Monday, July 27, 2015

RAIS OBAMA AWASILI NCHINI ETHIOPIA


Rais Barack Obama wa Marekani hatimaye amefika nchini Ethiopia katika ziara yake ya pili ya nchi za Afrika.

Ni mara yake ya kwanza tangu aongoze taifa la Marekani akiwa rais kuhutubia wanachama hamsini na mbili wa umoja wa Afrika katika makao makuu yake yaliyoko Addis ababa.

Mazungumzo yao yakiwa yamelenga kutafuta suluhu ya kutokomeza migogoro ya vita za wenyewe kwa wenyewe sudan ya kusini. 

Rais Obama, aliwasili nchini Ethiopia akiwa anatokea mjini Nairobi ambako aliwaambia wakenya kuwa amna kikomo cha kile wanachokihitaji na kusisitiza kwa kutoa angalizo katika athari za ukabila na rushwa. 

Tamaduni mbaya kama unyanyasaji wa kijinsia, ndoa za kulazimishwa, tohara kwa watoto wa kike na kutopeleka watoto shuleni.

MSANII BOBBI KRISTINA AFARIKI DUNIA


Bobbi Kristina afariki Dunia

Bobbi Kristina Brown, mtoto wa marehemu Whitney Houston ambaye alikuwa gwiji wa muziki wa R&B, amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa miezi sita tangu alipokutwa taabani kwenye bafu lake na pindi alipofikishwa hospitalini na kukutwa na matatizo kwenye ubongo.

Bobbi amekufa akiwa na umri wa miaka 22,huku akivutiwa kuwa muigizaji na muimbaji mahiri na mwenye ubora wa aina yake. Msemaji wa familia Kristen Foster amesema Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na familia yake, ''hatimaye yuko salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu,tunawashukuru wote walioungana nasi katika maombi na kuonesha upendo kwa miezi michache iliyopita''.

Bobbi ambaye alikuwa amepoteza fahamu tangu akutwe ameanguka kwenye bafu lake panapo tarehe 31 januari mwaka huu na kuwekwa kwenye matibabu huku akiwa amekosa ufahamu na mpaka kifo chake kumkuta alikuwa hajapata fahamu bado.

Inakumbukwa kuwa miaka mitatu iliyopita mama yake Bobbi,alikutwa pia kwenye bafu lake amepoteza fahamu baada ya kupitliza kiwango cha dawa za kulevya na pombe mwishowe kufa. Bobbi alikuwa mtoto pekee wa Whitney Houston na Bobby Brown,magwiji wa muziki wa miondoko ya R &B.

Sunday, July 26, 2015

MLIPUKO WAUA WATU 10 SOMALIA


Takriban watu 10 wameuawa katika mlipuko huo

Takriban watu 10 wameuawa kufuatia mlipuko mkubwa uliotokea katika hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Mwandishi wa BBC katika mji huo anasema kuwa lori moja lilitumiwa kushambulia hoteli ya Jazeera karibu na uwanja wa ndege wa taifa hilo. Wajumbe wa kimataifa wamekuwa wakiishi katika hoteli hiyo ambayo imelengwa katika siku za nyuma.

Ripota wetu anasema kuwa ni moja ya mashambulizi mabaya kuwahi kushuhudiwa mjini Mogadishu. Anasema kuwa magari ya ambulansi yameanza kuokota miili.

14 WAFA KATIKA SHAMBULIO CAMEROON


Watu 14 wameuawa jana usiku katika shambulizi la bomu lililotekelezwa na Boko Haram

Watu 14 wameuawa jana usiku katika shambulizi la bomu lililofanyika kwenye jumba moja la starehe katika mji wa Maroua Kaskazini mwa Cameroon.

Siku chache baada ya kutokea kwa mashambulizi mawili ya bomu katika mji mkuu wa eneo hilo kulingana na habari kutoka kwa maafisa wa usalama. Afisa mmoja wa jeshi lililopelekwa katika eneo hilo kupambana na Boko Haram ndiye aliyetoa habari hiyo kwa siri.

Shambulizi hilo lilifanyika saa mbili kasorobo jana usiku saa za Afrika Mashariki wakati mwanaume mmoja alirusha bomu ndani ya baa katika wilaya ya Ponre kulingana na afisa huyo wa jeshi ambaye hakutaka kutajwa. Wakazi walijaribu kumfuata lakini aliwarushia grunedi kuwafukuza.

