Thursday, August 21, 2014

MWINYI: SERIKALI HAIKUFUTA AZIMIO LA ARUSHA

Rais wa mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi
Rais wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi amesema serikali haijawahi kufuta Azimio la Arusha kama inavyodaiwa na baadhi ya wananchi, bali ilizimua azimio hilo kuwapatia viongozi wa kati uwezo wa kumudu makali ya maisha.
"Serikali haikufuta Azimio la Arusha. Ililizimua azimio hilo kuwapatia viongozi wa kati kumudu makali ya maisha, lakini baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia vibaya nafasi hiyo kuvunja sheria ya maadili ya viongozi," amesema.
Alhaji Mwinyi ameeleza hayo leo jijini Dar es Salaam katika semina ya siku moja ya maandalizi ya sheria ya kudhibiti mgongano wa maslai miongoni mwa viongozi na watumishi wa umma iliyoandaliwa na Sekretarieti ya Maadili ya viongozi.
"Baadhi ya watu wamekuwa wakitumia vibaya nafasi hiyo kuvunja maadili ya viongozi wa umma kwa kutumia raslimali za umma kujinufaisha. Tabia hii imewafanya wananchi kutokuwa na imani na viongozi wao," amesema.
Kwa mujibu wa Alhaji Mwinyi, mgongano wa maslai ini tatizo kubwa nchini linalotakiwa kuangaliwa kwa umakini vinginevyo baadhi ya viongozi wataendelea kujinufaisha kwa kutumia nafasi zao kazini.
Kwa upande wake Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi Jaji Salome Kaganda amesema lengo na makusudi ya mapendekezo ya sheria hii ni kuleta amani na utulivu wan chi.
Jaji Kaganda amesema, "mapendekezo ya sheria hii hayalengi kuwafanya viongozi kuwa maskini, bali kasi yao ya ukwasi iendane na halii halisi ya kipato chao."
"Sheria hii itakapopitishwa na ngazi husika, itapunguza ubinafsi wa viongozi walioko madarakani kujipendelea wenyewe na maeneo wanayotoka," amesema na kuongeza kuwa, "Lazima kuwepo na hatua uya serikali kurejesha maadili ya maadili. Kama itazingatiwa na kuheshuimiwa, taifa litafikia maendeleoo ya haraka yaliyokusudiwa." Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WAANDAMANAJI WAMTAKA NAWAZ SHARIF AJIUZULU

Waandamanaji wanaotaka waziri mkuu Nawaz Sharif ajiuzulu. Islamabad, Pakistan Aug. 19, 2014.
Waandamanaji wanopinga serikali nje ya bunge la Pakistan, hawaonyeshi ishara yoyote ya kuondoka,hadi pale waziri mkuu Nawaz Sharif atakapojiuzulu, dai ambalo serikali imekataa kwa misingi ya kuwai kinyume na katiba. Wakati huo, huo jeshi lenye nguvu la Pakistan limeonya pande zote kutatua mzozo wao kupitia majadiliano.
Maelfu ya waandamanaji wanopinga serikali wamekuwa katikati ya mji mkuu wa Pakistan kwa karibu wiki moja, katika juhudi za kumshinikiza waziri mkuu Nawaz sharif kujiuzulu.
Wote serikali na viongozi wa maandamano hayo hawaelekei kurudi nyuma, na hivyo kuongeza hofu ya mapambano baina ya polisi na waandamanaji hao kila kuchao.
Mwanasiasa wa upinzani Imran Khan na kiongozi mashuhuri wa kidini Tahir-ul Qadri, wameaanda maandamano ya umma, ingawa si kwa ushirikiano lakini wanamtaka waziri mkuu Sharif kuachia madaraka.
Maandamano hayo dhidi ya serikali yamelazimisha sehemu kubwa ya mji huo kufungwa na kuvuruga maisha ya kila siku pamoja na shughuli za kibiashara. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
CHANZO:VOA

RATIBA LIGI KUU BARA 2014/2015 YAANIKWA HADHARANI, MAXIMO KUANZA NA MTIBWA, PHIRI NA WAGOSI WA KAYA


Kocha mkuu wa Yanga akiongea na msaidizi wake
RATIBA ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 utakaoanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu umeanikwa hadharani na Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF.
Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo katika taarifa yake amesema ratiba hiyo imezingatia michuano ya Chalenji itakayochezwa Novemba, usajili wa dirisha dogo Nov 15- Des 15, ushiriki wa klabu za Azam na Yanga kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa (CL) na Kombe la Shirikisho (CC).
Wambura alisema mechi zitachezwa wikiendi ili kuongeza msisimko/kuwapa fursa washabiki wengi zaidi kuhudhuria, na katikati ya wiki imeachwa wazi kwa ajili ya mechi za Kombe la FA (Federation Cup).
DSC_0007-546x291
Kocha mkuu wa Simba sc Patrick Phiri akiongea na wachezaji wake  
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAREKANI YALAANI MAUAJI YA MWANDISHI

James Foley
Rais Barack Obama wa Marekani amesema mauaji ya mwandishi wa habari James Foley raia wa Marekani aliyeuawa na wapiganaji wa kundi la Kiislam yameishtua dunia.
Obama amesema kitendo hicho ni cha kikatili na kisichokubalika mbele za Mungu na kwamba ni matokeo ya mawazo duni yasiyoendana na karne ya sasa.
Kauli hiyo ya Rais Obama inakuja huku wazazi wa mwandishi huyo wakielezea kutoridhishwa kwao na hatua zinazochukuliwa na Marekani kutokana na mauaji ya mtoto wao.
Wazazi hao wamesema wakati mwingine waandishi wa habari huru hawathaminiwi katika aki zao hata pale wanapojitolea maisha yao kwa ujira mdogo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Wednesday, August 20, 2014

PAPA FRANCIS ATABIRI KIKFO CHAKE...!!!


Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis. PICHA|MAKTABA

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis kwa mara ya kwanza ametabiri hatima ya maisha yake duniani akisema kuwa anaamini Mungu anaweza kumpa muda wa miaka miwili au mitatu ya kuishi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ndege wakati akitoka ziarani Korea Kusini kurejea Vatican, Papa Francis alisema suala la kuendelea kuishi ni neema ya Mungu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WANAFUNZI BILA KUANDAMANA HAWAPATI HAKI ZAO...???


Sasa ni dhahiri kwamba Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (Tahliso) imepata mwarobaini wa matatizo yake, ikiwa ni pamoja na wanafunzi kulipwa stahili zao na mamlaka husika. Jumuiya hiyo imegundua kwamba mamlaka zilizopewa dhima ya kuhudumia elimu ya juu na kutatua matatizo ya wanafunzi hao hazifanyi hivyo hadi pale wanafunzi hao wanapotishia kuandamana nchi nzima. Ni utamaduni mpya unaotumiwa na baadhi ya viongozi wetu, kwamba wanafunzi, wakulima, madaktari na wananchi wengine watalipwa madai yao iwapo tu watafanya vurugu au kuandamana na kuitikisa dola.

Hivyo ndivyo ilivyotokea katika suala la madai ya wanafunzi hao ya kulipwa fedha za mafunzo kwa vitendo. Hivi sasa wanafunzi kutoka katika vyuo vya elimu ya juu wako sehemu mbalimbali nchini katika mafunzo kwa vitendo, lakini wanafunzi kutoka vyuo saba hawajalipwa fedha za kujikimu. Wanaishi vipi katika mazingira mageni wakiwa hawana fedha za chakula au malazi ni swali ambalo halina jibu. Viongozi wa Tahliso wamesema ucheleweshwaji wa fedha hizo zinazokadiriwa kuwa Sh6.6 bilioni umesababisha baadhi ya wanafunzi wa kike kudhalilishwa kimapenzi na kutupiwa vyombo vyao nje kwenye nyumba walizopanga.

Kutokana na hali hiyo, viongozi wa Tahliso walipanga kuongoza maandamano keshokutwa kwenda kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda hata kama maandamano hayo yangekosa kibali cha polisi. Pamoja na viongozi hao kukamatwa na polisi na baadaye kuachiwa kwa dhamana, walisisitiza kwamba lazima maandamano hayo yafanyike kwani Tahliso inasimamia haki za wanafunzi ambazo Serikali imeshindwa kuzishughulikia. Msimamo huo uliizindua Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB), ambayo ilitangaza jana katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, wanafunzi hao watakuwa wamelipwa fedha zao ifikapo wiki ijayo.

DR. NCHIMBI KUMRITHI MWIGULU

Dk. Nchimbi kumrithi Mwigulu 
MWELEKEO mpya wa mchakato wa Katiba mpya, adhabu kwa wagombea walioanza mbio za kusaka urais unatarajia unatarajia kujulikana leo baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu (CC), ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
CC ilikutana jana chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, ambaye alisema hana ajenda mfukoni kama ilivyodaiwa na baadhi ya watu.
“Nimekuja, Tuzungumze mambo yetu, tufanye uamuzi…..hivi mara ya mwisho kukutana ilikuwa  lini vile….aah mwezi uliopita” alisema mambo yetu.
Kikao hicho cha CC ambacho kilikuwa kianza saa nane mchana kama ilivyotangazwa kilianza saa tisa na nusu huku wajumbe wote wakiwa tayari ndani ya ukumbu isipokuwa viongozi wakuu.
Viongozi hao wakuu ni Rais Kikwete (Mwenyekiti), Katibu Mkuu Abdulrahman Knana, Makamu  Mwenyekiti (bara), Philip Mangula na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar) Dk. Alli Mohamed Shein.
Kabla ya Rais Kikwete, kuingia ukumbini Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alitoka faragha alikokuwa akizungumza na kwenda kuchukua nyaraka kwa Jenister Mhagama ambaye ni Katibu wa wabunge wa CCM na kurejea faragha ambapo alikaa kidogo kisha kurejea ukumbini kumuita Dk. Asharose Migiro.
Mara baada ya pilika pilika hizo, Rais Kikwete na viongozi wenzake waliokuwa faragha waliingia ukumbini ambapo Kinana alimkaribisha Rais Kikwete afungue mkutano huo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

