Friday, February 15, 2013
JAJI MKUU WA UGANDA MHE. ODOKI AKUTANA NA WAJUMBE WA TUME YA KATIBA
SPIKA WA BUNGE ANNA MAKINDA AONGEZEWA ULINZI
SPIKA wa
Bunge, Anne Makinda ameongezewa ulinzi pamoja na kubadilishiwa namba za
gari analotumia kutokana na vitisho anavyovipata kutoka kwa wananchi
ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe wa simu.
Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa Spika Makinda amepokea ujumbe mfupi wa simu zaidi ya 400 na kupigiwa simu zinazofikia 200 za kumkashifu na vitisho.
Taarifa zilizopatikana jana zinaeleza kuwa Spika Makinda amekuwa akitumiwa ujumbe mfupi wa vitisho ambavyo inaonyesha kuwa wananchi wana hasira naye na ndiyo maana ameongezewa ulinzi.
Vyanzo vyetu vya habari vimeeleza kuwa gari la Spika Makinda limebadilishwa namba kwa kuondolewa herufi S ambayo humaanisha Spika na kuwekwa namba nyingine ambazo bado hazijajulikana.
“Watu wanaomtumia ‘meseji’ wana hasira, wanaweza kumdhuru na ndiyo maana ameongezewa ulinzi. Hata magari yake aliyokuwa akitumia yamebadilishwa na kupewa mengine tofauti,” kilieleza chanzo chetu cha habari.
Spika Makinda mwenyewe alipopigiwa simu ili kueleza kuhusu suala hilo la kuongezewa walinzi simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah naye simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.Tangu Chadema wagawe namba hiyo baada ya kumtuhumu Spika pamoja na msaidizi wake, Job Ndugai kuwa amekuwa akipindisha kanuni wakati wa kuliongoza Bunge.
Taarifa zilieleza kuwa wamekuwa wakisumbuliwa na kutumiwa ujumbe za vitisho.Wakati hayo yakitokea, tayari Ofisi ya Bunge imesema itawachukulia hatua kali wale wote waliotumia lugha chafu kwa ujumbe mfupi ama kupiga moja kwa moja kwa Spika na Naibu wake.
Katibu Mkuu wa Bunge, Dk Kashililah juzi alisema kuwa kutoa namba si tatizo, bali kuzitumia namba hizo kinyume na taratibu ndiyo haitakiwi, jambo ambalo linaweza kusababisha baadhi yao kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Wote waliotoa lugha za matusi kwa Spika Makinda na Naibu Ndugai watachukuliwa hatua za kisheria.
Tutawatafuta kwa njia zote, hii itasaidia kuwa fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo ambao wanapewa namba kwa manufaa ya wananchi, lakini wanazitumia kinyume chake,” alionya Kashililah.
“Tutawasaka kwa kila hali, tutawabaini tu kwa kushirikiliana na idara mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Polisi ili wachukuliwe hatua kali.”
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alipoulizwa jana kuhusu msimamo wa chama chake baada ya kutoa namba hizo kwa wananchi alisema; “Bunge halijatuuliza ila wakituuliza tutajibu.”
Taarifa
ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa hatua hiyo imekuja baada ya
viongozi wa Chadema kutoa namba za Spika na kuzigawa kwa wafuasi wake
waliofika kwenye mkutano uliofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga,
jijini Dar es Salaam hivi karibuni ili wamtumie ujumbe mfupi wa simu.
Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa Spika Makinda amepokea ujumbe mfupi wa simu zaidi ya 400 na kupigiwa simu zinazofikia 200 za kumkashifu na vitisho.
Taarifa zilizopatikana jana zinaeleza kuwa Spika Makinda amekuwa akitumiwa ujumbe mfupi wa vitisho ambavyo inaonyesha kuwa wananchi wana hasira naye na ndiyo maana ameongezewa ulinzi.
Vyanzo vyetu vya habari vimeeleza kuwa gari la Spika Makinda limebadilishwa namba kwa kuondolewa herufi S ambayo humaanisha Spika na kuwekwa namba nyingine ambazo bado hazijajulikana.
“Watu wanaomtumia ‘meseji’ wana hasira, wanaweza kumdhuru na ndiyo maana ameongezewa ulinzi. Hata magari yake aliyokuwa akitumia yamebadilishwa na kupewa mengine tofauti,” kilieleza chanzo chetu cha habari.
