Friday, March 22, 2013

J MARTINS AFANYA COLLABO NA OMMY DIMPOZ, MWANA FA NA AY

 Kuanzia kushoto ni Mwana FA, AY (katikati), Ommy Dimpoz, J Martins na Marco Chali wakiwa kwenye studio za MJ Records

Mwanamuziki na producer mahiri wa nchini Nigeria, Martins Okey Justice aka J Martins yupo nchini na amefanya collabo na Mwana FA, AY na Ommy Dimpoz.
Inavyoonekana staa huyo amewashirikisha AY na Mwana FA kwenye wimbo mmoja uliotayarishwa na Marco Chali kwenye studio za MJ Records.

“Confirmed now @Realjmartins ft on @AyTanzania and @MwanaFA New Single coming out soon,” imesomeka tweet moja. 

Pia Ommy Dimpoz amemshirikisha staa huyo kwenye wimbo wake.“Finally @ommydimpoz did the Song with @Realjmartins (J.Martins) pic after the session,” imesomeka tweet nyingine ikiwa pamoja na picha.
Ommy Dimpoz akiwa ana J MartinsOmmy Dimpoz akiwa ana J Martins

Mwana FA na J MartinsMwana FA na J Martins
“Just left stu got an exclusive pre listening sesh of new @RealJMartins and @AyTanzania – INSAAAAANE #EastMeetsWest,” ametweet Vanessa Mdee.

KESI YA LWAKATARE: TUNDU LISU AMLAUMU "ISSA MICHUZI" NA " MWIGULU NCHEMBA


Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu leo amefanya mkutano wa wanahabari. Katika mkutano huo, Lissu ameongea yafuatayo:

1. Atafungua kesi Mahakama kuu kuiomba iiamuru Mahakama ya Kisutu kuendelea kusikiliza kesi ya awali iliyofutwa na DPP katika kesi inayomhusu Lwakatare kwani DPP amevuka mipaka yake inayomruhusu kufuta kesi na isitoshe kesi aliyofungua ni ile ile hivyo Mahakama iamuru shauri la awali liendelee.

2. Kuhusu video iliyoonyeshwa kwenye mitandao Lissu anasema kuna mashaka makubwa sana kuhusiana na video ile na kisheria kesi hiyo ikifika mahakamani haitachukua hata nusu saa ataibuka mshindi.
Lissu anasema
- Hakuna mtu anayepanga mauaji katika hadhara mahali ambapo watu wanapitapita kama inavyoonekana kwenye video ile.

-Lwakatare kama alirekodiwa basi lazima ielezwe je ilikuwa ni kwa hiari yake kama si hivyo ni makosa

-Issa Michuzi Mpiga picha wa Rais alikuwa akipongezana na watu wa Ikulu wenzake kuwa TISS (Usalama wa Taifa) wamefanya kazi nzuri kwa kurekodi ile video. Kisheria usalama wa taifa hawatakiwi wala hawaruhusiwi kurekodi au kuvifanyia ushushu vyama vya siasa kwa maslahi ya Chama tawala.

-Ludovick baada ya kukutana na Lwakatale tarehe 28 Desemba mwaka jana saa 5 muda mfupi baadaye yaani saa 5:59 alimpigia simuMwigulu Nchemba kwa kutumia namba ya simu ya Mwigulu ambayo ameiandikisha kwenye kumbukumbu na vitabu vya Bunge Lissu anadai wana rekodi ya mazungumzo yao.

-Siku iliyofuata tarehe 29 Desemba mwaka jana akiwa kwenye kipindi cha Tuongee asubuhi cha Star TV alidai ana mkanda wa video unaowaonyesha CHADEMA wakipanga mauaji.

-Pia amedai itabidi waambiwe video hiyo imerekodiwa studio gani, maneno gani yameondolewa na yapi yameongezwa.

Anamalizia kwa kusema walianza kwa kusema CHADEMA ni chama cha familia wakashindwa, wakasema ni chama cha wachaga wakashindwa, wakesema ni chama cha wakatoliki wakashindwa, wakasema ni chama cha wakristo wakashindwa, wakasema ni chama cha ukanda wakashindwa leo wanasema ni chama cha kigaidi WATASHINDWA.

