Saturday, December 31, 2016

SERIKALI NA UPINZANI WAAFIKIA MWAFAKA DRC

Wapatanishi wanaojaribu kutatua mzozo wa kisiasa huko Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo wamesema serikali ya nchi hiyo na vilevile washirika kutoka makundi ya upinzani sasa wameafikia mwafaka.

Maaskofu kutoka kanisa katoliki waliokuwa wakiendesha kikao hicho cha majadiliano wanasema makubaliano ni kwamba rais Joseph Kabila anaweza kusalia madarakani kwa mda wa mwaka mmoja, lakini ni sharti uchaguzi ufanyike ndani ya kipindi cha miezi 12.

Sharti jingeni ni kuwa rais Kabila asiwanie tena kiti cha urais katika uchaguzi huo.
Mwafaka huo unatarajiwa kutiwa saini hii leo. 

Mda wa utawala wa rais Kabila umemalizika mwezi huu lakini kutong'atuka kwake kumesababisha maandamano yaliyokumbwa na ghasia ambapo watu zaidi ya 40 wamefariki.

TRUMP AMONGEZA PUTIN KWA KUTOLIPIZA KISASI

 
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amempongeza mwenzake wa Urusi Vladmir Putin kwa kutowafukuza wanadiplomasia wa Marekani ,licha ya Marekani kufanya hivyo kujibu madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Bwana Trump alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter: Hatua nzuri ya kusubiri, nilijua kwamba yeye ni mwerevu sana!.

Moscow imekana madai yoyote ya kuingilia uchaguzi wa Marekani kupitia udukuzi.
Lakini katika hatua moja ya mwisho ya uongozi wa rais Obama ,Marekani iliagiza kuondoka kwa wanadiplomasia 35 wa Urusi kufikia siku ya Jumapili mchana. Lakini Putin alikataa kulipiza kisasi.

Mvutano huo unafuatia madai kwamba Urusi ilidukua kampeni ya chama cha Democrat na mgombea wake Hillary Clinton na kutoa habari kupitia mtandao wa Wikileaks ili kumsaidia Bwana Trump kushinda uchaguzi .

Mashirika kadhaa ya Marekani ikiwemo lile la FBI na CIA yamesema hayo yalitendeka ,lakini Trump amekuwa akipuuzilia mbali madai hayo akisema ni ya ''ujinga''. Hatahivyo amesema kuwa atakutana na maafisa wa ujasusi nchini Marekani ili kuelezewa hali halisi. Serikali ya Obama ilitangaza kisasi hicho siku ya Alhamisi.

Sunday, December 25, 2016

JAMBO TZ INAWATAKIA KHERI YA CHRISTMAS WATU WOTE DUNIANI

 
Jambo Tz inawatakia heri ya Christmas🎄 wakristu na watu wote duniani. Tusherehekee kwa amani na utulivu.
Like page yetu ya facebook/jambotz

Thursday, December 22, 2016

UWEZO WA WANAWAKE KUPATA MIMBA WASHUKA TANZANIA

Viwango vya wanawake kuweza kupata mimba nchini Tanzania vimepungua hadi 5.2 kwa kila mwanamke nchini Tanzania mwaka 2015/2016 kutoka 6.2 kwa kila mwanamke miaka ya 1991/92, kulingana na utafiti wa afya nchini humo

Kulingana na gazeti la The Citizen la nchini Tanzania, utafiti huo uliofanywa na kutolewa na Afisi ya kitaifa ya Takwimu nchini humo NBS wiki iliopita unaonyesha kushuka kwa viwango vya uwezo wa kushika mimba miongoni mwa wanawake .

Kwa mfano mwaka 1996 ripoti hiyo inaonyesha watoto 5.8, mwaka 2004/05} ni watoto 5.7 mwaka 2010 ni watoto 5.4.

WAJUMBE WAIDHINISHA USHINDI WA TRUMP

Wajumbe wa jopo la wateule wanaoamua ushindi wa rais wa Marekani, wamemwidhinisha Donald Trump kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba 8, mwaka huu.

