa haipatikani muda wote wa mchana baadaye kwenye mida ya saa kumi na mbili hivi jioni tuliweza kumpata hewani na Jibu lake lilikuwa moja tuu kuwa “achana nazo” na sisi tukaona kweli tuachane nazo ila tukufukishie wewe msomaji wetu mpendwa “response” hiyo ili mwenyewe uamue na kutafakari. Hilo ndo jibu alilotupa mwanadada mrembo wa bongo movies Irene Uwoya kuhusu tuhuma za yeye kutoka kimapenzi na msanii Diamond.
Source:Bongo Movies
SHILOLE ANASA KWENYE PENZI LA MZUNGU...!!
Kwa mujibu wa shushushu wetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika hoteli moja maarufu jijini hapa ambapo Shilole alikuwa kwenye ziara ya shoo yake.
Ilidaiwa kuwa mara tu baada ya kumaliza ziara ya shoo, Shilole hakuondoka jijini hapa na badala yake alionekana sehemu tofauti akijivinjari na jamaa huyo ambaye uchunguzi wetu ulibaini kuwa ni bosi wa klabu moja maarufu ya usiku Kanda ya Ziwa.
Kabla ya kuondoka katika jiji hili la sangara na sato, Alhamisi iliyopita na ndege ya jioni, Shilole alinaswa kimalavidavi na Mtasha huyo Jumatano katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere wa Gold Crest kulipokuwa na maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Syria.
Shilole alishuhudiwa akifanyiwa ‘shopping’ ya kufuru na bwana huyo ambapo gazeti hili lilinasa mpango mzima ambapo lilipotaka kujua kama ni wapenzi, Mtasha huyo alijibu kwa kifupi sana: “No comment” (sina la kusema).
Kwa upande wake Shilole alipobanwa mbavu alifunguka: “Nisingependa kuongelea jambo hilo kwani sasa najipanga kimuziki zaidi, shopping ni mambo ya kawaida sana kwa hiyo ni vyema tukaongelea muziki wangu kwani shoo yangu ya Pasaka ilijaa mashabiki wa kufa mtu so nakubalika sana Mwanza na siku moja nitaweka makazi hapa.”
SHAA AAHIDI KUVUA NGUO ZOTE HADHARANI ENDAPO VIDEO YAKE ITAFIKISHA VIEWS 100,000
Kwa
waliokuwa na hamu ya kumuona huyu naye akiwa nusu uchi na
kivazi cha kuogelea tuu, huu sasa ni wakati wao.....
Coca
Cola pop Star maarufu kwa jina la Shaa amedai kuwa yupo
tayari kuvua nguo zake hadharani na kuyaanika maungo yake nyeti
na kubakiza kichupi cha kuogelea tu endapo video yake mpya
ya Lava Lava itafikisha views 100,000 katika mtandao wa youtube
Popout
“Lava
Lava Video imefikisha views 44,000+ leo.Endapo itafikisha 100,000
basi ntavua nguo zote na kuogelea coco beach mchana kweupe lets do,”Alitweet Shaa katika mtandao wa kijamii wa Twitta na kuongeza
“Niliitupia kiutani tu nikidhani in one day kupata views elfu50 ni ngumu…sasa naona watu wameniamkia! Kwa spidi hii…mmmh…noma,”
BUNGE KITANZINI LEO
Mchakato
wa marekebisho ya kanuni za Bunge umeibua mjadala mkali baina ya
wabunge, huku wengi wao wakieleza kuwa hatua hiyo ina lengo la
kulifanya Bunge kukosa meno ya kuisimamia Serikali.
Miongoni
mwa mambo yaliyozua mvutano katika kikao cha awali cha wabunge wote ni
suala la muda wa wabunge kuchangia bungeni na jinsi wanavyotakiwa
kupangwa kulingana na idadi yao kwa kila chama.
Bunge
linakusudia kuwasilisha azimio la kutaka kubadili kanuni ambazo
zilitarajiwa kuwasilishwa na Naibu Spika jana bungeni, lakini kutokana
na baadhi ya mapendekezo kupingwa, hatua hiyo iliahirishwa hadi leo.