(Picha / Habari na Kurugenzi Ya Habari Chadema)

Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala yakutana na Ofisi ya Bunge

IMG_0677Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala leo imekutana na Ofisi ya Bunge kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo ikiwa ni utekelezaji wa shughuli za kamati.  kama anavyoonekana Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba Sheria na Utawala Mhe. Pinda Chana akizungumza jambo katika kikao na watendaji wa Ofisi ya Bunge  wakati kamati hiyo ilipokutana na watendaji wa Ofisi ya Bunge kufuatilia utekelezaji wa majuku ya Ofisi hiyo.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. William Ngeleja
IMG_0704Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa kamati ya katiba, Sheria na Utawala wakati wa kikao na kamati hiyo iliyokutana na watendaji wa Ofisi ya Bunge kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali watu Bi. Kitolina Kippa.IMG_0694
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa kamati ya katiba, Sheria na Utawala wakati wa kikao na kamati hiyo iliyokutana na watendaji wa Ofisi ya Bunge kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo.

MTOTO WA MIAKA 12 APATA MTOTO.....ALIKUWA DARASA LA SABA


Mtoto Sean Stewart wa nchini Uingereza, amekuwa baba mdogo pengine kuliko wote duniani baada ya mpenzi wake kujifungua wiki hii mtoto wa kiume mwenye afya.


Sean aliyetimiza miaka 12 mwezi uliopita, aliruhusiwa kutoenda shule ili kuwa pembeni ya mpenzi wake mwenye miaka 16, Emma Webster, wazazi wake Ray na Shirley, na mama yake Sean, Theresa. Alikuwa na miaka 11 na Emma miaka 15 alipopata ujauzito huo. 
Sean akimnywesha mwanae maziwaSean akimnywesha mwanae maziwa
Baba na mwanaBaba na mwana

Yupo darasa la saba katika shule ya Margaret Beaufort.
Mwaka jana Sean alisema kuwa atakuwa bega kwa bega na Emma na mtoto wake pia. “I was shocked at first when I was told Emma was pregnant but I am all right about it now,” alisema Sean.

JK: Mzee Kingunge Ngombale Mwiru Hospitali ya Taifa Muhimbili

8E9U0419Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyepumzishwa katika chumba cha Dharura katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo.Mzee Kingunge alikimbizwa Hospitalini Hapo Baada ya Kujisikia Vibaya.jopo la Madaktari Bingwa linamfanyia uchunguzi Mzee Kingunga ili kubaini ugonjwa unaomsumbua.Aliyesimama Nyuma ya Rais ni mke wa Mzee Kingunge na kushoto ni Mtoto wa Mzee Kingunge Bwana Kinjekitile(picha na freddy Maro)

Rais Kikwete awataka vijana wawe wazalendo, wasifurahie nchi inaposemwa vibaya


Rais wa JK amewataka vijana kuacha kushabikia watu wanaoisema nchi vibaya, amesema enzi zao watu waliokuwa wakiisema nchi vibaya walikuwa wanawachukia tofauti na saizi vijana wanashabikia!

Akizidi kuongea, kuwa endapo nchi itasemwa vibaya basi wao huchukia!
Kauli hiyo ameitoaJana jijini D'Salaam