Saturday, July 25, 2015

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 25, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.
.
Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

WEMA SEPETU ALA ‘NGUMI’ ZA USO UBUNGE SINGIDA

Wema
Msanii maarufu wa filamu nchini, Wema Abraham Sepetu amepigwa chini katika kura za maoni kugombea ubunge wa viti maalum Singida.
 
Aysharose Mattembe ndiye ameibuka kidedea akimtupa kwa mbali Madam Wema aliyeshika nafasi ya nne.
11228022_1051907251486527_8461334309566372025_n 
Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

ZLATAN YUKO TAYARI KUKIPIGA MAN UNITED, ILA ANAHOFIA JAMBO MOJA


2ABD88C600000578-0-image-a-66_1437751952554
Mshambuliaji msumbufu na mwenye majivuno, Zlatan Ibrahimovic maarufu kama ‘Cadabra’ amesema angependa kuichezea Manchester United siku moja lakini anahofia ‘ngumi’ za kila siku na kocha Louis Van Gaal.

Akiwajibu waandishi wa habari kama yuko tayari kujiunga na mashetani hao wekundu, Cadabra alisema angeweza kuchezea United lakini anahofia ugomvi wa kutoisha baina yake na Louis Van Gaal.

Zlatan na Van Gaal hawakuwa na mahusiano mazuri tangu wakiwa Ajax miaka ya 1990’s lakini moto uliwaka zaidi baada ya Zlatan kumtaja Van Gaal kama ‘pampasi’ katika kitabu chake.

Wawili hao hawana urafiki na kwamba hawawezi kuiva chungu kimoja. Hisia zimekuwa ni nyingi miongoni mwa mashabiki mara baada ya kocha Louis Van Gaal kutangaza kwamba atafanya usajili wa kushitukiza wa mshambuliaji siku za usoni.

Hata hivyo Cadabra nahodha wa Sweden anahusishwa na tetesi za kujiunga na AC Milan ya nchini Italia. Habari zinasema Zlatan amechoshwa na quality ya ligi nchini Ufaransa na sasa anafikiria kuihama klabu yake ya Paris St. Germain. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

HATIMAYE WAYNE ROONEY AMJIBU VAN GAAL

2AD1593000000578-3173794-image-m-25_1437770313268
Wayne Rooney amesema yuko tayari kuwa mfungaji bora wa Manchester Unites kwa mara nyingine na amewapa changamoto wenzake ya kuandika Historia msimu ujao.
 
Nyota huyo wa England alicheza namba nyingi msimu uliopita chini ya Louis van Gaal na ikifika wakati akashushwa mpaka kiungo cha chini.
 
Kwasasa Rooney anataka kucheza namba anayoipenda yaani namba 9 na amesema yuko tayari kufunga magoli.
 
“Niko tayari kubadili akili yangu na kuwa moja ya wafungaji wa magoli,” Amesema nyota huyo wa zamani wa Everton ambaye msimu uliopita aliifungia United magoli 12.
 
“Nataka kucheza nafasi ya mshambuliaji ambapo nadhani ninaweza kufunga, naamini naweza kulitekeleza hilo”
Rooney performed a number of roles for Manchester United last term but is keen to play as a number nine
Msimu wa 2009-10 na 2011-12, Rooney alifunga magoli 34 kwenye mashindano yote akicheza nafasi ya mshambuliaji wa kati na kama atarudishwa nafasi hiyo anaweza kufanya vizuri.
 
Siku za karibuni, kocha wa Man United, Louis van Gaal alisema anatarajia kumtumia Rooney kama mshambuliaji wa kati msimu ujao na maneno haya ya Wayne ni majibu kwa bosi wake. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

HATIMAYE WAYNE ROONEY AMJIBU VAN GAAL

2AD1593000000578-3173794-image-m-25_1437770313268
Wayne Rooney amesema yuko tayari kuwa mfungaji bora wa Manchester Unites kwa mara nyingine na amewapa changamoto wenzake ya kuandika Historia msimu ujao.
 
Nyota huyo wa England alicheza namba nyingi msimu uliopita chini ya Louis van Gaal na ikifika wakati akashushwa mpaka kiungo cha chini.
 
Kwasasa Rooney anataka kucheza namba anayoipenda yaani namba 9 na amesema yuko tayari kufunga magoli.
 
“Niko tayari kubadili akili yangu na kuwa moja ya wafungaji wa magoli,” Amesema nyota huyo wa zamani wa Everton ambaye msimu uliopita aliifungia United magoli 12.
 
