Sunday, January 29, 2017

TAZAMA PICHA ZA ZOEZI LA UOKOAJI KWA WALIOFUKIWA NA KIFUSI GEITA.

Wachimbaji wote 15 waliofukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ Geita wameokolewa asubuhi ya leo. Jambo Tz inawapa pole na kuwaombea wapone haraka ndugu wote waliokumbwa na ajali hii.

MBUNGE APENDEKEZA BIMA KWA WANYWAJI WA POMBE

Mbunge mmoja nchini Kenya amewasilisha mswada bungeni kuzishinikiza kampuni zinazouza pombe kutoa asilimia ndogo ya faida yao kuwadhamini wanywaji ambao wataathirika na pombe hiyo.

Mbunge Gideon Mwiti anataka watengenezaji wa pombe kutoa kati ya asilimia 5 na 10 ya mapato wanayopata kwa kampuni za bima ili kuwafidia watu ambao wataathirika na pombe ama hata kupata ajali kwa kuwa walevi kulingana na gazeti la Daily Nation nchini humo.

Mswada huo pia unapendekeza kwamba iwapo mtu atafariki kutokana na athari za kunywa pombe ,kampuni hizo za pombe zilazimike kufidia familia yake.

Bw Mwiti pia amezishutumu kampuni za pombe kwa kushindwa kukuza pombe zisizo na madhara kwa afya, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Thursday, January 26, 2017

WACHIMBAJI 14 WAFUNIKWA NA KIFUSI GEITA

Picha na maktaba.

Wachimbaji wadogo 14 kutoka mgodi wa dhahabu wa RZ uliopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita wamefukiwa na kifusi cha udongo baada ya kutokea maporomoko kwenye moja ya shimo walilokuwa wanachimba

Watu hao ni raia 13 Watanzania na raia mmoja wa China. Tukio hilo limetokea saa 9 usiku leo wakati wachimbaji hao wakiendelea na shughuli ya uchimbaji katika mgodi wa RZ unaomilikiwa na wachina.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga ametembelea eneo la tukio na kuona shughuli za uokozi zikiendelea na kuagiza nguvu ziongezwe

Tayari kampuni za madini ya dhahabu GGM, Kahama na Busolwa wameombwa kuongeza nguvu.

Wednesday, January 25, 2017

ECOWAS WABAINI KEMIKALI YA SUMU IKULU YA GAMBIA

Rais mstaafu wa Gambia Yahya Jammeh

Askari wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) wamegundua kemikali ya sumu kali iliyokuwa imetegwa kwenye vyumba vya Ikulu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ecowas kupitia gazeti la Freedom la Gambia, kemikali hiyo ilitegwa kwa lengo la kuua mtu yeyote atakayeingia ndani ya Ikulu hiyo.

Kutokana na hali hiyo, kiongozi mpya wa Gambia, Adama Barrow anatakiwa kuendelea kukaa Senegal kwa usalama wake huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.

CUF WAMGEUKIA JENERALI MWAMNYANGE

Kikao cha kutathmini uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani  cha  Chama cha  Wananchi (CUF), kimekusudia kumwandikia barua ya malalamiko Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange wakidai wanajeshi walishiriki kuleta hofu.

Hata hivyo, jeshi hilo limekana madai ya CUF likisema ni uzushi.

Madai hayo yalitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alipozungumza kwa simu na mwandishi wetu kuhusu uamuzi wa kikao hicho kilichofanyika jana Unguja chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na kuhudhuriwa na wajumbe 14.

Alidai kikao hicho kilichojadili mwenendo mzima wa uchaguzi kuanzia kampeni, kilifikia uamuzi wa kuandika barua ya malalamiko kwa Jenerali Mwamunyange wakidai wanajeshi walionekana wakizunguka mitaani katika jimbo, siku ya kuamkia uchaguzi na siku ya kupigakura.

FUMANIZI FEKI ZATIKISA MOSHI NA ARUSHA

(picha na maktaba) 

Utapeli wa aina yake unazidi kutikisa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha baada ya kuibuka matukio ya kupangwa ya kufumania watu wenye heshima katika jamii kwa lengo la kujipatia fedha.

Siku za karibuni kumekuwa na mlolongo wa matukio hayo, yakiwalenga viongozi wa kiroho, wanandoa na vigogo wenye nyadhifa serikalini.

Uchunguzi ulibaini utekelezaji wa matukio hayo huambatana na vitisho kwa walengwa, ikiwamo kuwapiga picha na baadaye kutakiwa kutoa fedha kati ya Sh milioni 5 na Sh milioni 15 ili tukio hilo lisichapishwe kwenye vyombo vya habari.

Wake au waume za watu, viongozi wa dini na watendaji serikalini ndiyo walengwa wakuu wa matukio hayo, kwa kuwa ndiyo wenye hofu ya kuvunjiwa heshima kwenye jamii.

Chanzo: Mwananchi.

IVORY COAST YATUPWA NJE YA AFCON

Wachezaji wa Morocco wakishangilia.

Bingwa mtetezi wa michuano ya kombe la mataifa ya afrika tembo wa Africa Ivory Coast, wametupwa nje ya michuano ya mwaka huu baada ya kuchapwa kwa bao 1-0 na Simba wa Atlas Moroco

Goli pekee liliowaondoa miamba hao wa soka wa Afrika mashindanoni lilifungwa na Rachid Alioui katika dakika ya 64 ya mchezo.

Nayo timu ya Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo ilitambia Togo kwa kuichapa kwa mabao 3-1 na hivyo kufuzu hatua ya robo fainali wakiwa vinara kwa kundi C kwa alama 7 huku Moroco wakiwa nafasi ya pili kwa alama 6.

Moroco na Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo wanafuzu katika kundi hilo la huku Ivory Coast na Togo zikitupwa nje ya michuano hiyo.

Tuesday, January 24, 2017

MAALIM SEIF "NIMESHAMALIZANA NA JECHA"

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad 
  
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamada mesema ameshamalizana na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha na haoni umuhimu wa kuzungumzia wala kumjibu, kwa sababu atampa sifa asizostahili.

Akihojiwa katika kipindi cha Funguka cha kituo cha televisheni cha Azam TV juzi, Jecha alisema hakumshirikisha Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katika kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015 visiwani humo.

Jecha alifuta matokeo hayo Oktoba 28, 2015, siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa uchaguzi wa rais, huku ZEC ikiwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 31 na mengine tisa yaliyosalia yakiwa yameshahakikiwa.

Alitangaza uchaguzi mpya Machi 20, 2016 ambao ulisusiwa na CUF na Dk Shein kuibuka mshindi.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...