Sunday, March 31, 2013

MLEMAVU AMWANGUKIA WEMA SEPETU

Na. Mwandishi Wetu
MPIGAPICHA wa kujitegemea  ambaye ni mlemavu wa miguu wa mjini hapa, Elias Ngole Ngoswe amemwangukia msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu kwa kumuomba msaada ili aweze kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza na mwandishi wetu Jumanne iliyopita, Ngoswe ambaye ulemavu wake ulitokana na kugongwa na gari kwenye mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe, Februari 2, mwaka jana na akavunjika miguu na mfupa wa nyonga, alisema uamuzi wake wa kumuomba msaada Wema unatokana na kuvutiwa kwake na msaada aliompa  msanii mwenzake, Kajala Masanja ambaye alimuokoa kufungwa jela kwa kumtolea faini.
 
“Nimegundua kuwa Wema ana huruma sana nami nikaamua nimuombe msaada kupitia gazeti hili kwani nina matatizo mazito. Nilipovunjika miguu na nyonga nilikimbizwa Hospitali ya Wilaya Magunga, Korogwe baadaye nikahamishiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha, nikalazwa miezi mitatu baadaye nilihamishiwa Muhimbili ambako bei niliyoandikiwa nilipe imenishinda,” alisema Ngoswe.

Kwa mujibu wa hati ya malipo ya Muhimbili ya Septemba 10 mwaka jana (nakala tunayo), Ngoswe alitakiwa alipe gharama za matibabu shilingi 9,798,250 ambazo hana.
“Ni fedha nyingi sana ambazo kutokana na ugumu wa maisha, nimeshindwa kulipia. Namuomba Wema na watu wengine wenye huruma wanisaidie ili nitibiwe,” alisema kwa masikitiko Ngoswe. Wema au yeyote aliyeguswa na habari hii awasiliane naye kwa namba 0766 224 284 na Mungu atawabari

Maaskofu waijia juu Serikali

Wakristo wamesema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeshindwa kuwasaidia ili waishi kwa amani na utulivu katika nchi yao.

 
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu 
Kauli hiyo ilitolewa jana na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu, wakati akisoma tamko la Maaskofu wa madhehebu ya Kikristo Tanzania katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa lililopo eneo la Jamatini.
Katika tamko hilo alilolisoma kwa niaba ya Maaskofu wote, Kinyunyu alisema kuwa umefika wakati ambao Wakristo wamechoka na vitendo wanavyofanyiwa na baadhi ya waumini wa dini zingine.

“Tatizo ni kuwa Serikali inashindwa kuchukua hatua mapema, makanisa yanachomwa, migogoro inazidi, lakini hakuna hatua zozote ambazo Serikali inachukua katika kunusuru hali hiyo, tumechoka,” alisema.

“ Serikali imeshindwa kuchukua hatua kwa muda mwafaka kwa kila jambo ambalo linatokea kwa Wakristo na hata inapoonyesha kuwa imechukua hatua haionyeshi sana kujali juu ya yale wanayofanyiwa Wakristo. Askofu huyo alisema kuwa matokeo yanayotokea Zanzibar mathalan, Wakristo wanaoishi huko yamewasababishia hofu hivyo wengi kuanza kuvikimbia visiwa hivyo na kukimbilia Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa Askofu Kinyunyu, suala la uchomaji wa makanisa hadi sasa limeshindwa kupatiwa ufumbuzi na kila kukicha bado makanisa yanaendelea kuchomwa moto akahoji Serikali kukaa kimya maana yake nini.
Aidha, tamko hilo limeitaka Serikali kuweka utaratibu mzuri na ufafanuzi wa kina kuhusu uchinjaji wa nyama ambao umekuwa ni tatizo kubwa hapa nchini. “Hapa litolewe tamko kila mtu kwa imani yake achinje mwenyewe siyo kuanza kulaumiana au kumpa haki mmoja akachinja na mwingine akaachwa. Tunaomba sana ufafanuzi wa kina juu ya suala hilo ili kuondoa mgogoro baina yetu na wenzetu.”
wamekuwa wakifanyiwa, lakini akasisitiza kuwa wanatakiwa kupigana kwa maombi na ndiyo silaha kubwa ya ushindi.