Spika Makinda mwenyewe alipopigiwa simu ili kueleza kuhusu suala hilo la kuongezewa walinzi simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah naye simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.Tangu Chadema wagawe namba hiyo baada ya kumtuhumu Spika pamoja na msaidizi wake, Job Ndugai kuwa amekuwa akipindisha kanuni wakati wa kuliongoza Bunge.
Taarifa zilieleza kuwa wamekuwa wakisumbuliwa na kutumiwa ujumbe za vitisho.Wakati hayo yakitokea, tayari Ofisi ya Bunge imesema itawachukulia hatua kali wale wote waliotumia lugha chafu kwa ujumbe mfupi ama kupiga moja kwa moja kwa Spika na Naibu wake.
Katibu Mkuu wa Bunge, Dk Kashililah juzi alisema kuwa kutoa namba si tatizo, bali kuzitumia namba hizo kinyume na taratibu ndiyo haitakiwi, jambo ambalo linaweza kusababisha baadhi yao kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Wote waliotoa lugha za matusi kwa Spika Makinda na Naibu Ndugai watachukuliwa hatua za kisheria.
Tutawatafuta kwa njia zote, hii itasaidia kuwa fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo ambao wanapewa namba kwa manufaa ya wananchi, lakini wanazitumia kinyume chake,” alionya Kashililah.
“Tutawasaka kwa kila hali, tutawabaini tu kwa kushirikiliana na idara mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Polisi ili wachukuliwe hatua kali.”
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alipoulizwa jana kuhusu msimamo wa chama chake baada ya kutoa namba hizo kwa wananchi alisema; “Bunge halijatuuliza ila wakituuliza tutajibu.”
WIVU WA PENZI LA MAINDA WAMFANYA RAY NA STEVEN NYERERE WAKOSANE
MASTAA wawili wenye majina makubwa ndani ya Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wanadaiwa kuwa kwenye bifu zito kisa kikielezwa kuwa ni mwigizaji , Ruth Suka ‘Mainda’,
Kwa mujibu wa vyanzo makini vilivyo karibu na mastaa hao, hofu imetanda kwamba huenda wawili hao wakazama kwenye ugomvi kama ule wa Ray na marehemu Steven Kanumba.
“Ugomvi wa Ray na marehemu ulikuwa mdogo ila ulikuzwa na alipofariki dunia Kanumba kuliibuka mambo mengi sana, naomba marafiki wa dhati wa wawili hawa wakae nao ili kuweka mambo sawa,” ’ alisema mwigizaji mmoja.
Inadaiwa kuwa chanzo cha yote ni pale Steve Nyerere alipoanzisha kampuni ya kazi zake za sanaa akimshirikisha Mainda, jambo linalosemekana kumkera Ray aliyekuwa akifanya kazi na mwigizaji huyo wa kike chini ya Kampuni ya RJ Production.
“Kuna wakati eti Ray huwa hapendi kumuona mtu akiwa karibu na Mainda, mara nyingi huwa anakuwa na wivu kwa kuwa anahisi kuna kitu zaidi ya kazi,” kilisema chanzo kingine na kusisitiza kuwa Ray alimpiga ‘stop’ Mainda kushirikiana na Steve Nyerere huku suala la wivu wa kimapenzi likitajwa.
Ilidaiwa kuwa kabla ya mtafaruku huo, Steve Nyerere na Ray walikuwa ni maswahiba lakini sasa wamegeuka chui na paka na katika kutafuta ‘sosi’ ya yote hayo, ndipo Mainda akatajwa.
Vyanzo hivyo vilifunguka kuwa hali hiyo ilizua tafrani kubwa kwa kuwa tayari filamu ya Steve Nyerere (jina kapuni) ilikuwa imeanza kurekodiwa.
Baada ya kupata taarifa hizi, mwandishi aliwatafuta wahusika, wa kwanza alikuwa Steve Nyerere, alipoulizwa kuhusiana na hilo alikiri kutokea kwa ishu hiyo.
“Ni kweli mimi na Ray ni chui na paka lakini sitaweza kukwambia sababu ya ugomvi wetu kwa kuwa nitaibua mambo mengi sana, kipindi hiki nipo katika kubadilisha maisha yangu,” alisema Steve Nyerere.
Ray alipotafutwa kwa simu ya kiganjani hakupatikana na hata alipofuatwa ofisini kwake Sinza-Mori, Dar hakuwepo.
Kwa upande wake Mainda, simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kuwapata wawili hao ili nao wafunguke ya moyoni mwao zinaendelea.