Hatua hiyo imezima juhudi za dakika za mwisho za kutaka kumzuia Trump kuingia ikulu ya White House Januari 20.

Baada ya ushindi huo, Trump ameahidi ‘kufanya kazi kuunganisha nchi yake na kuwa rais wa Wamarekani wote’.

RAIS WA GAMBIA ASEMA HANG'ATUKI MADARAKANI NG'OO............!!!

Rais wa Gambia Yahya Jammeh ameonya kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa kieneo kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na mfanyibiashara Adama Barrow.

Akihutubia wanachama wa muungano wa Bar Afrika nchini humo Bw Jammeh alisema: ''Waje wajaribu kuniondoa.wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka mshindi''.

Amesema kuwa alikataa wito wa muungano wa viongozi wa mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia.

Saturday, December 10, 2016

RAIS DR. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA DANGOTE IKULU DAR ES SALAAM

Rais Magufuli alivyokutana na Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kumaliza kwa kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza kikao chake na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo  Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

Tuesday, November 01, 2016

WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE KUANZA MITIHANI LEO, WAZIRI AONYA UDANGANYIFU

 
Wanafunzi wa kidato cha nne wakimsikiliza naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo mara baada ya kukagua maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne unaofanyika Leo. 
 

Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiagana na wanafunzi wa  shule ya sekondari Msalato mara baada ya kuzungumza nao.

Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, amefanya ziara kwenye shule mbalimbali mjini Dodoma kuangalia maandalizi kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne unaoanza Leo nchini.

Katika ziara yake kwenye Shule ya sekondari Jamhuri, Kiwanja cha ndege na Msalato, Jafo amewaonya walimu na wanafunzi hao nchini kuepukana na vitendo vya udanganyifu.

Akizungumza na walimu na wanafunzi katika shule hizo, Jafo amesema katika mtihani huo hawatarajii kuwepo na udanganyifu kwa kuwa wamejifunza kupitia mtihani wa darasa la saba ambapo kumekuwepo na tabia ya walimu kujificha chooni ili kuwasaidia wanafunzi.
Amesema shule zitakazofanya fanya hivyo zitakuwa zimepoteza thamani yake. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

WANAWAKE WANAOFANYA NGONO BILA KINGA WANAUWEZEKANO MKUBWA WA KUPATA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala akiwa anazungumza na waandishi wa habari wanawake kuhusu tatizo la Saratani ya shingo ya Kizazi, katika Ukumbi wa Olasiti Lodge Jijini Arusha, aliyepo kushoto kwake ni Dkt. Mathew Kasumuni kutoka hospital ya Mountmeru iliyopo jijini Arusha.
Waandishi wa habari wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala, Aliyepo kushoto kwake ni Dkt. Mwanahamis Ghembe kutoka Mountmeru Hospital.

Naibu waziri wa Afya Hamisi Kigwangala amesema kuwa wanawake wanaoshiriki tendo la ndoa bila kinga wapo hatarini kupata virusi vinavyoitwa HPV vinavyosababisha   Saratani ya mlango wa kizazi.

Kigwangala amesema wanawake wanaofanya ngono bila kinga wanaweza kupata saratani ya mlango wa kizazi, ambapo husababishwa kwa kufanya ngono bila kinga,huambukizwa  kwa kujaamiana. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 1, 2016 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

20161101_041402

20161101_041409

20161101_041420

Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

Thursday, October 27, 2016

SERIKALI YATANGAZA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2016

Serikali imetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la 7 kwa mwaka 2016 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.52 na shule iliyoongoza kitaifa ni shule ya Msingi Kwema ya mkoani Shinyanga. 

Mtihani huu ulifanyika tarehe 7 na 8 mwezi Septemba mwaka huu. Kutazama matokeo hayo bofya hapa.