“Nataka kucheza nafasi ya mshambuliaji ambapo nadhani ninaweza kufunga, naamini naweza kulitekeleza hilo”
Rooney performed a number of roles for Manchester United last term but is keen to play as a number nine
Msimu wa 2009-10 na 2011-12, Rooney alifunga magoli 34 kwenye mashindano yote akicheza nafasi ya mshambuliaji wa kati na kama atarudishwa nafasi hiyo anaweza kufanya vizuri.
 
Siku za karibuni, kocha wa Man United, Louis van Gaal alisema anatarajia kumtumia Rooney kama mshambuliaji wa kati msimu ujao na maneno haya ya Wayne ni majibu kwa bosi wake. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

Friday, July 24, 2015

WAJUMBE WA CCM WAPATA AJALI, MMOJA AFARIKI


Mtu mmoja amefariki Dunia baada ya basi Dogo aina ya toyota HIACE, lililokuwa limewabeba wajumbe wa chama cha mapinduzi wa kata ya Milanzi kwenye manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, waliokuwa kwenye kampeni za kura za maoni za udiwani kuacha njia na kupinduka, ambapo pia ajali hiyo imeacha majeruhi kumi na moja.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga, mwenyekiti wa CCM wa kata ya milanzi Bw. Edgar Mwanandenje ambaye ni miongoni mwa majeruhi hao, amesema walikuwa wakitokea kwenye mchakato wa kampeni ya kura za maoni katika kata yao, ndipo dereva wa basi hilo dogo alipolazimisha kuipita kwa kasi pikipiki aina ya bajaj iliyokuwa mbele yao, na kupoteza mwelekeo kabla ya kupinduka. 

Katibu wa ccm wilaya ya sumbawanga mjini Bw Gabriel Kiula akiongelea juu ya ajali hiyo,amemtaja aliyepoteza maisha kuwa ni Didas Mwanisenga aliyekuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya kata ya milanzi, huku kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw. Jacob Mwaruanda akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

EU YAJADILI KUKATA MISAADA BURUNDI


Bendera ya Burundi

Muungano wa Ulaya EU umeanza kikao maalum kujadili uwezekano wa kukata msaada wake nchini Burundi. Inakisiwa kuwa fedha kutoka muungano huo unafikia zaidi ya nusu ya bajeti nzima ya Burundi ya kila mwaka. 

Mkuu wa masuala ya kigeni wa Muungano wa EU Federica Mogherini, ameelezea wasiwasi wake juu ya ghasia zilizototokea nchini humo kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais, na ametilia shaka iwapo serikali itakayoundwa baada ya uchagzui huo itakuwa wakilishi ya taifa nzima. 

Upande wa uchaguzi ulisusia kura hiyo iliyofanywa siku ya Jumanne. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa Ijumaa hii Uamuzi wa Rais Pierre Nkurunzinza kuwania urais kwa muhula wa tatu umetajwa kwenda kinyume na mkataba waliosaini mjini Arusha miaka kumi na tano iliyopita, ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mingi.

Ghasia zimezuka nchini humo tangu rais Pierre Nkurunzinza kutangaza kuwania kiti hicho ambapo zaidi ya watu laki moja wamikimbia nchi hiyo huku makumi ya maelfu wengine wakiuawa katika maandamano. Juhudi kadhaa za kuleta upatanishi kati ya makundi hasimu zimeambulia patupu.

BUHARI "MAREKANI INAWASAIDIA BOKO HARAM"


Rais Mahammadu Buhari akiwa na mwenyeji wake Obama alipokua ziarani nchini Marekani wiki hii.

Marekani "inawasaidia na kuchochea " kundi la wanamgambo wa kiislam wa Boko Haram kwa kukataa kutoa silaha kwa Nigeria, ni kauli ya rais wa Nigeria Mahammadu Buhari.

Sheria ya Marekani inazuia serikali kuuza silaha kwa nchi ambazo zinashindwa kushughulikia ipasavyo masuala ya haki za binadamu.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alikutana na rais Barack Obama Jumatatu kuomba msaada zaidi. Boko Haram limewauwa watu 10,000 tangu mwaka 2009 na limewateka mamia ya wasichana na wanawake.

