Thursday, February 18, 2016

Saturday, February 13, 2016

MWANAMKE ALIYEWAPORA SILAHA MAJAMBAZI APEWA ZAWADI NA JESHI LA POLISI

http://jambotz8.blogspot.com/
Sophia Manguye akisaini mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake.
Mwanamke aliyepambana na jambazi na kufanikiwa kumnyang’anya bunduki aina ya SMG, Sophia Manguye (46), amepewa zawadi ya Sh 500,000 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Tarime/Rorya, Gemini Mushy.

Mwanamke huyo ambaye aliomba Serikali kumpa silaha ili kujilinda, alisema kuwa hajaridhika na zawadi hiyo kwa kuwa kama asingemmudu jambazi huyo watu wengi wangepoteza maisha.
http://jambotz8.blogspot.com/
Hata hivyo, Mushy alimwomba Manguye kupokea kiasi hicho japokuwa ni kidogo kwa kuwa ni zawadi kutoka ofisi yake. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

UTAFITI: UMAARUFU WA MAGUFULI WAONGEZEKA LOWASSA WASHUKA...!!!

Matokeo ya utafiti mpya uliofanywa mapema mwezi huu yanaonyesha kuwa umaarufu wa Rais John Magufuli umeongezeka kufikia asilimia 74.5, akimuacha mbali mpinzani wake wa karibu kwenye Uchaguzi Mkuu, Edward Lowassa.

Magufuli alishinda mbio za urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, akipata asilimia chache kuliko wagombea wengine kutoka CCM, lakini amejiongezea umaarufu kutokana na hatua ambazo amekuwa akichukua tangu alipoapishwa Novemba 5, 2015.

Katika uchaguzi huo, Dk Magufuli alipata kura milioni 8.8 sawa na asilimia 58.47, akifuatiwa na Lowassa aliyepata kura milioni 6.07, sawa na asilimia 39.97. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

PICHA YA DEREVA WA BASI LA SIMBA MTOTO ENZI ZA UHAI WAKE

http://jambotz8.blogspot.com/
Fred Venance enzi za uhai wake.

Huyu ndiye aliyekuwa dereva wa bus la Simba Mtoto lililopata ajali juzi . Taarifa zinasema ametoka kufunga ndoa Jumapili iliyopita tu. Baba wa kijana huyu ni dereva wa bus la Tashriff.
http://jambotz8.blogspot.com/

http://jambotz8.blogspot.com/
Like page yetu ya facebook Jambo Tz
http://jambotz8.blogspot.com/
http://jambotz8.blogspot.com/
Watu 11 akiwamo mama, mwanawe na mjukuu wake wamekufa papohapo na wengine 34 kujeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya Simba Mtoto lililogongana uso kwa uso na lori. Familia iliyopatwa na janga hilo ni ya mwandishi wa habari mwandamizi wa Redio ya Mlimani, Hamis Dambaya aliyefiwa na mkewe, Raya Said, mtoto wake Nargis Hamis na mama mkwe wake ambaye jina lake halikutambuliwa mara moja. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
Watu 11 akiwamo mama, mwanawe na mjukuu wake wamekufa papohapo na wengine 34 kujeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya Simba Mtoto lililogongana uso kwa uso na lori. Familia iliyopatwa na janga hilo ni ya mwandishi wa habari mwandamizi wa Redio ya Mlimani, Hamis Dambaya aliyefiwa na mkewe, Raya Said, mtoto wake Nargis Hamis na mama mkwe wake ambaye jina lake halikutambuliwa mara moja

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARI 13, 2016

DSCN0208 DSCN0209 DSCN0210
Like page yetu ya facebook Jambo Tz

UFISADI WA SHILINGI MILIONI 20 WAZUA TAFRANI MSIKITINI JIJINI DAR ES SALAAM


Waumini wa dini ya Kiislam wakizozana nje ya Msikiti wa Masjidi Pelapela uliopo eneo la Mtakuja Vingunguti jijini Dar es Salaam katika swala ya Ijumaa leo mchana, baada ya kutokea tafrani ya waumini hao dhidi ya viongozi wao ambao wanatuhumiwa kutafuna fedha zaidi ya sh.milioni 20 walizochanga kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya.
Muumini wa Msikiti huo, Mbarouk Mohamed Makame (kushoto), akizungumza kuhusu fedha hizo zinazodaiwa kutumiwa vibaya na viongozi wao. Kulia ni mmoja wa wazee wa msikiti huo, Mzee Selasela.
 Mzee Selasela akionesha dari la msikiti huo lililochakaa ambapo fedha hizo zinazodaiwa kutumiwa vibaya na viongozi wao zingesaidia kuufanyia ukarabati. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