Katika hatua nyingine, wakati Wakristo wakiwa na hofu ya kusherehekea Sikukuu ya Pasaka watu wasiofahamika wamevamia makanisa matatu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Kaskazini na kuvunja ofisi za wachungaji na wainjilisti.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Kuhusu sikukuu ya Pasaka

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA

Anuani ya Simu
“MKUUPOLISI”

Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734

Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556
S.L.P. 9141,

28/03/2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

1. KATIKA KUELEKEA SIKUKUU YA PASAKA, INAYOTARAJIWA KUADHIMISHWA KUANZIA TAREHE 29 MACHI HADI TAREHE 1 APRILI, 2013. JESHI LA POLISI LINAPENDA KUWAONDOA HOFU WANANCHI WOTE KUWA LIMEJIPANGA KIKAMILIFU KATIKA KUIMARISHA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO KWA KIPINDI CHOTE CHA SIKUKUU NA BAADA YA SIKUKUU, HIVYO WANANCHI WASHEREKEE SIKUKUU KWA AMANI NA UTULIVU, PASIPO VITENDO AMA VIASHIRIA VYOVYOTE VYA UVUNJIFU WA AMANI.

2. IKUMBUKWE KUWA, WANANCHI WENYE IMANI YA KIKRISTO NA HATA MADHEHEBU MENGINE HUTUMIA MUDA HUO KWENDA KUABUDU PAMOJA NA MUENDELEZO WA SHEREHE HIZO KWENYE MAENEO MBALIMBALI YA STAREHE. UZOEFU UNAONYESHA KUWA BAADHI YA WATU HUTUMIA KIPINDI HICHO CHA SIKUKUU KUFANYA MATUKIO YA UHALIFU KUTOKANA NA MIKUSANYIKO HIYO YA WATU KATIKA MAENEO MBALIMBALI.

3. JESHI LA POLISI LINAPENDA KUWAONDOA HOFU WANANCHI NA WAUMINI WOTE KUWA, ULINZI UMEIMARISHWA KWENYE MAENEO YOTE YA KUABUDIA, FUKWE ZA BAHARI, SEHEMU ZA STAREHE NA MAENEO MENGINE YOTE AMBAYO YATAKUWA NA MIKUSANYIKO MIKUBWA YA WATU.AIDHA, TUNAPENDA KUWATAHADHARISHA WALE WOTE AMBAO WATAKUWA WAKITUMIA BARABARA, KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA HASA KWA MADEREVA KUEPUKA KWENDA MWENDO KASI NA KUTUMIA VILEVI WAWAPO KAZINI.

4. VILEVILE, JESHI LA POLISI LINAWATAKA WANANCHI KUONDOA HOFU NA KUWAPUUZA WATU WACHACHE AMA KIKUNDI CHA WATU WANAOTUMIA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU KUWATIA HOFU KWA KUSAMBAZA MESEJI ZA VITISHO KWA WATU MBALIMBALI KWA LENGO LA KUVURUGA AMANI NA UTULIVU KATIKA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU. KITENDO HICHO CHA KUSAMBAZA MESEJI ZA VITISHO KWA WANANCHI NI UHALIFU KAMA UHALIFU MWINGINE NA WAKIBAINIKA HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.

5. KATIKA KUHAKIKISHA USALAMA KWENYE KUMBI ZA STAREHE, WAMILIKI WA KUMBI HIZO WAZINGATIE UHALALI NA MATUMIZI YA KUMBI ZAO KATIKA UINGIZAJI WA WATU KULINGANA NA UWEZO WA KUMBI HIZO, BADALA YA KUENDEKEZA TAMAA YA FEDHA KWA KUJAZA WATU KUPITA KIASI. VILEVILE, WAZAZI WAWE MAKINI NA WATOTO WAO NA HASA DISKO TOTO, ILI KUEPUKA AJALI NA MATUKIO MENGINE YANAYOWEZA KUSABABISHA MADHARA JUU YAO.

6. JESHI LA POLISI LINATOA TAHADHARI KWA WANANCHI WOTE KWAMBA, WATOKAPO KWENYE MAKAZI YAO WASIACHE NYUMBA WAZI AMA BILA MTU NA WATOE TAARIFA KWA MAJIRANI ZAO, NA PALE WANAPOWATILIA MASHAKA WATU WASIOWAFAHAMU WASIKAE KIMYA BALI WATOE TAARIFA KWA JESHI LA POLISI AU VIONGOZI WAO WA SERIKALI YA MTAA, SHEHIA, KIJIJI AU KITONGOJI ILI HATUA ZA HARAKA ZIWEZE KUCHUKULIWA.

