Weekend iliyopita comedian maarufu “Kupa” alifunga ndoa na mke wake
ambapo sherehe yao ilihudhuriwa na wasanii wenzake kibao kutoka
bongomovie unit. Cheki mpango mzima ulivyokuwa siku ya siku na wasanii
walivyopendeza kwenye party hiyo. Short list ya wasanii waliofika kwenye
party hiyo ambayo MC alikuwa Dr Cheni ni Ray,JB,Nisha,Irene
Uwoya,Wolper na wengine wengi.
Thursday, April 04, 2013
WEMA SEPETU AMSUPRISE MARTIN KADINDA KWA BOOOOOOONGE LA KEKI NA MSHIKO WA MAANA
ahahahhha a this woman is something Else.. baada ya kukurukakala zangu Wema sepetu aliniita nyumbani kwake.... as soon as i got there nitwishwa boooooonge la keki... You i was like whaaat? |
hakuishia hapo.... mkononi kashika nini hapo?? usisonye sasa... hahha |
SHILOLE, Q-CHILLAH WAFUMWA LAIVU WAKIWA KATIKA MAHABA
Aibu
hiyo ilitokea Machi 29, mwaka huu ambayo ilikuwa Ijumaa Kuu ambapo
wasanii hao walikuwa wakitoka Dar kwenda Mwanza kwa ajili ya kufanya
shoo siku ya Pasaka. Akilisimulia gazeti hili, shuhuda wetu aliyekuwemo ndani ya ndege hiyo (jina tunalo) alisema aliwaona Shilole na Q-Chillah wakiwa katika ‘malovee’ ambapo mara kwa mara walikuwa wakipigana mabusu kitendo kilichowafanya abiria wengine kuwakodolea macho yenye kuwashangaa. |
Airtel, Samsung wakubaliana kukuza soka la vijana: Airtel Rising Stars Awamu ya tatu kuanza mwishoni mwa mwezi huu
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel inayofanya kazi pamoja na kampuni ya
Samsung zimesaini makubaliano ya kushirikiana kudhamini mashindano
makubwa Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17.
Katika
mkataba huo wa mamilioni ya dola, Samsung pia itakuwa mtoaji rasmi wa
vifaa vya mawasiliano kwenye mpango huo wa mashindano maarufu kama
Airtel Raising Star (ARS) unaoendeshwa na Airtel.
Airtel
inatoa huduma za mawasiliano kwa simu za mkononi kwenye nchi 20 barani
Asia na Africa huku Samsung ikiwa ni miongoni mwa makampuni makubwa ya
vifaa vya kisasa vya elektoniki.
Chadema wamtuhumu Mwakyembe kutoa zabuni kinyume cha sheria
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtuhumu Waziri wa Uchukuzi,
Dk Harrison Mwakyembe kwamba alitoa zabuni ya ujenzi wa bandari ya
nchikavu kwa kampuni inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinyume
cha sheria za ununuzi. Chadema
walisema jana kwamba, kampuni hiyo ni Jitegemee Trading Company ambayo
ilipewa zabuni ya ujenzi wa bandari katika Viwanja vya Sukita pasipokuwa
na mchakato wa kushindanisha kampuni nyingine.
Mkurugenzi
wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila alisema:
“Mwakyembe aseme alitoa zabuni hiyo kwa Jitegemee kwa kuzingatia vigezo
gani? Kampuni ngapi zilishindanishwa katika mchakato huo na asipofanya
hivyo hastahili kukaa wizarani hapo bali alipelekwa Segerea gerezani
kwani ni kosa kubwa kutoa zabuni kinyemela.”
Hata
hivyo, Dk Mwakyembe, ambaye yuko jimboni kwake Kyela mkoani Mbeya
alipoulizwa kuhusu madai hayo alijibu na kukata simu; “Mimi nina kazi ya
kuongoza wizara na wao Chadema wana kazi ya kuchonga mdomo, hivyo
waache mimi niongoze Serikali.
MAUNO YA WOLPER YAWACHENGUA WATU UKUMBINI
Baada ya kuonesha vitu adimu ambavyo havikuoneshwa na staa yeyote kati ya waliomtangulia, wageni waalikwa walishangilia na kupiga makofi hadi aliporejea sehemu aliyokaa awali.
RAY ASALIMU AMRI JUU YA FILAMU YAKE INAYO SHUTUMIWA KUUDHALILISHA UKATOLIKI
Cover la filamu hiyo ya Sister Marry.
HATIMA
ya filamu ya mwigizaji, Vincent Kigosi ‘Ray’, Sister Mary iliyokuwa
imezuiwa kwa kudaiwa kudhalilisha ukatoliki, imefahamika kuwa mwigizaji
huyo amesalimu amri ya viongozi wa kanisa hilo.Kanisa Katoliki nchini
linaloongozwa na Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, liliizuia filamu hiyo
kwa kile kilichodaiwa kuwa ilikuwa ikionesha udhalilishaji kwa namna
ambavyo watawa wamevaa mavazi mafupi.
Baadhi ya vipande vilivyomo katika filamu hiyo.