Wednesday, February 10, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEBRUARI 10, 2016

DSCN0076 DSCN0078 DSCN0079 DSCN0080 
Like page yetu ya facebook Jambo Tz

WEST HAM YAITUPA NJE LIVERPOOL

Raha ya mechi bao, wachezaji wa West Ham United wakishangilia 
 
Wagonga nyundo wa London West Ham United imewatupa nje majogoo wa Anfield Liverpool katika mchezo wa raundi ya nne ya kombe la FA.
West Ham walianza kuandika bao lao la kwanza kupitia kwa Michail Antonio katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza baada ya kunganisha krosi nzuri Enner Valencia's
Liverpool wakachomoa bao hilo kupitia kwa kiungo Philippe Coutinho aliyepiga mpira wa adhabu na kujaa nyavuni moja kwa moja.
Dakika tisini zikamalizika kwa sare ya bao 1-1, katika dakika 30, za nyongeza West Ham wakapata bao kupita kwa Angelo Ogbonna,
West Ham watawavaa Blackburn ugenini katika mchezo wa raundi ya tano ya michuano hiyo hapo Februari 21. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

Tuesday, February 09, 2016

MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA POLE KWA MKE WA PINDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za pole Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda aliyepatwa na ajali ya gari, iliyotokea jana tarehe 08 Februari, 2016 akiwa safarini kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mkundi lililopo katika Manispaa ya Morogoro ambapo gari aliyokuwa akisafiria Mama Tunu Pinda, ilipinduka baada ya kumgonga mwendesha pikipiki aliyeingia ghafla barabarani.

Katika salamu hizo alizozituma kupitia kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko taarifa za kutokea kwa ajali hiyo na amemuombea Mama Pinda na Majeruhi wengine kupona haraka.

"Kupitia kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu Pinda, naomba unifikishie pole nyingi kwa mkeo Mama Pinda kwa kuumia katika ajali hii, na namuomba Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi wote ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku" alisema Rais Magufuli.

Mama Tunu Pinda anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es salaam, na hali yake inaendelea vizuri.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
09 Februari, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARI 09, 2016


DSC00926 DSC00927 DSC00928 

Like page yetu ya facebook Jambo Tz

Friday, February 05, 2016

HAYA NDIO MAGARI MAPYA YA POLISI UGANDA


 Magari Maalum ya Jeshi la Polisi la Uganda yakiwa yamewasili Bandari ya Mombasa Nchini Kenya, tayari kwa safari ya kuelekea Kampala.

Jeshi la Polisi la Uganda limejiimarisha zaidi kipindi hiki cha kampeni na hasa siku ya Uchaguzi utakaofanyika hivi karibuni.


MAGUFULI: MIMI SI KICHAA WALA DIKTETA

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli.


RAIS Dk. John Magufuli amesema anapochukua hatua yeye si kichaa, si dikteta, si shetani wala si mnyama, ila ni mpole, lakini amefika mahali lazima afanye hivyo kwani ndani ya Serikali yanafanyika mambo ya ajabu.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam katika kilele cha Siku ya Sheria nchini, alipokuwa mgeni rasmi kwa mara ya kwanza katika uzinduzi wa Mwaka wa Mahakama tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisifu kazi kubwa inayofanywa na Idara ya Mahakama, huku akitangaza uamuzi wa gharama za kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge zaidi ya Sh bilioni nne ni bora zikawasaidia wananchi.

“Ninapochukua hatua mimi si mnyama, si dikteta, si shetani, ni mpole kweli, lakini inafika mahali lazima nifanye, yanayofanyika serikalini ni mambo ya ajabu sana, nataka kutoa sadaka yangu, inawezekana hata nikifa naweza kuwa rais wa malaika,” alisema.

Alipongeza kazi kubwa inayofanywa na mahakama huku akibaki kujiuliza kwanini katika maadhimisho ya siku yao hawarushi matangazo yao moja kwa moja kupitia luninga.

“Mnafanya kazi kubwa, nilipofika niliuliza kwanini hii siku yenu hamrushi ‘live’, nikajibiwa fedha za kurusha ‘live’ zinapelekwa kuwahudumia wananchi.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...