VAZI LA MBUNGE SHYROSE BHANJI LAZUA UTATA BAADA YA KUKIANIKA "KITOVU" CHAKE
VAZI alilotinga Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji limezua utata kufuatia kuonesha sehemu yake ya tumboni (kitovu).
Utata huo umekuja mara baada ya picha inayomuonesha mbunge huyo akiwa amejipara na kuvalia vazi hilo ambalo linamuonesha sehemu hiyo nyeti na kutupiwa mtandaoni.
“Jamani huu ni utata sasa, inakuwaje mheshimiwa anatinga vazi kama hili? Haya mambo bora angewaachia mastaa wadogo, umri wake haufanani na mambo haya!” aliandika mdau mtandaoni
ASKOFU AMANI: TUMEINGILIWA NA SARATANI YA UVUNJIFU WA AMANI
Askofu wa Jimbo la Moshi la Kanisa
Katoliki Tanzania, Askofu Isaac Amani Massawe amesema kuwa Tanzania
imeingiliwa na ugonjwa wa saratani wa kuvunja amani na utulivu na
Watanzania wasipobalika na kukubatia amani watajuta.
Amesema kuwa baada ya miaka 50 ya Uhuru,
Watanzania sasa wamefungua ukurasa mpya na nchi imeanza kupoteza sifa
ya kuwa nchi ya amani na utulivu.
Aidha, amesema kuwa wajibu wa watu
kuishi kwa amani siyo wajibu wa Serikali ama wa Dini ama wa Kanisa bali
ni wa kila mtu kwa nafsi yake.
Askofu Amani ameyasema hayo leo,
Alhamisi, Februari 14, 2013 wakati alipokuwa anatoa neno la shukurani
baada ya kumalizika kwa Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Askofu Jimbo la
Moshi, Askofu Mstahivu Amedeus Peter Msarikie katika Kanisa Kuu la
Kristo Mfalme mjini Moshi.
Askofu amewaambia mamia kwa mamia ya
waumini: “Tumefungua ukurasa mpya katika Tanzania. Baada ya miaka 50 ya
amani na utulivu sasa tumebadilika. Tanzania ya leo siyo Tanzania ya
zamani sasa tumeanza kuongozwa na misingi ya vurugu za kidini na vurugu
za kifedha.”
Ameuliza Baba Askofu Amani: “Tumeelimika
zaidi ama tumechoka amani? Tumeingiwa na saratani ya uvunjifu wa amani
na migawanyiko kwa misingi ya kidini na kifedha na mingine ya aina mbali
mbali. Njia nzuri ya kuagana na mzee wetu Askofu Msarikie ni kuishi
maisha aliyoishi yeye- maisha ya amani na utulivu. Yeye alikuwa chombo
cha amani na anapumzika kwa amani kwa sababu aliishi maisha ya amani.”
Ameongeza: “Kuishi kwa amani na utulivu
siyo suala wala wajibu wa Serikali ama wa Kanisa ama wa Dini ni wajibu
wa kila mtu kwa nafsi yake na kila mmojawetu anao wajibu wa kusali ili
kuombea amani ambayo imedumu katika nchi yetu kwa miaka mingi sana –
miaka 50 sasa lakini inaonyesha kila dalili ya kutoweka.”
Amesisitiza: “Ndugu zangu amani
hairithishwi, amani hujengwa na hulindwa. Changamoto alichotuachia
Askofu Msarikie ni kutafuta na kuilinda amani katika nchi yetu. Huwezi
kuwa mtu wa vurugu na mvunja amani na bado ukapata starehe ya milele
mbele ya Mwenyezi Mungu. Sasa ni wakati wa kulea taifa letu,
kulitengeneza upya na tumwombe Mungu atusaidie katika safari hii ndefu.”
Thursday, February 14, 2013
MAANDALIZI YA NYAMA YA FARASI INAYOLALAMIKIWA KUUZWA KWA WANANCHI UINGEREZA
Wafanyakazi wa Kampuni Spanghero, inayosambaza nyama
nchini Uingereza wakiandaa nyama hiyo tayari kwa kupaki katika vifuko
kwa kuwauzia wateja wao, ambapo hivi sasa Kampuni hiyo inaandamwa kwa
kudaiwa kuwauzia wateja wake nyama ya Farasi badala ya nyama ya Ng'ombe.