Akipiga
stori na paparazi wetu, Ray amebainisha kuwa baada ya kuambiwa achomoe
vipande vingi kwenye filamu hiyo, ameona ni bora kuachana nayo kwani
hata akitoa haitaleta maana hivyo atakujairudia upya wakati mwingine. “Asilimia
85 ya filamu niliigizia kanisani na ndivyo walivyosema niviondoe, sina
ujanja kwa sasa nimeanza kushuti filamu nyingine kabisa ile labda nije
kuirudia upya hapo baadaye,” alisema Ray.
WAJUE WASANII SITA (6) WA BONGO FLEVA WENYE KUHESHIMIKA SANA TANZANIA.
1.LADY JAY DEE
Mwanadada
JIDE ama binti machozi ameweza kuongelewa sana kama msanii
anayeheshimika sana tanzania kutokana na idadi kubwa ya watu walio
hojiwa kumtaja yeye kama ndo mwana muziki mwenye kuheshimika sana
tanzania kwa upande wa muziki wa kizazi kipya
2.PROF J
3.FID, Q
Polisi Wavamia Nyumba Ya Diddy
Diddy
Polisi
na Helikopta mbili za polisi walivamia Nyumba ya Diddy iliyopo Los
Angelos Marekani Usiku wakuakia Leo . Lakini habari zilizotoka kwenye
vyomba vya usalama viliimbia TMZ kuwa tukio hilo lilikuwa la bahati
mbaya
Habari zilizotoka polisi ziliwaambia TMZ kuwa Kuna Mtu alipiga simu polisi kuwa ndani nyumba ya Diddy kuna mtu anarusha risasi.
Baadae
polisi na wakubwa wengine walipojua kuwa ni mchezo mwingine unaofanyiwa
wasani wakubwa marekani waliamukuondoka katika tuukio hilo.
TMZ
wanasema kuwa waliambiwa kuwa Tukio hilo lilikuwa limepangiwa kufanyiwa
kwa muigizajiSteve Carell ambapo nyumba yake ilikuwa imezungukwa na
Polisi wengi kwasababu ilikuwa karibu na nyumba ya Diddy.
Hapa ndio nje kwa Diddy
Inasemekana
Diddy sio staa wa kwanza kufanyiwa tukio hilo, kuna baadhi ya mastaa
walishawahi kufanyiwa hivyo kama vile nyumbani kwa wazazi wa Miley Cyrus
mwaka jana Walifanyiwa kitendo hicho hicho.
Polisi
wamesema kuwa matukio hayo yakutishia ya mekuwa ya kudumu na sugu sasa
wamesema watamshitaki kwa sheria kali kwa yeyote atakayefanya tena tukio
kama hilo.
Mauaji ya Padri: DPP, Polisi wakorogana
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim, ametupilia mbali uchunguzi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na kusema mtuhumiwa hana kesi ya kujibu mahakamani.
Padri
Mushi ambaye alikuwa Paroko wa Kanisa Katoliki Minara Miwili aliuawa
kwa kupigwa risasi Febuari 17, mwaka huu katika eneo la Beitrasi mjini
hapa akiwa ndani ya gari alipokuwa akielekea kuongoza misa ya Jumapili
katika Kanisa la Mtakatifu Theresia, mjini Zanzibar.
Baada
ya mauaji hayo, Rais Jakaya Kikwete alitoa kibali cha kukaribisha
maafisa wa FBI kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa
mauaji hayo na Machi 17, mwaka huu Jeshi la Polisi lilimkamata Omar
Mussa Makame kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
Wednesday, April 03, 2013
UWOYA NA NDIKUMANA WARUDIANA...ANGALIA PICHA ZAO MBILI WAKIWA KATIKA POZI LA MAHABA
BREAKING NEWzzzzzzzzzzzzzzz!!!! MPAKA WA TUNDUMA MBEYA WAFUNGWA KWA MUDA POLISI WATUMIA MABOMU
kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman
Taarifa kutoka Tunduma mkoani Mbeya zinadai kuwa hali si shwari katika eneo hilo kutokana na kuzuka kwa vurugu kubwa zinazodaiwa kusababisha na masuala ya kiimani ya nani achinje kati ya mkristo na Muislam . Mwandishi kutoka Tunduma mkoani Mbeya Moses Ng'wat anaripoti kuwa vurugu hizo zimeanza majira ya saa nne asubuhi kwa makundi ya vijana kuandamana mitaani na kuvutana kuhusu uamuzi wa viongozi wa dini ya kikristo Tunduma kuandika barua kwa mkuu wa wilaya kutaka kuruhusiwa kuchinja wakati wa pasaka.
PINDA AFUNGA MACHIMBO YA MORAMU
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyepoteza maisha kutokana na kuporomoka kwa udongo katika machimbo ya Moramu yaliyopo eneo la Moshono, Arusha.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana alitangaza kuyafunga rasmi machimbo ya moramu eneo la Moshono, Arusha hadi Serikali itakapoweka utaratibu mzuri wa shughuli mbalimbali za uchimbaji katika eneo hilo.
Hatua
hiyo ya Pinda imetokana na ajali ya watu 14 waliopoteza maisha baada ya
kufukiwa na kifusi juzi, wakati wengine wawili walijeruhiwa kwenye
ajali hiyo iliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na mvua zinazonyesha jijini
Arusha.
Pinda
alitoa agizo hilo alipotembelea eneo hilo pamoja na kuwajulia hali
majeruhi wawili waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mt Meru
CHANZO:MWANANHI.
Subscribe to:
Posts (Atom)