Thursday, July 23, 2015

MATOKEO YA KURA ZA MAONI UBUNGE CHADEMA MBEYA NA MAJIMBO MENGINE

http://jambotz8.blogspot.com/

http://jambotz8.blogspot.com/

YANGA SC YAZINDUKA, YAWAPIGA 3-0 TELECOM, MSUVA NA TAMBWE WAKOSA PENALTI

Yanga imerejea katika michuano ya Kagame baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Telecom ya Djibout katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jana.

Katika mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo, Yanga ilianza kwa kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia huku mshambuliaji wake Donald Ngoma akilambwa kadi ya nyekundu.

Malimi Busungu ndiye shujaa baada ya kufunga mabao mawili huku Geofrey Mwashuya, akifunga bao la tatu.

BENTEKE AHAMIA LIVERPOOL RASMI


Christian Benteke

Timu ya Livepool imekamilisha kumsajili rasmi mshambuliaji mwenye asili ya Jamuhuri ya Kidemokrasia wa kongo Christian Benteke kutoka Aston Villa kwa kitita paundi milion 32.5. 

Benteke alikubali mkataba wa muda mrefu na kuwa mchezaji wa pili kununuliwa kwa gharama kubwa huko England.

Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji ameifunga magoli 49 katika mechi 101 alizocheza kwenye timu yake ya zamani ya Aston Villa.

Wednesday, July 22, 2015

KURA ZAANZA KUHESABIWA BURUNDI


Rais Pierre Nkurunziza

Shughuli ya kuhesabu Kura imeanza nchini Burundi kufuatia uchaguzi wa urais ambao umeshutumiwa na wengi nchini humo na hata kimataifa.

Rais Pierre Nkurunzinza anatarajiwa kupata ushindi mkubwa kwa muhula wa tatu huku upinzani ukisusia kabisa kura hiyo.

Huku hayo yakijiri Marekani na Uingereza wamekashifu kura hiyo wakisema kuwa haikuwa ya huru na haki. Marekani kwa upande wake imependekeza kugawana madaraka huku ikitishia kuchukua hatua dhidi ya Burundi iwapo muafaka hautapatikana.

Tuesday, July 21, 2015

UCHAGUZI UMEEANZA NCHINI BURUNDI


Uchaguzi wa urais umeanza Burundi

Baada ya ghasia na maandamano ya miezi kadhaa, hatimaye raia nchini Burundi sasa wamefika katika vituo vya kupiga kura ili kumchagua rais wao. Watu wawili wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu Bujumbura.

Foleni zimeonekana katika vituo vya kupigia kura

KESI YA RAIS WA ZAMANI WA CHAD YAAHIRISHWA HADI SEPTEMBA

Rais wa zamani wa Chad arejeshwa kortini 

Kesi ya kihistoria dhidi ya Kiongozi wa zamani wa Chad Hissene Habre iliyokuwa imerejeshwa mahakamani leo nchini Senegal sasa imeahirishwa hadi mwezi Septemba.

Mahakama imetoa muda huo kwa wakili wapya wa kiongozi huyo wa zamani wa kimla kujiandaa kwa kesi inayomkabili ya makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu, ukatili na uhalifu wa kivita.

Bwana Habre ambaye amekataa kuitambua mahakama hiyo alikataa kuzungumza mahakamani huku akiwashauri wakili wake wasimwakilishe mahakamani.

KITIMTIM MICHUANO YA KLABU BINGWA ULAYA

Michuano ya Klabu Bingwa Ulaya inaendelea tena hii leo kwa timu zile zinacheza round ya kwanza ambapo Dila Gori ya Geogia itakuwa na kibarua kigumu itakapoumana vikali na Partizan Belgrade ya Serbia.

Huku FC Pyunik ya Armenia ikikutana uso kwa uso na Molde ya Norway.

Milsami ya Boldova itapimana nguvu na Ludo Bulgaria.

Mechi nyingine za Klabu Bingwa barani Ulaya hapa chini Dila Gori v Partizan Belgrade 13:30

FC Pyunik v Molde 15:00

Milsami Orhei v Ludo Razgd 16:00

HJK Helsinki v FK Ventspils 17:00

Maccabi Tel Aviv v Hibernians FC 18:30

Lincoln Red Imps v FC Midtjylland 19:00

Vardar v Apoel Nic 19:00

Zalgiris v Malmö FF 19:10

Crusaders FC v Skenderbeu Korce 19:45

Monday, July 20, 2015

NCHIMBI AENGULIWA KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE...!!!