WAZIRI SITTA ACHONGEWA KWA LOWASSA

                                                                                      Edward Lowassa 
KWA UFUPI
Historia ya kisiasa baina ya vio ngozi hao inakifanya kikao cha leo kuwa mvuto wa aina yake kwani kitendo cha wabunge kuichongea Wizara ya Sitta kwa Kamati ya Lowassa kitatoa mwanya wa mpambano kati ya wanasiasa hao wawili.
Wakati hayo yanatokea, kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Edward Lowassa itakutana na Wizara hiyo inayoongozwa na Waziri Samuel Sitta kujadili mambo mbalimbali yakiwamo sera ya Tanzania katika jumuiya hiyo.
Lowassa, alijiuzulu Uwaziri Mkuu 2008 wakati Sitta akiwa Spika na inasadikiwa kwamba tukio hilo lilijenga ufa kati ya wanasiasa hao wawili, ambao tayari wanatajwa katika kinyang’anyiro cha Urais 2015.
Historia ya kisiasa baina ya vio ngozi hao inakifanya kikao cha leo kuwa mvuto wa aina yake kwani kitendo cha wabunge kuichongea Wizara ya Sitta kwa Kamati ya Lowassa kitatoa mwanya wa mpambano kati ya wanasiasa hao wawili.
Wakizungumza mbele ya kamati hiyo, wabunge wa EAC walisema wizara hiyo haijawapa mwongozo wa kutetea maslahi ya Tanzania ndani ya jumuiya, jambo ambalo linawafanya washindwe kuchangia hoja zenye uzito.
“Tunatengwa na wizara, jambo ambalo linatufanya tutoe hoja tunazozijua wenyewe, kutokana na hali hiyo wanapaswa kubadilika,”alisema Shyrose Bhanji.
Aliongeza kuwa kila wanapojaribu kuwasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, wamekuwa waki pigwa kalenda, jambo ambalo linawafanya kupata taarifa nyingine kupitia vyombo vya habari.
“Tulitarajia tungeelezwa msimamo wa nchi, lakini mpaka sasa hatujaelezwa chochote na kwamba kila mmoja anachangia kutokana na upeo wake,” aliongeza. Mbunge mwingine, Abdallah Mwinyi alisema mpaka sasa Tanzania haina sera ya mtangamano ambao utawaweka pamoja wabunge hao katika kujadili mambo ya jumuiya.
“Nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki zina sera ya mtangamano ambazo zinawaweka pamoja wabunge kujadili mambo mbalimbali yanayohusu maslahi ya nchi zao, lakini sisi hatuna, wakati Rwanda imejiunga juzi tu tayari wameandaa sera inayowapa mwongozo wabunge wao,” alisema Mwinyi.
Sitta akana
Alipoulizwa juu ya malalamiko, Sitta, ambaye jana jioni alikuwa anahudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu, alijibu kwa ujumbe mfupi wa maandishi;”Si kweli...niko kwenye kikao nitakupigia baadaye.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Stargomena Tax amewashangaa wabunge hao kwa kulalamika kukosa ushirikiano na kwamba madai hayo si ya kweli.
“Hivi wabunge hawa wanataka tuwape ushirikiano wa aina gani? Mbona tumekuwa tukikutana nao mara kwa mara na kuwapa misimamo ya nchi?
“Tulishakaa na Bunge la Jamhuri ya Muungano na tuliwapa hadidu za rejea ili wawape wabunge wa Afrika Mashariki,” alieleza Dk Tax.
Dk Tax pia alisema wamechapisha kijitabu cha kuwapa mwongoza wa maeneo ya kuzingatia wakati wanapokwenda kwenye vikao vya Bunge la Afrika Mashariki.

Miss Utalii Tanzania 2012/13 watembelea Ukumbi wa Kimataifa na kisasa wa Makumbusho ya Taifa.