OKWI: SINA MPANGO WA KURUDI BONGO

Emmanuel Okwi 
WAKATI uongozi wa Yanga ukidai hauna muda kuendelea kulijadili suala la mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi, mshambuliaji huyo naye amesema hana mpango wa kurudi kucheza soka Tanzania.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kupitia ukurasa wake wa Facebook, Okwi alisema hana mpango wa kurudi nchini kwa sasa, kwani anachoangalia ni kucheza soka barani Ulaya na sio Tanzania.
Awali, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alikaririwa akisema, wanachoangalia wao kwa sasa ni wachezaji gani wamefika na maendeleo yao katika mazoezi, sio kumfuatilia yule ambaye hajafika.
Okwi inadaiwa kwa anaidai Yanga zaidi ya sh. milioni 60 zilizotokana na fedha zake za kusajiliwa akitokea Etoile du Sahel ya Tunisia, huku akisaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya sh. milioni 160.
Hata hivyo klabu hiyo inatakiwa kuvunja mkataba na mchezaji mmoja wa kimataifa kutokana na kuzidi kwa idadi ya wachezaji watano wa kigeni kama zinavyotaka sheria za usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Wachezaji wengine wa kimataifa waliopo katika klabu hiyo ni Andrey Coutinho, Geilson Santos ‘Jaja’ raia wa Brazil, Mbuyu Twite wa Burundi, Hamis Kiiza wa Uganda na Haruna Niyonzima wa Rwanda. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

FURSA YA MIKOPO KATIKA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI

Serikali imetoa fursa ya mikopo kwa wanafunzi watakaojiunga na masomo ya stashahada maalum ya ualimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam.
" Wanafunzi wapatao 5,000 wanatarajiwa kujiunga na stashahada maalum katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo wote watanufaika na mikopo ya elimu ya Juu."Alisema Mwaisobwa
Akifafanunua, mwaisobwa alisema kuwa lengo la mpango huo ni kusaidia kuondoa tatizo la walimu wa masomo ya sayansi hapa nchini .
Aidha Mwaisobwa alibainisha kuwa jumla ya maombi 58,037 ya mikopo yalikuwa yamepokelewa hadi kufikia Julai 2014 ambapo maombi 37,689 ni waombaji wa kiume na 19,592 ni waombaji wa kike.
Pia Mwaisobwa alibainisha kuwa majina ya wanafunzi watakaopata mikopo kulingana na udahili yatatangazwa kwenye tovuti ya Bodi ambayo ni www.heslb.go.tz.na taarifa hiyo itatangazwa katika vyombo vya habari.
Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) inakusanya wastani wa shilingi bilioni 3 kwa mwezi ikiwa ni marejesho ya mikopo iliyokwisha tolewa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

PAPA FRANCIS AMRUHUSU PADRI KUOA...!!!

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.PICHA|MAKTABA 

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amekubali kumuondolea sakramenti ya upadri, Raymond Mosha wa Jimbo Katoliki la Moshi ikiwa ni miaka 20 tangu padri huyo aombe kuachana na daraja hilo.
Barua ya uamuzi wa Papa Francis ilisomwa juzi katika parokia na vigango vyote vya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi katika ibada zilizofanyika katika makanisa ya jimbo hilo.
Miongoni mwa parokia ambazo barua hiyo ilisomwa ni Karanga ambako Paroko wake, John Matumaini alitoa tangazo hilo katika ibada zote. Uamuzi huo ambao ni nadra kutolewa na Papa, unamaanisha kuwa sasa padri huyo yuko huru kuoa na kuwa na familia.
Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukitangazwa rasmi juzi, tayari Padri Mosha ambaye ni profesa wa falsafa na maadili katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Arusha, ana mke na watoto watatu ambao kwa sasa wako vyuo vikuu.
Padri Mosha alisema aliandika barua kuomba kuondolewa daraja hilo mwaka 1994 kabla ya uamuzi kutolewa juzi.
Katika orodha ya mapadre 185 wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi iliyopo katika tovuti ya jimbo hilo, jina la Padri Mosha linaonekana likiwa ni namba 23.
Akizungumzia hatua hiyo, Padri Mosha alisema: “Ninafurahi kufunguliwa kifugo hiki na hii itanifanya niishi kama Mkristo. Kwa vile hawajaniondolea sifa ya kutoa huduma kama vile ibada za mazishi, sakramenti ya mwisho na ubatizo, nitaendelea kutoa kwa wahitaji kwa sababu ninaupenda ukristo.
“Nashukuru sasa nimekuwa muumini wa kawaida nitaweza kufunga ndoa kanisani kwa kuwa nilikuwa nimefunga ndoa ya kisheria tu kwa DC.”
Kuhusu kwa nini aliamua kuacha upadri, Profesa Mosha alisema ni baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 20 na akaona ipo haja ya kuwa na familia lakini kanisa lilikuwa haliruhusu.
“Sasa kwa kuwa kanisa haliruhusu mapadri kuoa ndiyo maana nikaamua kuandika barua ambayo hata hivyo, imechukua muda mrefu kujibiwa na tayari nina watoto watatu wako chuo kikuu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...