Friday, April 06, 2018

SOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRIL 06, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS



SALMAN KHAN AHUKUMIWA KUFUNGWA JELA KWA KOSA LA UWINDAJI HARAMU

Mahakama nchini India imemuhukumu nyota muigizaji wa sinema za Bollywood Salman Khan, kifungo cha miaka mitano jela kwa kuua aina mojawapo ya swala ambao ni adimu kupatikana duniani mwaka 1988.

Mahakama hiyo iliyoko Jodhpur imemtoza faini ya rupia 10,000 ($154; £109) kwa kosa hilo.
Amepelekwa korokoroni na anatarajiwa kusalia huko kwa muda.

Khan aliwaua swala wawili kwa jina blackbucks, ambao hulindwa na kuhifadhiwa, Magharibi mwa jimbo la Rajasthan alipokuwa akiigiza filamu yake.

Thursday, April 05, 2018

CHADEMA WATAJA MAJINA 25 YA WAFUASI WAKE WANAOSHIKILIWA NA POLISI BILA KUPELEKWA MAHAKAMANI

Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa orodha ya majina ya watu 25, wakiwemo viongozi, wanachama na wafuasi wa wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam na kuwaagiza wanasheria wake kuchukua hatua zaidi za kisheria kwa kuwasilisha maombi ya ‘Habeas Corpus’, Mahakama Kuu, iwapo jeshi hilo halitawaachia au kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao kama taratibu zinavyotaka.

Chama hicho kimesema kimefikia uamuzi huo, kutokana na tabia ya Jeshi la Polisi kuendeleza utaratibu unaovunja haki na sheria kwa kuwakamata watu na kuwashikilia mahabusu za Polisi kinyume na matakwa ya taratibu za nchi.

Kati ya watu hao 25 wanaoshikiliwa na Polisi, mmoja ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, John Heche, ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Vijiji huku watu wengine 24 wakiwemo viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA waliikamatwa juzi wakiwa maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakifuatilia hatma ya dhamana ya viongozi wakuu wa chama mahakamani hapo.

BASI LA CITY BOYS LAGONGANA NA FUSO, 12 WAFARIKI, 46 WAJERUHIWA!

Basi la Kampuni ya City Boys lenye namba za usajili T983 DCE Scania limepata ajali ya kugongana na lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T486 ARB katika eneo la Makomero Tarafa na Wilaya Igunga Mkoa wa Tabora usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya watu 12 na wengine 46 kujeruhiwa.

Kaimu Mkuu wa Usalama Barabarani wa Mkoa wa Tabora, Insp Hardson, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni tairi la kulia la Fuso lilitumbukia kwenye mashimo mawili na kusababisha tairi kupasuka na rimu kupinda hivyo likakosa mwelekeo na kuligonga basi la City Boy uso kwa uso.

Insp Hardson amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya igunga huku baadhi ya majeruhi wakipelekwa Hospitali ya Nkinga na wengine Bugando Mwanza kwa ajili ya matibabu.

ALIEKUWA RAIS KUFUNGWA MIAKA 12 JELA

Mahakama ya rufaa nchini Brazil leo imeagiza aliekuwa rais wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva kuwa ni sharti aanze kutumikia kifungo chake cha miaka kumi na mbili gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika katika ufisadi.
Majaji sita kati ya kumi na mmoja wa mahakama ya rufaa walipinga rufaa hiyo huku watano kati yao wakimuunga mkono. Kesi hiyo imezua hali ya wasi wasi wa kisiasa nchini humo.

Lula amekutwa na hatia kutokana na uchunguzi wa muda mrefu wa sakata la rushwa linalojulikana kama ”Operation Car Wash" Lula aligundulika kukubali rushwa yenye thamani Euro laki 7.

WAZIRI ATAJA HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA

 Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi akizungumza na wadau wa utafiti wakati akifungua Warsha ya siku mbili kwa watafiti wa Tanzania na kutoka nje iliyoandaliwa na Tasisi ya Utafiti ya REPOA jana jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi  Amina Salim Alli akizungumza wakati anaongoza mjadala juu ya Uchumi wa Viwanda kufikia 2025
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesisitiza  Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na hatua  za kuhakikisha kunakuwepo mazingira wezeshaji yatayofanikisha ujenzi wa viwanda nchini. 

Prof.Kabudi amesema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya utafiti iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya REPOA ambapo mada kuu ilikuwa kujadili kuelekea jamii inayoendeleza viwanda 2025 kwanini ushindani ni muhimu.

Pia kwenye warsha hiyo wadau wamejadili masuala ya kisera katika safari ya Tanzania kuelekea kwenye uchumi mseto na shindani, ukiongozwa na viwanda, pamoja na kufikia nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama inavyotarajiwa kwenye dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

ZITTO KUMPELEKA NONDO UHAMIAJI KUHOJIWA

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema atamsindikiza kiongozi wa mtandao wa wanafunzi Abdul Nondo katika makao makuu ya uhamiaji Tanzania.
Hii ni baada ya taarifa iliotoka mtandao huo ambayo ilieleza kuwa Nondo alipata barua ya kuitwa na uhamiaji ili 'akahojiwe kuhusu taarifa za uraia wake pamoja na za ndugu zake'.