Washiriki wa Fainali za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012/13,jana  wametembelea Ukumbi wa kwanza na wa Kisasa na wa aina yake Tanzania ambao unamilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia kurugenzi ya mambo ya kale na makumbusho ya Taifa uliopo ndani ya Makumbusho ya Taifa jirani na Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) karibu na maeneo ya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wakiwa katika Ukumbi huo wenye uwezo wa kuchukua watu 470 kwa wakati mmoja, walishuhudia Viti,Mitambo na vifaa vingine vya kisasa vyenye uwezo wa kuendesha Matamasha na mashindano ya Urembo kwa kiwango cha hadhi ya nyota tano.
Wengi wa washiriki hao walionyesha hamasa na kujaribu kuwashawishi viongozi na wakuu wa msafara wao ili kufanya Fainali hizo katika Ukumbi huo ambao umekuwa ni kivutio kikubwa, jambo ambalo Viongozi na kamati iliokuwa na jopo la msafara huo lilionekana kukubaliana na mawazo ya nia ya warembo hao ya kuomba Fainali hizo zifanyike ndani ya Ukumbi huo. 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Rais wa Mashindano hayo nchini na Barani Afrika Erasto G., Chipungahelo,kuhusu uwezekano wa kuandaa Fainali hizo katika Ukumbi huo wa kimataifa wa NATIONAL MUSIUM  THEATRE,  alisema kuwa kila jambo ni mipango, hivyo na kwa kuwa lengo na nia ya Mashindano ya Miss Utalii ni kutangaza Vivutio vya Taifa kuna uwezekano pia Fainali hizo zikafanyika hapo ikiwa pia ni kuwapa heshima Wizara ya Maliasili na Utalii ambao ndiyo walezi wakuu wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania kwa kuwa wao ndiyo wamiliki wa Ukumbi huo ambao kwa sasa unaonekana kuwa ni kati ya kumbi pekee zilizojengwa kisasa na hadhi ya kimataifa hapa nchini Tanzania.
ziara hiyo ya kutembelea Ukumbi huo kwa washiriki wa Miss Utalii Tanzania  2012/2013 iliandaliwa na Washiriki wenyewe baada ya kuusikia sifa zake kutoka kwa watu mbalimbali na Mitandao ya Kijamii.
 Aidha Chipungahelo amesema kwamba warembo hao wanatarajia kupanda katika jukwaani baada ya kutoka kwenye ziara ya kutembelea hifadhi za Taifa ambazo ni pamoja na Saadan, Mikumi, Udzungwa, Mkomanzi, Arusha na Mlima Kilimanjaro watakaokuwa wameambatana na waandishi wa habari.
Akizungumzia hali ya Ukumbi  huo Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo amesema kwamba ni heshima kubwa kwa Taifa na sekta nzima ya Utalii kuona Warembo ambao wanatangaza Utalii wa Nchi yetu wakivutiwa  na ukumbi huo hata kufikia kupeleka maombi ya kutaka wao kuwa Warembo wa kwanza kupanda katika jukwaa hilo la Ukumbi wa kisasa na wa kimataifa wa NATIONAL MUSIUM  THEATRE ulipo ndani ya Makumbusho ya Taifa ambao ni kivutio kikubwa kwa sasa katika anga za Burudani na sanaa.
“Ukumbi ni mzuri kama ambavyo wenyewe wandishi mlivyoona na kutazama, hakika ni jambo la kujivunia na kusifiwa kwa Wizara yetu, maana unaonekana ni jambo la kujipanga hadi kuweza kutengeneza kwa ubora huo unaoonekana sasa, bila shaka nyie wenyewe mtaona ni kwa kiasi gani Umeandaliwa, lakini hata hivyo ni changamoto kwa Wizara zingine katika kubuni  na kuweka rasilimali kama hizi kwa manufaa ya Taifa, kama ambavyo mnaona wenyewe, kwani hata Washiriki wamefurahi na hata kusifia sana hivyo pia nachukua fulsa hii kuishukuru Wizara kwa kuwekeza Ukumbi wa Kisasa ambao ni faida kwa Taifa” alisema Chipungahelo.
Pia aliendelea kusisitiza na kuomba wadau na wapenzi mbalimbali wa mashindano haya kujitokeza kuunga mkono kudhamini na kununua tiketi siku ya shindano..
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania wakiwa wanatembelea Ukumbi wa Kimataifa wa Makumbusho ya Taifa(NATIONAL MUSEUM THEATRE).

Mahakama ya Zimbabwe yaweka ngumu kumuachia mwanasheria Mtetwa kwa dhamana.

Mahakama nchini Zimbabwe imekataa kumuachia kwa dhamana mwanasheria anayetetea haki za binadamu Beatrice Mtetwa na wasaidizi wanne wa Waziri Mkuu Bw. Morgan Tsvangirai.
Mwanasheria huyo Mtetwa alikamatwa Jumapili iliyopita akishutumiwa kuzuia mkondo wa sheria kufanya kazi yake na atabakia kizuizini hadi tarehe 3 mwezi Aprili mwaka huu.
Wasaidizi wane wa Bw. Morgan Tsvangirai wanashikiliwa kwa kutuhumiwa kujifanya maaafisa wa polisi, lakini wamekana tuhuma hizo.-DW.

Thursday, March 21, 2013

WOLPER, HARTMANN WAPATA AJALI

Issa Mnally na Richard Bukos
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amenusurika kufa ajalini baada ya gari lake kugongana na gari lingine.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar, jirani na nyumba ya staa mwenzake, Wema Sepetu ambapo Wolper aliyekuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota-Brevis Saloon alivaana uso kwa uso na gari lingine aina ya Toyota-Nadia.
Kwenye ajali hiyo, gari la Wolper lilibondeka mbele na kuvunjika kioo cha pembeni (side mirror).

 
                                                                                 Wolper.
Akizungumza na mwandishi wetu, Wolper alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kumshukuru Mungu kwa kumnusuru kwani hakuumia popote.
“Nilikuwa na mdogo wangu tunaelekea gereji kufuata gari langu, hili nililopata nalo ajali, siyo la kwangu hata sijui itakuwaje!” alisema Wolper.


