Dar es
Salaam.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Aprili
18, mwaka huu inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi inayomkabili Katibu
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (55)
na wenzake 49.
Mbali na
kupangwa kwa tarehe ya hukumu hiyo, Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa jana
aliutaka upande wa mashtaka na utetezi kuwasilisha hoja zao kama
washtakiwa hao watakuwa na hatia ama la, Aprili 3, mwaka huu.
Juzi wakati
Sheikh Ponda akijitetea aliieleza mahakama hiyo, kuwa yeye hana nyaraka
za umiliki wa Kiwanja cha Malkazi Chang’ombe bali historia ya eneo hilo
inawafanya wao kuwa wamiliki.
Sheikh
Ponda na wenzake hao 49, wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kuingia
kwa jinai, kuvamia ardhi inayomilikiwa na Kampuni ya Agritanza Ltd kwa
nia ya kujimilikisha isivyo halali, wizi wa mali yenye thamani ya Sh
59.6 milioni na uchochezi.
Akijitetea
dhidi ya mashtaka hayo, Sheikh Ponda, akiongozwa na wakili wake, Juma
Nassoro, alidai kuwa awali kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa na
Taasisi ya Jumuiya ya Kiislamu ya East African Muslim Welfare Society
(EAMWS) ambayo ilivunjwa na Serikali mwaka 1958 na Serikali kuunda
chombo kingine kilichosajiliwa kama Bakwata.
Alidai kuwa
Bakwata iliundwa ili kusimamia shughuli zilizokuwa zikiendeshwa na
Taasisi ya Jumuiya ya Kiislamu ya East African Muslim Welfare Society na
siyo mali kama majengo, viwanja na hata shule.
“Tulitumia
njia ya mazungumzo ya kidiplomasia kurejesha kiwanja cha Malkazi
Chang’ombe kwa kuzingatia kuwa itatatua mgogoro huo katika njia nyepesi”
alidai Sheikh Ponda.
Alidai
Sheikh Ponda.Nyerere sasa tusilete mijadala isiyokuwepo.”
Hata hivyo,
Sheikh Ponda alikubali kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliohusika kutoa
taarifa kwa maimamu wa misikiti mbalimbali kuwaeleza waumini wao
kushiriki kujitolea katika ujenzi wa msikiti wa muda uliojenga katika
eneo la Malkazi Chang’ombe Oktoba 11 na kukamilika Oktoba 14, mwaka
jana.
Alidai kuwa
walijenga msikiti huo baada ya kufanya makubaliano na mmoja wa wamiliki
wa Kampuni ya Agritanza Ltd, Hafidhi, na kukubaliana kuweka alama
ambayo kila Muislamu akiiona ataiheshimu na kutofanya shughuli zake
binafsi katika eneo hilo na kupendekeza kujenga msikiti huo wa muda.
Kuhusu
kukamatwa kwake.
Sheikh
Ponda alidai kuwa yeye alikamatwa Oktoba 16, 2012, nyakati za saa 4
kasoro usiku alipokuwa akijiandaa kuingia katika Msikiti wa Tungi Temeke
, akipanda ngazi alitokea mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari nyeusi aina
ya Toyota Harrier akimtaka amfuate.