7. MWISHO, NAPENDA KUWAHAKIKISHIA WANANCHI KWAMBA, JESHI LA POLISI LINATEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA KUZINGATIA SHERIA ZA NCHI NA HIVYO HALITAWAJIBIKA KUMWONEA HURUMA AMA UPENDELEO MTU YEYOTE ATAKAYEENDA KINYUME NA SHERIA ZA NCHI.
NAWATAKIENI WATANZANIA WOTE PASAKA NJEMA.

IMETOLEWA NA:
ADVERA SENSO
MSEMAJI WA JESHI LA POLISI (T)

Saturday, March 30, 2013

Uhuru Kenyatta ndiye rais halali wa Kenya

 
Willy Mutunga rais wa mahakama ya juu zaidi Kenya

Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya, imeamua kuwa rais mteule Uhuru Kenyatta atasalia kuwa rais mpya wa Kenya baada ya kusema kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia huru na ya haki.
Uchaguzi wenyewe ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ambapo hesabu ya kura ilimpa ushindi Kenyatta kwa zaidi ya laki nane.

Rais wa mahakama hiyo jaji mkuu Willy Mutunga alisema kuwa mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia ya huru na wazi na kuwa Kenyatta na mgombea mwenza wake walichaguliwa kihalali.

Katika hali ya kutatanisha Korea Kaskazini yatangza vita na Korea kusini.

Korea Kaskazini hii leo imesema inaingia katika hali ya vita na Korea Kusini, katika muendelezo wa vita vya maneno dhidi ya utawala mjini Seoul na Washington, baada ya kuwekewa vikwazo vya kimataifa kufuatia jaribio lake la silaha za nyuklia.
Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA, limetoa taarifa inayosema kuwa kuanzia sasa, uhusiano wa Kaskazini na Kusini utaingia katika hali ya vita, na kwamba maswala yote yanayojitokeza kati ya Kaskazini na Kusini yatashughulikiwa ipasavyo.
Tangu mwanzoni mwa mwezi huu Korea kaskazini imekuwa ikitishia kila siku kuishambulia Korea kusini pamoja na kambi za kijeshi za Marekani, baada ya Marekani na Korea Kusini kuanzisha mazoezi ya kawaida ya kijeshi na imeyaamrisha majeshi yake kukaa kwa tahadhari.
Korea kaskazini imetoa kitisho kipya kuishambulia Marekani, baada ya ndege mbili za Marekani chapa B-2 zenye uwezo wa kubeba makombora ya nyuklia kufanya mazoezi nchini Korea ya Kusini.

HUYU NDO BINTI ALIYECHEZEA KICHAPO KUTOKA KWA MPENZI WAKE BAADA YA KUBUSU KIFUA CHA DIAMOND

Binti uzalendo ulimshinda, akaenda kumnyonya matiti Diamond
Binti uzalendo ulimshinda, akaenda kumnyonya kifua Diamond
Binti huyo akilia baada ya 
kuvutwa na kuchezea kichapo kutoka kwa bwana wake

Binti huyo akilia baada ya kuvutwa na kuchezea kichapo kutoka kwa bwana wake
Binti alipokua kwenye show ya Diamond, uzalendo ulimshinda, akaenda kunyonya chuchu za diamond kama inavyoonekana pichani  Kitendo hicho kilimuudhi bwana wake, ambapo alimvuta binti huyo na kumchapa makofi. Katika picha ya pili, binti huyo anaonekana akilia baada ya kuchezea kichapo, huku akiwa amewekwa “chemba” na boyfriend wake.

"NYIE WALALA HOI MIE SIHESABU MATUSI NAHESABU MAHELAAAAAAAA.''MANGE KIMAMBI


 Mange Alikuwa Arusha Ambapo Alipeleka Vitu vya Kuuza Kutoka Ulaya Hizo ndio Picha na Maneno aliyoandika kwenye Website yake..........

HIKI NDICHO ALICHO ANDIKA....

"NYIE WALALA HOI MIE SIHESABU MATUSI NAHESABU MAHELAAAAAAAA...


