Thursday, February 18, 2016

Saturday, February 13, 2016

MWANAMKE ALIYEWAPORA SILAHA MAJAMBAZI APEWA ZAWADI NA JESHI LA POLISI

http://jambotz8.blogspot.com/
Sophia Manguye akisaini mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake.
Mwanamke aliyepambana na jambazi na kufanikiwa kumnyang’anya bunduki aina ya SMG, Sophia Manguye (46), amepewa zawadi ya Sh 500,000 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Tarime/Rorya, Gemini Mushy.

Mwanamke huyo ambaye aliomba Serikali kumpa silaha ili kujilinda, alisema kuwa hajaridhika na zawadi hiyo kwa kuwa kama asingemmudu jambazi huyo watu wengi wangepoteza maisha.
http://jambotz8.blogspot.com/
Hata hivyo, Mushy alimwomba Manguye kupokea kiasi hicho japokuwa ni kidogo kwa kuwa ni zawadi kutoka ofisi yake. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

UTAFITI: UMAARUFU WA MAGUFULI WAONGEZEKA LOWASSA WASHUKA...!!!

Matokeo ya utafiti mpya uliofanywa mapema mwezi huu yanaonyesha kuwa umaarufu wa Rais John Magufuli umeongezeka kufikia asilimia 74.5, akimuacha mbali mpinzani wake wa karibu kwenye Uchaguzi Mkuu, Edward Lowassa.

Magufuli alishinda mbio za urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, akipata asilimia chache kuliko wagombea wengine kutoka CCM, lakini amejiongezea umaarufu kutokana na hatua ambazo amekuwa akichukua tangu alipoapishwa Novemba 5, 2015.

Katika uchaguzi huo, Dk Magufuli alipata kura milioni 8.8 sawa na asilimia 58.47, akifuatiwa na Lowassa aliyepata kura milioni 6.07, sawa na asilimia 39.97. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...