Taarifa hizo zilisema 'afisa uhamiaji mkoa alitamka kuwa sheria inawaruhusu kumuhoji mtu yeyote wanaotilia mashaka uraia wake. Na kuwa wanamashaka na uraia wa Abdul Nondo,hivyo awathibitishie kuwa yeye ni Raia wa Tanzania'.

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS APRIL 05, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS




Wednesday, April 04, 2018

TAZAMA MUONEKANO MPYA WA MBOWE BAADA YA KUKAA MAHABUSU KWA SIKU SABA



Baada ya kukaa mahabusu kwa siku saba na kusherehekea sikuu ya Pasaka wakiwa gerezani, Mwenyekiti wa Chadema Taifa  Mhe. Freeman Mbowe pamoja na vigogo wengine sita wa chama hicho leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia kwa dhamana, baada ya kukamilisha masharti.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRIL 04, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS





KIKWETE AINGILIA KATI AFYA YA MZEE MAJUTO, HII HAPA AHADI YAKE

LICHA ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume bado hali ya staa wa filamu za Kibongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ ni tete ambapo Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’, amejitosa baada ya kumuona alivyodhoofu kwa sasa.

JK na Mzee Majuto walikutana uso kwa uso wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar ambako kulikuwa na shughuli ya utoaji tuzo za filamu zilizojulikana kwa jina la Tuzo za Kimataifa za Sinema Zetu ambapo walionekana wakiteta kwa dakika kadhaa kabla ya kila mmoja akaenda kukaa kwenye siti yake.

Mzee Majuto alionekana akiwa amedhoofu kwani aliingia ukumbini akitembea kwa msaada wa fimbo huku akionekana kutokuwa mchangamfu kama ilivyo kawaida yake, hali iliyowahuzunisha mashabiki wake waliokuwa ukumbini hapo.

AGNES MASOGANGE AKWEPA KWENDA JELA BAADA YA KULIPA FAINI

Msanii wa kupamba video za muziki (Video Queen), Agnes Gerald ‘Masogange’ amekwepa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kulipa faini ya Sh. milioni 1.5.

Msanii maarufu nchini, Agnes Gerald maarufu Masogange alikutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya na kuhukumiwa kwenda jela au kulipa faini.

 Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri, ametoa hukumu hiyo leo Aprili 3 na kuieleza mahakama kuwa Masogange katika kosa la kwanza amekutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin na kosa la pili kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

“Hivyo katika kosa la kwanza, mahakama inamhukumu kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh1 milioni na kwa kosa la pili, amehukumiwa kwenda jela miezi 12 au kulipa faini ya Sh 500, 000,” amesema Hakimu Mashauri.

Februari 17 mwaka jana, aliyekuwa Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaeleza wanahabari kuwa Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kupimwa iwapo anatumia dawa hizo za kulevya.

NUKUU SITA (6) MAARUFU ZA WINNIE MANDELA ENZI ZA UHAI WAKE

Winnie Madikizela-Mandela, ex-wife of former South African President Nelson Mandela, arrives at the Union Buildings in Pretoria 27 April 2004 for the inauguration of President Tahbo Mbeki second and final term as the country celebrated the 10th anniversary of the end of apartheid. 
Winnie Madikizela-Mandela enzi za uhai wake.
 
Mwanasiasa na mwanaharakati aliyepigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini Winnie Madikizela-Mandela alifariki dunia Jumatatu akiwa na miaka 81.

Alikuwa mke wa zamani wa rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini Nelson Mandela lakini alikuwa na msimamo mkali zaidi kumshinda hata Bw Mandela mwenyewe. Winnie alifahamika sana na wengi kama Mama wa Taifa.
Winnie Mandela, former wife of former South African President Nelson Mandela attends the opening of the 53rd National Conference of the African National Congress (ANC) on December 16, 2012 in Bloemfontein.
Winnie alikuwa nembo kuu ya vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, na ingawa sifa zake ziliingia doa miaka ya baadaye, lakini bado alitambuliwa kama mtetezi wa wanyonge.

Tuesday, April 03, 2018

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRIL 03, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS

Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

MBOWE NA WENZIE KUACHIWA LEO...??!

Viongozi sita wa Upinzani nchini (CHADEMA) wanatarajiwa kuachiliwa kutoka kizimbani baada ya kulipa dhamana, siku ya Alhamisi.

Viongozi hao akiwemo mwenyekiti Freeman Mbowe, walishtakiwa kwa uchochezi, kuleta vurugu na kuandamana mwezi wa Februari mwaka huu.

Alhamisi iliopita, mahakama ya hakimu mkazi Kisutu iliwapatia dhamana viongozi hao sita lakini kusema kuwa watasalia rumande hadi kesi leo tarehe 3 Aprili ambapo wataletwa mahakamani kukamilisha masharti ya dhamana.

Wanasiasa hao hawakuletwa mahakamani katika uamuzi wa dhamana yao huku afisa wa magereza akiiambia mahakama ni kutokana na gari lililotakiwa kuwasafirisha kuja mahakamani hapo kuwa bovu.

Miongoni mwa mashtaka waliyosomewa ni pamoja na maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa chuo cha NIT Akwilina Akwiline. Wanashtakiwa pia kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali wilayani Kinondoni shtaka linalowakabili washtakiwa wote.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...