MKIMALIZA KUTUKANA NJOONI NIWAPE AJIRA.

....LOLEST!!!!!

SIJIBISHANI NA WACHOVU...........


NDO KWANZAAAAA NATENGEZA MAHELAAA NA MUME ANANISUBIRI KWA HAMU,


MTACHONGA SANA HAACHWI MTU NA BONGOLICIOUS NDO MAMBO YOOOOTE.......


MWAKA HUU MTAISOMA NUMBERRRR.......


HATA MUONGEE NINI MIE NDO MANGE KIMAMBI NA MTAENDELEA KU KISS THE


GROUND I WALK ON........." Says Mange
SOURCE THE CHOICE

Chadema waonyesha picha za video alivyouawa Mwangosi

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
*Picha zinaonyesha jinsi RPC Iringa alivyoshuhudia tukio
*Zinaonyesha baada ya Mwangosi kuuawa, polisi walilaumiana
*Waandishi wa habari, viongozi wa Chadema waangua vilio
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeonyesha picha za mnato na video zinazoonyesha jinsi Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Television cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, alivyouawa.

Picha hizo zilionyeshwa jana jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichohudhuriwa pia na waandishi wa habari. Kikao hicho cha Kamati Kuu kilikuwa ni cha dharura na kilifunguliwa na kuongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Wakati picha hizo zikionyeshwa wazi wazi, viongozi wa CHADEMA na waandishi wa habari, walishindwa kujizuia kwani baadhi yao walijikuta wakiangua vilio wakionyesha kusikitishwa na jinsi Mwangosi alivyouawa.

Katika tukio hilo, Mbowe ni kati ya waliolia na ilifika wakati akanyanyuka kutoka meza kuu na kwenda nje ya ukumbi, ili asiendelee kushuhudia Mwangosi alivyouawa.

Afukua kaburi la mwanamke, atundika mtini nguo za marehemu

MKAZI wa Kijiji cha Itunge wilayani Kyela, Asanga Mwandepu (67) amefukua kaburi la mwanamke katika kijiji cha Kingila, akachukua nguo za marehemu na kuzitundika juu ya mti na kulima tuta la viazi kwenye kaburi hilo. Inadaiwa katika kaburi hilo alizikwa mwanamke Basikaja Nkemwa miaka mitatu iliyopita.

Akielezea tukio hilo mtoto mkubwa wa marehemu, Semu Mwakalebela alisema wazazi wake wote wamekwisha kufariki dunia.

Semu alisema alishangazwa na kitendo alichokumbana nacho cha kukuta kaburi la mama yake likifukuliwa na mfukuaji akitoa nguo za marehemu na kuzitundika juu ya mti.

Alisema alipiga mayowe kuomba msaada kwa majirani ambao walifika na kujionea kitendo hicho wakamkamata mtu huyo na kumfikisha kwenye ofisi ya serikali ya kijiji kabla ya kumfikisha polisi.

“Nashangazwa na kitendo hiki kwa maana mtu huyu analifahamu fika kaburi la mama yangu na hata yeye alishiriki katika mazishi hayo… sijui ni kipi kilichomsibu hadi kufikia uamuzi hao mgumu,’’ alisema Mwakalebela.
Mmwenyekiti wa Kijiji cha Kingila, Gwandumi Mwaipyana alisema serikali ya kijiji iliamua kumfikisha mtuhumiwa polisi ili sheria ifuatemkondo wake.

Alisema awali wazee wa mila wa kijiji hicho walikaa baraza lao na kumtaka mtuhumiwa huyo kutozwa faini ya Sh 400,000 kama adhabu lakinihakuwa na kiasi hicho lakini serikali ya kijiji ilishauri jambo hilo lishughulikiwe kisheria.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kajunjumele, Imani Mwailunga alisema suala hilo limeachiwa serikali kwa hatua za sheria.

Maiti 18 zaopolewa katika jengo lililoporomoka jana katikati ya jiji la Dar es Salaam

Jumla ya maiti 18 zimeopolewa katika kifusi cha jengo la ghorofa zaidi ya kumi lililopromoka jana asubuhi katika mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam, idadi hiyo ya watu waliopoteza maisha ikiwa ni ya kihistoria kwa majanga ya aina hii.