Dr. Emmanuel Nchimbi

KAMATI ya Siasa ya chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Songea Mjini imetupilia mbali fomu ya mgombea UBUNGE Dr. Emmanuel Nchimbi kwa madai kuwa fomu hiyo haikuwa na vigezo na kusababisha kushindwa kuijadili baada ya mgombea kutokuwepo kwenye kikao hicho.

Akizungumza asubuhi ya leo ofisini kwake katibu wa CCM wa Wilaya hiyo Juma Mpeli alisema kuwa mpaka jana majira ya saa kumi jioni fomu za kugombea ubunge jimbo la Songea Mjini zilipokelewa tisa (9) lakini fomu moja ya Dr. Nchimbi ilikuwa imechukuliwa na mmoja wa wakazi wa Songea na ikalejeshwa siku hiyo hiyo ikiwa imejazwa.

Alisema kuwa fomu hiyo ya mgombea ilishindikana kujadiliwa kwa kuwa mgombea mwenyewe Dr. Nchimbi hakuwepo kwenye kikao ambacho wagombea wote waliitwa kujadiliwa kadri ya maelezo waliyoyatoa kwenye fomu ya kugombea ubunge kwenye jimbo hilo.

MAN U KUTOONGEZA WASHAMBULIAJI

Kocha Mkuu wa Manchester United Louis Van Gaa

 Kocha mkuu wa Manchester United Louis Van Gaal ametamba kuwa hatanunua mwingine kwani alio nao kwa sasa wanatosha wakiongozwa na Wayne Rooney.

Pamoja na Wayne Rooney washambuliaji wengine waliobaki ni Javier Hernandes Chicharito, na James Wilson baada ya mshambuliaji mpachika magoli Robin Van Persie kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki hivi karibuni na Radamel Falcao mkopo wake kumalizika.

Van Gaal anatarajia kumtumia Rooney kama mshambuliaji pekee pale mbele ambapo atasaidiwa na Mephis Depay aliyesajiliwa wakati wa majira ya joto kutoka PSV Eindhovenya Uholanzi. Van Gaal anatamba kuwa Depay anaweza kuwa mshambuliaji wa katikati tofauti na alivyokuwa akitumika wakati alipokuwa PSV.

Saturday, July 18, 2015

WAZEE WA KIMILA MONDULI WAMUANGUKIA LOWASSA

Wazee wa kimila wa jamii ya wafugaji wa Kimaasai (Malaigwanan) kutoka Wilaya ya Monduli wamemuomba waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kubaki na kuendelea kuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu ndicho kilichomlea na anakijua.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Monduli kwa niaba ya Malaigwanan, Mzee Joseph Mesopiro kutoka Kata ya Sepeko wilayani humo alisema viongozi wa mila wanakusudia kutuma ujumbe maalumu kwa Lowassa kumshauri asihame CCM kama baadhi ya watu aliowaita wapambe wanavyomshauri.

“Sote Monduli tumesononeka kwa jinsi vikao vya chama vilivyomtendea mbunge wetu. Bado tunampenda kama ambavyo tunakipenda chama chetu. Tunaamini ataendelea kubaki CCM na kupigania ushindi wa chama katika uchaguzi ujao,” alisema Mzee MMesopiro

TUNAWATAKIA EID MUBARAKA WATU WOTE



Leo ni sikukuu kubwa sana duniani... ina maana kubwa sana kwa waislam na watu wote duniani.

Kwakulijua hili Jambo Tz tunachukua nafasi hii kuwatakia sikukuu njema watanzania wote na dunia kwa ujumla.

OBAMA KUTOTEMBELEA KIJIJI CHA BABA YAKE

Barack Obama

#ObamainKenya ndilo neno linalotawala mitandao ya kijamii nchini Kenya huku rais huyo akitarajiwa kulitembelea taifa hilo.

Hata hivyo wakaazi wa kijiji cha Kogelo ambapo babaake Obama alizaliwa na kulelewa sasa hawatalazimika kufanya maandalizi ya aina yoyote kufuatia ziara hiyo baada ya balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec kusema kuwa rais huyo hatozuru kijiji cha Kogelo.

''Ana mda mchache sana kwa hivyo basi atakuwa nairobi pekee'', alisema bwana Godec akizungumza na runinga ya KTN.

Bibiye Obama Sarah Obama alikuwa amejiunga na wakaazi wa Kogelo akimtaka Obama kuwatembelea kulingana na ripoti za kituo cha habari cha Capital fm.

