TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI ZINAZOONEKANA ZA MTOTO AYUBU HAPA NICHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI TUKUYU
|
Tuesday, April 02, 2013
RUNGWE MBEYA IMEENDELEA KUKUMBWA NA MATUKIO YA MAUAJI YA KUTISHA, TAHADHARI PICHA HIZI ZINATISHA.....!!
Rais Jakaya Kikwete Akutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Naibu Rais mteule wa Kenya MheWilliam Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya MheWilliam Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Monday, April 01, 2013
Mgodi wafukia wachimbaji Arusha; zaidi ya watu 18 wanahofiwa kufariki.. Wanajeshi wafanaya uokozi sasa na tayari mtu mmoja ameokolewa hai na wengine watatu wakiwa wameshakufa
Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akiwasili eneo la ajali mapema
Mwili
wa dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na
askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva
huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa
ndani ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram
asubuhi ya leo
KAMANDA MPINGA MATATANI
ADAIWA KUAMURU GARI LILILOBEBA MAZAO YA MISITU LIACHIWE.
Kutokana na tukio hilo, askari mwenye namba D.9523 Koplo Azizi wa kituo kidogo cha polisi Ikungi mkoani Singida ameingia matatani baada ya kulikamata gari hilo lenye namba za usajili T 271 BTR na trela namba T 686 BTX lenye urefu wa futi 40.
SIMULIZI YA ALIYENUSURIKA KIFO KUTOKA GHOROFA YA 15.
Fundi ujenzi, Yusuph Abdallah ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi), ameeleza jinsi alivyonusurika kifo baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Ijumaa iliyopita.
Rais Kikwete na Mkewe, Mama Salma Kikwete wakimpa pole Yusuph Abdallah katika Hospitali ya Muhimbili walipotembelea majeruhi wa ajali ya kuporomoka jengo la ghorofa 16. Picha na Muhidin Michuzi.
FUNDI ujenzi, Yusuph Abdallah ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi), ameeleza jinsi alivyonusurika kifo baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Ijumaa iliyopita.
Yusuph aliliambia Mwananchi akiwa wodini kwamba kilichomponya ni neema za Mungu kwani kabla jengo hilo kuporomoka yeye alikuwa ghorofa ya 15 kwenye jengo hilo katika Mtaa wa Indira Gandhi akiendelea na ujenzi.
Alieleza kuwa hakuwa anafahamu kinachoendelea, bali aliona ghafla jengo linaaanza kuporomoka, na baada ya hapo hakufahamu zaidi kilichotokea hadi alipojikuta yuko hospitalini.
OBAMA AENDA KANISANI KWA MIGUU NA FAMILIA YAKE SIKU YA PASAKA, TAZAMA PICHA HAPA
Rais Barack Obama akitembea kwa miguu na Familia yake kutoka White House across Pennsylvania Ave. hadi Lafayette Park. huku akiwa amemshikili mtoto wake wa pili Sasha mkono pamoja, Mkewe Michelle Obama na binti yao mkubwa Malia kuelekea katika Kanisa la St. John’s Episcopal liliopo Washington, DC ambapo walihudhuria katika Pasaka Siku ya Jumapili Machi 31, 2013. ( Official White House Picha na Pete Souza)
Rais Barack Obama na first lady Michelle Obama walipotembea kutoka White House na binti zao Sasha Obama, wa pili kutoka kushoto, na Malia Obama, kulia, wakitembea kwa miguu kupitia Lafayette Park kwenda katika Kanisa la St. John’s Episcopal kwa ajili ya Pasaka Siku Jumapili, Machi 31, 2013, Mjini Washington. (AP)
Obama alipokua akitembea Mitaa ya Lafayette Park hadi St. John's Episcopal Church Siku ya Jumapili , March 31, 2013, ndani ya Jiji la Washington. (Picha na Carolyn Kaster)
Obamas akitembea kupitia Lafayette Park kwenda Kanisasani kwajili ya Pasaka.
Rais wa Marekani Barack Obama na familia yake walipo maliza ibada katika Kanisa la St. John’s Episcopal kwa ajili ya Pasaka Siku Jumapili, Machi 31, 2013, Mjini Washington.
HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 MACHI, 2013
Ndugu Wananchi;
Naomba
nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na kunipa
fursa ya kuzungumza nanyi kwa kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa kila
mwisho wa mwezi. Leo ninayo mambo matatu ninayopenda kuzungumza nanyi.
Ziara ya Rais wa China Nchini Tanzania
Ndugu wananchi;
Jambo
la kwanza ni ziara ya Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa
China aliyoifanya nchini kwetu kati ya tarehe 24 na 25 Machi, 2013.