 

                                                                      Hartman Mbilinyi.
Wakati huohuo, Hartman Mbilinyi ambaye ni prodyuza wa filamu, Jumatatu usiku alipata ajali baada ya gari lake kugongana na pikipiki wakati akirudi nyumbani kwake, Tegeta.

MAMA LINEX AMKATAA MCHUMBA WA KIZUNGU WA LINEX

Sunday Mangu ‘Linex’ akiwa na mchumba wake Suvi Rikka.
 
SIKU chache baada ya Mbongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’ kumvisha pete ya uchumba demu wake mtasha, Suvi Rikka, mama wa staa huyo, Imelda Barnabas ameibuka na kumchana mwanaye kuwa haitambui pete wala mchumba huyo kwa kuwa kitendo hicho hakina baraka zake wala za familia.
Shemeji yetu katika pose
Linex alipoulizwa juu ya sakata hilo, alifunguka:
“Yah! Bi mkubwa amenijia juu ile mbaya, ila najitahidi kumuomba msamaha, hope atanielewa.”

JACK WOLPER NA RADO WAJIPANGA KUTOKA NA "MAHABA NIUE"

Muigizaji wa filamu mwenye mvuto nchini, Jacquiline Wolper hivi karibuni ataonekana kwenye filamu mpya aliyoigiza na Simon Mwapagata maarufu kama Rado iitwayo Mahaba Niue.

Akiongea na mtandao wa bongomovies, Rado amesema katika kuwapa raha zaidi mashabiki wao, filamu hiyo itatoka na zawadi ya bure ya kalenda.

Filamu hiyo imetayarishwa na Step Entertainment.

PENZI LA MWANAFUNZI LAZUA BALAA LASABABISHA VIZEE KUPIGANA HADHARANI

Kwa kawaida tumezoea kusikia kuwa vijana wakipigana kuhusu wanawake huku tukidhani kuwa wivu wa mapenzi unawatesa vijana peke yao kumbe si kweli mpaka wazee nao wanateswa sana na wivu, Hiki ndicho kilicho tokea katikati ya jiji ambapo wazee wawili walinasa na kamera yetu wakitaka kupigana kisa denti wa shule aliyekuwa akiwachanganya wote wawili bila wao kujijua utata ulikuja pale wazee hao marafiki mmoja wao alipopigiwa simu na msichana huyo baada ya kumaliza kuongea ndipo mzee wa jirani alipouliza huyo nani mwenzake akajibu huyu mpenzi wangu zai hapo ndipo ugomvi ulipoanza na wazee hao kutaka kupigana kisa mwaafunzi wa kidato cha tatu.

Wanafunzi washinda danguroni Dar

Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Majani ya Chai iliyopo Kipawa jijini Dar es Salaam, wametajwa kujiingiza katika kashfa ya ngono, kuvuta na kuuza bangi katika moja ya nyumba zinazozunguka shule hiyo.

Hilo ni tukio lingine jipya, kwani mwishoni mwa mwaka jana, kuliibuka matukio ya ajabu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi, Ruaruke, Rufiji mkoani Pwani ambao walielezwa kujihusisha na uvutaji bangi hata kukonyeza na kubaka walimu wao.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Yasinta Assey akionyesha baadhi ya nguo na viatu vya wanafunzi vilivyokutwa katika eneo linalodaiwa kuwa danguro linalotumiwa na wanafunzi wa shule hiyo, jana. Picha na Pamela Chilongola 
Mkuu wa Sekondari hiyo, Jasinta Assey alikiri na kusema kwamba vitendo vya uvutaji bangi na biashara ya ukahaba kwa wanafunzi wake, vinachangiwa na askari wa Kituo kidogo cha Stakishari ambao alidai wanachukua rushwa kwa wauzaji wa bangi na nyumba bubu za wageni. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Shule hiyo, Jasinta Assey alisema ni kawaida ya polisi hao kwenda kwenye nyumba hizo kunakofanyika biashara hizo na kuchukua rushwa badala ya kutatua tatizo.

Alisema ongezeko la utoro katika shule hiyo ni tatizo kubwa na wanafunzi wa kidato cha nne wanaosoma masomo ya sanaa ndiyo wanaoongoza kwa kuvuta bangi na kwenda kufanya ngono katika nyumba zilizo jirani na eneo la shule hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema hajapata taarifa za hali hiyo.