Friday, July 17, 2015

MSAIDIZI WA NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA AJIUNGA NA CHADEMA

 Bw. Jumanne Juma Msunga.

MSAIDIZI wa Naibu Katibu Mkuu wa (CCM) Bara, Jumanne Juma Msunga ametangaza rasmi kuhama CCM na kujiunga na CHADEMA, kwa madai kuwa CCM ni chama cha kudhulumu haki za wanachama wake. 

Akitangaza uamuzi wake huo jana mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi za CHADEMA Mkoani Singida, Msunga alisema ameamua kujinga na CHADEMA, huku akidai kuwa CCM haikutenda haki katika mchakato mzima wa kumpata Mgombea wa nafasi ya Urais.

Alisema CCM haina shukrani kwani imejaa dhuluma kwani katika mchakato huo baadhi ya Wagombea walikatwa bila kujieleza mbele ya kamati husika.

WATU ZAIDI YA 40 WAFA KATIKA MLIPUKO NIGERIA

Wapiganaji wa Boko haram

Wafanyakazi wa uwokoaji Nigeria wanasema katika eno la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo katika mji wa Gombe watu arobaini wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya milipuko kutokea kwenye soko katika eneo hilo.

Mlipuko wa kwanza umetokea nje ya kwenye maegesho nje ya duka la viatu, na kufuatiwa na mlipuko mwingine muda mfupi baadae.

Mmoja ya wafanyakazi wa uokoaji miongoni mwa waliouwa ni wanawake na watoto. Mashuhuda wa tukio hilo amesema hali ni mbaya kwenye mitaa ya Gombe.

WANAJESHI WANNE WANAMAJI WAUAWA MAREKANI

Rais wa Marekani Barack Obama

Mtu mwenye silaha amewaua askari wanne wa jeshi la wanamajiwa Marekani katika shambulio lililofanywa kwenye majengo mawili ya jeshi hilo katika mji wa Chattanooga, Tennessee.

Wanajeshi hao wote waliuawa katika jengo moja. Maafisa nchini humo wameyaita mauaji hayo kuwa ni Shambulio la ndani. 

Shirika la Upelelezi la Marekani FBI linalochunguza mauaji hayo, limesema halijajua bado kilichosababisha shambulio hilo.

SIMBA KUCHEZA NA AFC LEOPARDS, SIMBA DAY 2015

Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Imani Kajula akiwa Pamoja na Rais wa Simba Sport Club, Evans Aveva, wakati wa uzinduzi wa Simba Day. 

Dima ya Simba Sports Club ya kuendeleza mabadiliko ndani ya Simba bado inaendelea kushika kasi, Katika kipindi cha miezi mitatu sasa, mmekuwa mashuhuda wa Simba inayolenga kuleta mapinduzi makubwa katika jinsi mpira unavyoendeshwa, kujali wanachama, wapenzi wake na kukuza vyanzo vya mapato.

Akizungumza wakati wa kutangaza rasmi Simba Week 2015 Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema ‘’Kila mwaka timu yetu ya Simba imekuwa na utaratibu wa kuwa na siku maalum kwa ajili ya kufurahi, kuwatambulisha rasmi wachezaji, jezi za timu na kujiandaa kwa msimu mpya, siku hii imekuwa maarufu kama Simba Day.

FIFA KUZIFANYIA MABADILIKO BAADHI YA KANUNI

Makao makuu ya FIFA

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA lina mpango wa kuzifanyia marekebisho kanuni zake ili kuzibana nchi zinazowania kuandaa Kombe la Dunia, zisitumie mwanya wa misaada ya kifedha kwa nchi nyingine kama rushwa.

Kipengele kile kinachoziruhusu nchi zinazoshindania nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia kusambaza pesa katika nchi nyingine huenda kikafutwa. 

Aidha FIFA inazitaka nchi zote zinazowania nafasi hiyo kuzingatia haki za binadamu na sheria za kazi wakati wote. Hivi sasa nchi zinazotupiwa jicho ni Urusi inayoandaa kombe la dunia mwaka 2018 na Qatar inayoandaa 2022. 

ura za kuamua nchi gani italiandaa Kombe la Dunia la mwaka 2026 zitapigwa mwaka 2017 huko Kuala Lumpur, Malaysia. Nchi zinazoiwania nafasi hiyo ni Marekani,Canada, Mexico na Colombia.

Tuesday, July 14, 2015

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...