Wednesday, October 26, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATANO OCTOBA 26, 2016 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

20161026_041718
20161026_041734
20161026_041746

Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

MPIGIE KURA RAIS MAGUFULI ASHINDE TUZO ZA MTU MASHUHURI ZA FORBES

Rais John Magufuli ni miongoni mwa watu mashuhuri barani Africa waliopendekezwa kuwania tuzo ya FORBES AFRICA PERSON OF THE YEAR 2016.

Mpaka sasa rais Magufuli anaongoza kwa 80% ya kura zote zilizopigwa. Unaweza kumpigia kura yako hapa.

Share na wenzio.

Tuesday, October 25, 2016

MABUSHA TATIZO LA WENGI JIJINI DAR

UTAFITI uliofanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii unaonyesha kuwa wakazi wa Mkoa wa Dar es salam 6800 tayari wamepata athari ya matende na mabusha. 

 Akizungumza katika zoezi hilo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk Grace Magembe alisema mpaka sasa tayari watu 104 kwa Mkoa wa Dar es Salaam wameshafanyiwa upasuaji wa mabusha. 

Alisema kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wa mabusha Jijini Dar es Salaam wanatarajia kuwafanyia upasuaji wagonjwa 1000. 

Akizungumza wakati wa ugawaji wa dawa za kinga tiba ya Matende, Minyoo na Mabusha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, alisema kuwa kiwango hicho ni kikubwa sana kwa wakazi wa dar es salaam kwani mpaka sasa watanzania milioni 2.7 wameathirika na magonjwa yasiyopewa kipaumbele ikiwemo ngiri maji pamoja na matende hususani vijijini. 

Alisema zoezi la utoaji wa dawa za kinga tiba litatolewa bure ambapo zaidi ya watanzania milioni 4.5 wanatarajiwa kupata kinga tiba hizo. 

 “Kinga tiba imeanza kutolewa Oktoba 25 hadi 29 kwa watu wenye umri kuanzia miaka 5 na kuendelea kwa kumeza dawa za Mectizan na Albendazole za kukinga na kutibu magonjwa ya minyoo tumbo,mabusha na matende,” alisema Makonda.

FORBES: RAIS MAGUFULI KUWANIA TUZO YA FORBES YA MTU MASHUHURI

Ikiwa ni mwaka mmoja tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu,Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania tuzo la Forbes la mtu mashuhuri wa mwaka.

 Jarida hilo la biashara limemtambua rais Magufuli kwa umuhimu wake katika kuimarisha uchumi wa taifa. Wengine walioteuliwa kuwania tuzo hiyo ni pamoja na Benki ya Capitec nchini Afrika Kusini, Rais wa Mauritania, Mtetezi wa haki za umma nchini Afrika Kusini na raia wa Rwanda. 
Mwaka uliopita tuzo hilo lilichukuliwa na mfanyibiashara wa Tanzania Mohammed Dewiji.

Chanzo: BBC Swahili

Sunday, October 02, 2016

MSANII WA JAMAICA ALIYEJICHORA TATTOO YA MAGUFULI....!!!

Las Laciano

Mwanamziki wa Jamaica Las Laciano aliyewahi kutamba na nyimbo kadhaa, ikiwemo "its me against jah" amejichora tatoo ya rais kutokea Africa anayemkubali, ambaye ni rais wa Tanzania Mh. Dr. John Magufuli. 

Sababu ni kuwa ndo rais muwajibikaji, anayeona mbele hatishiwi na matatizo ya mpito ila anatishiwa na matatizo ya muda mrefu kama rushwa, urasimu na uzembe kazini. Mheshimiwa Magufuli ameendelea kugonga kimataifa na anazidi kukubalika.

Like page yetu ya facebook ya Jambo Tz.
https://m.facebook.com/jambotz/

Wednesday, September 21, 2016

TAZAMA PICHA ZAIDI ZA NDEGE MPYA YA TANZANIA




Like page yetu ya facebook ya Jambo Tz.

NDEGE MPYA YA ATCL YAWASILI NCHINI, YA PILI ITATUA WIKI IJAYO

Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa. 

Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake (Water Salute). 

Baada ya kupokewa ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga). Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye.

Tuesday, September 20, 2016

PICHA ZAIDI ZA AJALI YA BUS LA NEW FORCE ILIYOTOKEA MKOANI NJOMBE



Watu 12 wamefariki dunia katika ajali ya basi la kampuni ya New Force lililokuwa likisafiri kutoka Dar kwenda Songea jana, katika watu waliofariki kati yao wanaume ni 4 na wanawake 8. Huku majeruhi wakiwa 19. Zoezi la uokozi lilimalizika majira ya saa 8 usiku.

Tuesday, August 23, 2016

POLISI WAMZUIA LOWASSA KUINGIA RUKWA

Msafara wa aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa umekwama kwenda Mikoa ya Rukwa na Katavi baada ya polisi kuuzuia kwa hofu kwamba unaweza kuingilia ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anayetembelea mikoa hiyo.
Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alianzia ziara yake mkoani hapa tangu Agosti 21 na juzi alifanya vikao vya ndani katika majimbo yanayoshikiliwa na wabunge wa chama chake mkoani Songwe wakati leo asubuhi alitarajiwa kwenda Katavi na Rukwa.
Katika Mikoa ya Rukwa na Katavi alitarajiwa kufanya mikutano ya ndani Majimbo ya Nkasi Kaskazini na Kusini na Sumbawanga. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wanayoiita ‘Kanda ya Nyasa’, Frank Mwaisumbe alisema kwamba polisi walimpigia simu Lowassa juzi saa 1.00 jioni akiwa Tunduma wakimtaka aahirishe ziara yake Mkoa wa Rukwa.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa, Gorge Kyando alipoulizwa kwa njia ya simu alisema waliwashauri viongozi wa Chadema wapange siku nyingine ya ziara kwa sababu mkoa ulikuwa na ugeni mkubwa.

MAZEMBE YAICHAPA YANGA 3-1 NA KUONGOZA KUNDI A

MZ 6
Mchezo wa mwisho wa Kundi A michuano ya kombe la Shirikisho Afrika kati ya TP Mazembe dhidi ya Yanga umemalizika kwa Yanga kukubali kichapo cha magoli 3-1 ikiwa ugenini na kuendeleza rekodi yake ya kutoshinda michezo yake mitatu ya hatua ya nane bora msimu huu.
Bolingi alianza kuifungia Mazembe bao la kwanza dakika ya 28 kipindi cha kwanza.
Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

MZ 4
Yanga ilipata pigo dakika mbili baada ya kuruhusu goli, Andrew Vicent ‘Dante’ alioneshwa kadi nyekundu na kuiacha Yanga ikicheza pungufu kwa dakika zote zilizobaki.
MZ 2
Dakika 11 baada ya kipindi cha pili kuanza, Rainford Kalaba aliifungia Mazembe bao la pili kabla kuongeza bao lake la pili likiwa ni bao la tatu kwa Mazembe mnamo dakika ya 64.
Amis Tambe aliifungia Yanga bao pekee akiunganisha mpira uliogonga ‘mtambaa panya’ baada ya Haruna Niyonzima kupiga mpira wa adhabu ndogo.
MZ 5
Matokeo hayo yanaipa Mazembe fursa ya kuongoza Kundi A kwa pointi 13 bila kujali matokeo ya wapinzani wake Medeama na MO Bejaia.
Yanga  imemaliza ikiwa nafasi ya nne (yamwisho) kwenye Kundi A ikiwa na pointi nne baada ya kupata ushindi katika mechi moja (Yanga 1-0 MO Bejaia) sare moja (Yanga 1-1 Medeama) huku mechi nyingine nne ikiwa imepoteza. (MO Bejaia 1-0 Yanga, Yanga 0-1 TP Mazembe, Medeama 3-1 Yanga, Mazembe 3-1 Yanga).
Yanga imefunga jumla ya magoli 9 huku yenyewe ikiwa imefunga magoli manne.
Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...