Imeelezwa kuwa wateja wa kampuni hiyo wamekuwa wakifurahia huduma hiyo
wanayoipata kwa bei nafuu tofauti na awali.
RAIS KIKWETE ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA MAREHEMU ASKOFU MSTAAFU JIMBO KATOLIKI MOSHI MHASHAMU AMEDEUS MSARIKIE
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za Mwisho mbele ya jeneza la Askofu Mtsaafu jimbo Katoliki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa misa ya Mazishi iliyofanyika katika kanisa na Kristu Mfalme, mjini Moshi leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Askofu Mstaafu Jimbo katoliki la Moshi,Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi leo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Askofu Mstaafu jimbo Katoloki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi leo. Picha na Freddy Maro wa Ikulu
CHADEMA yawakumbuka wagonjwa siku ya wapendanao
''Siku ya leo CHADEMA
tumefanya usafi; kufagia, kufyeka, kukusanya takataka, kusikiliza
changamoto zinazowakabiri wagonjwa na wauguzi, pia katika kuonyesha
ishara ya upendo katika siku hii tumewaletea wagonjwa vitu mbalimbali
ikiwemo mikate, juice, maji, sabuni nakadhalika.'' Alikaririwa mmoja wa
makanda
Mwanariadha Oscar Pistorius amuua mpenzi wake kwa risasi. “Valentine’s Day surprise that went tragically wrong”.
Mwanariadha Oscar Pistorius alipokuwa katika
mashindano ya Olympic mwaka 2012 mjini London.
Mwanariadha na mshindi wa medali za dhahabu wa
Paralympic raia wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, amekamatwa nyumbani kwake mjini Pretoria kwa kosa la kumuua
mpenzi wake baada ya kumpiga risasi moja kichwani na nyingine mkononi ,
majeraha yaliyopelekea kifo cha binti huyo.
Chanzo cha Pistorius kumsuti mpenzi wake bado
hakijaeleweka, japo fununu za awali zinadai uenda Pistorius
alijichanganya na kudhani amevamiwa na mwizi/jambazi kutokana na hali
mbaya ya uhalifu anayoikabili nchi ya Afrika Kusini.
Binti huyo Reeva Steenkamp, (30) mwanamitindo
alilenga kumsuprise Pistorius kwaajili ya valentine.
Msemaji wa Polisi aliliambia shirika la habari
la Reuters “tumekuta pisto ya mm9 eneo la tukio, na mtuhumiwa amepelekwa
kituoni kwaajili ya utaratibu mwingine”.
Pistorius mwenye miaka 26 maarufu kama “blade
runner” amekuwa ni mlemavu wa kwanza kushiriki Olympic mbali na
mashindano yao maalum ya Paralympic , hukimbia riadha kwa kutumia vifaa
maalum vilivyofungwa miguuni kwake, baada ya
kuzaliwa bila miguu yote miwili.
Mpenzi
wa Pistorius, Mwanamitindo Reeva Steenkamp aliyepigwa risasi na
kupoteza maisha.
Zimbabwe kuipigia kura Katiba mpya.
Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai
anasema nchi hiyo inatarajiwa kufanya uchaguzi wa bunge na urais mwezi
Julai baada ya kupiga kura maoni juu ya katiba
mpya mwezi Machi.
Alisema hayo Jumatano baada ya waziri wa maswala ya katiba Eric
Matunenga kupanga tarehe ya Machi 16 kwa ajili ya
kupiga kura ya maoni.
Katika mkutano na
waandishi wa habari huko Harare , Matinenga alieleza wasi wasi wake kuwa
muda hautoshi na pengine muda zaidi huenda ukahitajika kwa ajili ya
uchaguzi wa Machi.
Baraza la kitaifa la
bunge (NCA) ambalo linajumiwsha makundi ya
harakati za kidemokrasia huko Zimbabwe limesema litapinga tarehe upigaji kura wa maoni hapo
Machi 16 mahakamani .
Katika mahojiano na Sauti ya Amerika mwenyekiti
NCA Lovemore Madhuku amesema kundi lake linataka
serikali itoe kipindi cha mdahalo cha miezi
miwili hivi kabla ya wapiga kura kufanya uamuzi
wao juu ya katiba mpya.
Chama cha Bw. Tsvangirai
cha MDC na kile cha rais Robert Mugabe cha ZANU
PF wote wanaunga mkono mabadiliko hayo mapya.