Lengo la ziara yake ilikuwa kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo
kati ya China na Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru
wakazi wa Dar es Salaam kwa kumpokea vizuri mgeni wetu na ujumbe wake.
Wameondoka wakiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu na watu wake.
MKAPA ASEMA:TUSITANGULIZE UDINI KWENYE KATIBA
Ujumbe
wa amani na tahadhari ya umakini kwenye utoaji maoni kwenye Katiba
ndiyo vilitawala wakati wa misa za Sikukuu ya Pasaka zilizofanyika
sehemu mbalimbali nchini jana na juzi.
Miongoni mwa waliotoa hotuba wakati wa sikukuu hiyo ni
pamoja
na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ambaye alikuwa mkoani
Mtwara; na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliyekuwa jijini Dar es
Salaam.
Mkapa akataa udini
Rais mstaafu Mkapa alitumia fursa ya kutoa salamu katika Kanisa
Katoliki mjini Masasi kuliasa taifa kujiepusha na utoaji wa maoni ya
Katiba kwa misingi ya dini.
Mkapa alisema katiba ijayo haipaswi kuwa na itikadi za kidini kwa kuwa zinaweza kuliangamiza taifa.
WANAUME BONGO MOVIE HAWANA MAPENZI YA KWELI: SNURA
MKALI
wa filamu na muziki Bongo, Snura Mushi amesema anaogopa kuingia kwenye
uhusiano wa kimapenzi na wasanii wa filamu kwani wengi wao hawana
mapenzi ya kweli.
Akipiga
domo na paparazi wetu, Snura alisema tangu aanze kucheza filamu
alijiapiza kuwa kamwe hatajiingiza kwenye mapenzi na waigizaji zaidi ya
kushirikiana nao katika kazi ya kuzalisha filamu.
“Mimi siwapendi wanaume wasanii wa filamu, sijawahi kuwa nao labda awe msanii wa Bongo Fleva,” alisema Snura.
“Mimi siwapendi wanaume wasanii wa filamu, sijawahi kuwa nao labda awe msanii wa Bongo Fleva,” alisema Snura.
MAKAHABA RAIA WA RWANDA MATATANI DODOMA
WANAWAKE watatu raia wa Rwanda wanaosadikiwa kuendesha biashara ya ukahaba mjini Dodoma wamekamatwa na
kupewa siku tatu kuondoka nchini, huku wawili kati yao wakikutwa na vidonge vya kupunguza makali ya virusi ya Ukimwi (ARVs).
Sunday, March 31, 2013
ANGALIA PICHA YA KHANGA MOJA WAFUNIKA USIKU WA IJUMAA KUU NA MASHUJAA BAND
Rapa
wa bendi ya Mashujaa, Saulo John 'Fagason', akirap na kumchezesha mmoja
wa wasanii wa kundi la Khanga moja, wakati walipofanya shoo ya pamoja
kwenye Ukumbi wa Green Acres, Victoria usiku wa Ijumaa Kuu na
kuwapagawisha vilivyo mashabiki wa bendi hiyo.
Kiongozi
wa bendi ya Mashujaa, Chalz Baba (wa pili kushoto) akiwaongoza waimbaji
wa bendi hiyo kushambulia jukwaa wakati wa onyesho lililofanyika kwa
pamoja na kundi la Khanga Moja, katika ukumbi wa Green Acrers uliopo
Victoria jijini Dar es Salaam, usiku wa Ijumaa Kuu.
Mnenguaji wa kundi la Khanga moja akionyesha umahiri wake wa 'Miuno Miuno, jukwaani
Wanenguaji wa bendi hiyo ya Mashujaa, wakishambulia jukwaa wakaati wa onyesho hilo.
Mashambulizi yanaendelea jukwaani...
NA SUFIANI MAFOTO
RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAJERUHI WALIOUMIA KATIKA GHOROFA LILILOPOROMOKA DAR ES SALAAM
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bw.
Yusuf Abdallah ambaye ni mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo
lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya
watu 25, katika wodi ya Sewa Haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam. kushoto ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),
Mhe. Hawa Ghasia.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika
wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na
kumpa pole Bw. Selemani Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika
jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha
vifo vya watu 25 Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala,
Mhe. Raymond Mushi Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya
Moi.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika
wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na
kumpa pole kijana Baqir Dhamji, mmoja wa majeruhi walionusurika katika
jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha
vifo vya watu 25. Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya
MOI.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi
ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
jijini Dar es salaam wakimpa pole kijana Mohamed Ally Dhamji ambaye ni
miongoni mwa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka
katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25.PICHA
NA IKULU.
ANGALIA PICHA ZA KANGA MOKO WA KANDA YA ZIWA
Subscribe to:
Posts (Atom)