“Ngoja nimtume Mkuu wa Kituo cha Polisi Stakishari afuatilie kwa karibu,” alisema Minangi na kuongeza: “Lakini ngoja nikwambie, hili suala nakumbuka liliwahi kuripotiwa 2011 wakati nikiwa mkuu wa kituo hicho; nililishughulikia na tulibaini kuwa hakuna mwanafunzi ambaye alikuwa anaenda kwenye nyumba hizo kuvuta bangi wala kufanya ngono.
“Kilichotokea kwa wakati huo ni kwamba, tuliwachukua baadhi ya wanafunzi ili watupeleke mahali walipokuwa wakifanyia vitendo hivyo kutokana na maelezo na vielelezo vyao, lakini hatukubaini hizo sehemu.

“Inawezekana basi haya mambo yameibuka upya baada ya kuona kuna mkuu wa kituo mwingine mpya,” alisema Kamanda Minangi.
Kutokana na matendo hayo, wanafunzi wengi walifanya vibaya mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka jana.

“Walifeli sana mwaka jana hawa, walimu wapo, tunawapa nyenzo lakini hawataki, ninaiomba Serikali kuingilia kati suala hili kwani ni la muda mrefu na ni faida ya vijana hawa,” alisema.

Shule ya Majani ya Chai ilishika nafasi ya 61 kimkoa kati ya shule 226 wakati ngazi ya taifa, ilishika nafasi ya 543 kati ya shule 3,392.

Wanafunzi 274 walijisajili kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana na kati yao 130 walipata sifuri, wakati waliopata daraja la nne ni 85, waliopata Daraja la Tatu ni 18 wakati waliopata daraja la pili ni watano. Hakukuwa na daraja la kwanza na wanafunzi 36 hawakufanya mtihani.

“Baada ya kuona utoro umekithiri shuleni hapo, nilikwenda kutoa taarifa kituo kidogo cha Polisi Stakishari, lakini hawakuonyesha ushirikiano matokeo yake wanakwenda kwa wenyeji hao na kuchukua rushwa.

“Hili inaonekana kama ni dili la hawa askari, kwani wapo walionifuata na kunieleza niache kufuatilia, lakini mimi niliwaambia nitafuatilia tu na ilifikia hatua nikatishiwa maisha.
“Baada ya kuona nazidi kutishiwa maisha, niliogopa, nikaacha...na hivi ninavyoongea na wewe, najua tu watanifuata kwani nimeshaambiwa nikipita peke yangu eneo wanakofanyia biashara zao watanifanyia kitu kibaya,” alisema Assey.Mwalimu huyo alisema kwamba, wanafunzi wa kidato cha nne wanaosoma masomo ya sanaa wapo 54, lakini wakati mwingine utakuta wanafunzi watano tu darasani na waliobakia wanakwenda kuvuta bangi na kufanya vitendo vya ngono.


Assey alisema kuwa iliwahi kutokea wasamaria wema waliwapelekea baadhi ya nguo na viatu vya wanafunzi wa shule hiyo vilivyokutwa eneo wanakofanya biashara hiyo ya haramu.

“Hili darasa linaongoza kwa utovu wa nidhamu na limeshindikana...Nilikuwa nawategemea sana polisi, lakini hawaonyeshi ushirikiano wowote ule...Unaona hizi nguo za wanafunzi zililetwa na mama mmoja baada ya kuzikuta kwenye danguro ‘bubu’,” alisema Assey huku akionyesha sare hizo za shule.

SHILOLE, BABY MADAHA WAFUATA NYAYO ZA WEMA


WAREMBO wawili wanaotesa katika soko la muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha na Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wameamua kufuata nyayo za Wema Sepetu kwa kunyoa nywele na kuonekana katika muonekano mpya.
 

Akizungumza na paparazi wetu, Shilole ambaye amenyoa nywele staili ya kiduku alisema ameamua kufanya bhiv yo ili kuwa na muonekano wa tofauti kwani watu wameshamzoea kila siku kumuona na mawigi na rasta.
 

Kwa upande wa Baby Madaha alisema ameamua kubadilisha mfumo wa maisha kuanzia nywele hadi mavazi kwani huu ni mwaka mpya hivyo kutoka na staili mpya.
Hivi karibuni Wema alikuwa wa kwanza kutangaza kuwa na muonekano tofauti kwa kutupia picha zake mtandaoni zilizomuonesha akiwa amenyoa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...