Mwili mmoja umeopolewa muda mfupi uliopita, ikiwa ni masaa kadhaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Meck Sadik kuthibitisha mapema asubuhi kwamba miili 17 ilikuwa imepatikana baada ya kazi za uokoaji ya usiku kucha na inayoendelea hivi sasa.

Makampuni kadhaa ya ujenzi yamejiunga katika zoezi hilo toka usiku kusaidia kuinua vifusi na kuopoa miili ya marehemu. Uwezekano wa kukuta mtu aliye hai hadi sasa ni mdogo sana wakati waokoaji wakiwa ni pamoja ya wanajeshi na vijana wa JKT wakiendelea na kazi.

Tutaendelea kuwapa Updates kila itapobidi.

Mola aziweke roho za marehemu mahala pema peponi - AMEN

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 30.03.2013

.
.
.
.
.
.

Lady Gaga anunua ‘wheelchair’ yenye dhahabu tupu

Siku zote Lady Gaga hupenda kuwa tofauti na kwa kuthibitisha hilo, amenunua baiskeli ya walemavu yenye dhahabu tupu iliyobuniwa na Ken Borochov kwaajili ya brand ya Louis Vuitton ambayo alionekana nayo mitaa ya Chicago jana.
article-2301275-18FEF183000005DC-721_634x868
Hiyo ilikuwa ni zawadi yake mwenyewe kwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 27 hiyo jana.
Gaga amekuwa akitumia wheelchair tangu February, baada ya kupata tatizo kwenye hips na hivyo kulazimisha kusitisha ziara yake ya Born This Way Ball na hatimaye kufanyiwa upasuaji.
Pamoja na kuwa mgonjwa, Lady Gaga ameendelea kuipromote perfume yake ya FAME. Pia albam yake ijayo iitwayo ARTPOP, itapatikana kwa awamu mbili miezi kadhaa ijayo.

UWANJA WA NDEGE WA SONGWE KUITWA JK, SUGU ANG'AKA


MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) amesema haungi mkono pendekezo la Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya kutaka kuuita Uwanja wa Ndege wa Songwe jina la Rais Jakaya Kikwete. 

Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Mbilinyi maarufu kama Sugu alisema mapendekezo hayo yametolewa na watu wenye kutaka kujipendekeza kwa mkuu wa nchi badala ya kufikiria kuutangaza Mkoa wa Mbeya katika nyanja ya kimataifa. 

Alisema Mbeya ina historia ya kutaka kujitangaza kimataifa na uwanja huo ni fursa pekee ya kufikia malengo hayo aliyoeleza kuwa yanataka kufifishwa na wateule wa rais. 

“Siungi mkono uwanja kuitwa kwa jina la JK, tunataka jina litakaloasisi uhalisia wa Mbeya nasi tufahamike kimataifa, kamati ya ushauri ya mkoa chini ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini, Norman Sigala ilikurupuka kuleta wazo hilo kabla ya kuwasiliana na wabunge,” alisema. 

Alisema hatua hiyo ya Sigala haiwakilishi mawazo ya wananchi bali inawakilisha mawazo ya mtu aliyeteuliwa na kwamba wao wakiwa wawakilishi wa Mkoa wa Mbeya kwa ridhaa ya wananchi hawawezi kukubaliana na suala hilo. 

Kauli ya Sugu iliungwa mkono na wabunge wengine wa Mkoa wa Mbeya, ambapo Mchungaji Lukson Mwanjale wa Mbeya Vijijini (CCM) alisema anasikitishwa na hatua hiyo ya kuliwasilisha wazo hilo bila ya kuwashirikisha wabunge. 

Alisema wakati wa kikao cha kamati ya ushauri wabunge wengi hawakuwepo na taarifa hizo walizisikia baada ya kusoma kwenye vyombo vya habari. 

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo ambaye pia ni mbunge wa Songwe, aliomba apewe muda wa kutaka kujua sababu zilizoibua wazo hilo. 

Wazo la kuuita Uwanja wa Ndege wa Songwe jina la Rais Jakaya Kikwete linazidi kupata upinzani ambapo awali chama cha NCCR-Mageuzi na kile cha PPT Maendeleo kupitia kwa viongozi wa Mkoa wa Mbeya vilipinga wazo hilo. 

:::TANZANIA DAIMA:::

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...