HOTUBA YA RAIS WA KENYA MARA BAADA YA KUAPISHWA HII HAPA
PRESIDENT UHURU KENYATA
SPEECH
BY H.E. HON. UHURU KENYATTA, C.G.H., PRESIDENT AND COMMANDER-IN-CHIEF
OF THE DEFENCE FORCES OF THE REPUBLIC OF KENYA DURING HIS INAUGURATION
AND SWEARING-IN CEREMONY ON TUESDAY, 9TH APRIL 2013 AT THE MOI
INTERNATIONAL SPORTS COMPLEX, NAIROBI.
o Your Excellency Hon.Mwai Kibaki, C.G.H., M.P.;
o Your Excellency Daniel arap Moi;
o Your Excellencies, Visiting Heads of State & Government;
o Chief Justice Willy Mutunga;
o All our Invited Guests;
o Fellow Kenyans,
Let
me begin by thanking all Heads of State present and the representatives
of Heads of State for choosing to be here as a symbol of your continued
support and goodwill towards Kenyans.
I
particularly note, with gratitude, the large presence of our brothers
and sisters from across the continent. This is a clear indication of
your commitment to the Pan-African agenda. You have bestowed a great
honor on me and our country by being here. On behalf of the Kenyan
people I welcome all of you to Kenya. Karibuni Sana!Let me also
acknowledge with gratitude and respect the distinguished service of my
predecessors. President Mwai Kibaki, a true statesman and a great leader
who over the past 10 years has laid a firm foundation for the future
prosperity of our country. Asante sana Mzee. Shukrani nyingi sana.
YANGA WAKATAA RASMI MECHI ZAO KUONYESHWA BURE NA SUPER SPORT
Siku
moja baada ya shirikisho la soka nchini TFF kubadilisha ratiba ya
baadhi ya mechi za ligi kuu ya Tanzania bara ili kuweza kufanikisha
mpango wa kuonyesha mechi hizo kupitia kituo cha Supersport, klabu ya
Yanga kupitia makamu wake mwenyekiti Clement Sanga imesema haikubaliani
na mpango huo kwasababu haujafuata utaratibu na pia utaziingizia hasara
kubwa klabu zinazohusika na mpango huo.
Akizungumza
na mtandao huu Sanga alisema kwamba mpango huo wa kuonyesha mechi za
ligi kuu bure kwenye Supersport haupo katika kuzinufaisha vilabu bali
wahusika wengine wa mpango huo.
Tuesday, April 09, 2013
SKENDO YA ASKOFU PENGO KUUZA MADAWA YA KULEVYA YAITIKISA KANISA KATOLIKI............!!!
SKENDO kwamba Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, anafanya biashara ya madawa ya kulevya, ilitikisa kisha ikapoa, ila sasa Uwazi lipo kwenye nafasi nzuri ya kupasua jipu.
Januari mwaka jana, Pengo ndiye alikuwa wa kwanza kutamka hadharani kuwa anaambiwa anauza ‘unga’, kipindi hichohicho, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa ambaye alisema wanafanya kazi kisayansi.
“Kama jina la Pengo tunalo kwamba anauza madawa ya kulevya au hatuna, siwezi kutamka kwa sasa, hatutaki kupindisha ushahidi au kuvuruga upelelezi wetu,” alisema Nzowa.
Hata hivyo, hivi karibuni, Uwazi lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa vigogo wa jeshi la polisi nchini, aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini, akasema kuwa suala la Pengo lina utata ila siyo zito.
“Labda mimi nipasue jipu kwamba jina la Pengo halionekani katika orodha ya viongozi wa dini wanaochunguzwa kutokana na kashfa ya madawa ya kulevya,” alisema kigogo huyo.
Aliongeza: “Hata kwenye ule mkanda uliokwenda bungeni, ukionesha wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, Pengo haonekani. Tulishangaa sana aliposema anaambiwa anauza madawa ya kulevya.”...
Subscribe to:
Posts (Atom)