Jumuiya ya maendeleo ya Afrika Kusini inataka katiba mpya iidhinishwe kabla ya Zimbabwe kufanya uchaguzi mkuu.
TANESCO, Symbion Power signs MOU for a joint venture in 400MW Mtwara plant
TANESCO
and Symbion Power today signed a Memorandum of Understanding for
building and operating a 400MW power plant in Mtwara through a Public
Private Partnership. The work will include the construction of a 650 km
transmission backbone from Mtwara to Songea where it will be connected
to the TANESCO national grid through a line that will be built from
Makambako to Songea.
This
development will be phased and it will take three years from financial
closure to completion. The first phase will involve increasing the
existing capacity in Mtwara to meet the growing demand in the southern
regions including Lindi and Mtwara. Engineering study work will
commence in March.
TANESCO
and Symbion have been in discussions since Symbion presented a proposal
to TANESCO and the Ministry of Energy in September 2012. This has now
led to the signing of the board-approved MOU that allows the two
companies to form a Public Private Partnership and develop the project.
It will take around 12 months to put the necessary financing in place
before the three-year clock begins to tick.
Speaking
at the signing of the MOU in Dar es Salaam, Paul Hinks, the Chief
Executive Officer of Symbion Power said, “The south of this country has
been starved of energy for decades and this has severely stunted its
development. This project will succeed because it includes transmission
lines that will feed the grid system. The transmission lines will be
owned exclusively by TANESCO but they will be built as a part of the
project.”
“Symbion
and TANESCO will be working with a number of international funding
agencies, banks and private equity firms in 2013 to put the financial
package together, many of whom have already expressed great interest in
the project. We are hopeful that U.S. government agencies such as the
U.S. Exim Bank and the U.S. Overseas Private Investment Corporation will
show keen interest in the investment too.”
“In
the three years since Symbion came to Tanzania we have seen rapid
development and improved network stability. Tanzania will in the future
have an abundance of gas and it can become entirely self sufficient and
even a regional exporter to countries that are not blessed with the
fuel resources that are available in the country. The days of complete
reliance on rain-driven hydro electric systems are gone and alternative
sources of power need to be implemented to ensure that there is security
of supply.”
Speaking
during the signing event, TANESCO’s Acting Managing Director Eng.
Felchesmi Mramba said, “For many years the Southern part of the country
has been suffering from poor power reliability due to the region not
being connected to the National Grid. However, through this planned
partnership, Lindi, Mtwara and Ruvuma will be connected to the National
Grid. Connecting the Southern regions to the National grid will
significantly improve reliability of the entire network. This is one of
the ways TANESCO can benefit from the PPP arrangement whereby the
Public and Private sector join forces to undertake projects that would
otherwise be difficult to implement.”
Wabunge wa Tanzania kukomeshwa kwa kufuta Matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji wa kanuni za
bunge uliofanywa na baadhi ya wabunge wakati wa mkutano wa 10 wa bunge
uliomalizika mjini Dodoma na mabadiliko yaliyofanyika kwa baadhi ya
kamati kuondolewa pamoja na uundwaji wa kamati mpya 3
zitakazoshughulikia Ushirikiano wa Afrika, Mashariki, Bajeti, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa. (
Akasema
ili kurejeza maadili kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha
matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa
hoja zisizokuwa za msingi.
Akasema
jamii imeendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za msingi
kutokana na kukiukwa kanuni hizo.
Dk
Kashilila amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya kamati za bunge ambazo
zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati hizo kuingilia katika utendaji
jambo ambalo limekuwa likipoteza maana ya kamati hizo.
Ameahidi
kuwa ofisi yake itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari
katika utoaji wa taarifa mbalimbali za bunge pamoja na uandaaji wa
mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wanaoandika habari za bunge, huku
akiwasisitiza waandishi wa habari kuitumia ipasavyo ofisi yake kupata
taarifa sahihi za kuwasaidia katika uandishi.
Pinda akutana na Mkurugenzi wa WFP na Ujumbe Wabunge wa Ujerumani
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa
Chakula Duniani (WFP), Bibi Ertharin Cousin Ofisini kwake jijini Dar es
salaam Februari 13, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya bunge
la Ujerumani walipomtembelea, Ofisini kwake jijini Dar es salaam
Februari 13, 2012.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya
Bajeti ya bunge la Ujerumani baada ya kuzungumza nao, Ofisini kwake
Februari 13, 2012.Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
William Lukuvi
Subscribe to:
Posts (Atom)