Sunday, February 17, 2013

TAMKO LA RAIS KIKWETE KUHUSU MAUWAJI YA PADRI ZANZIBAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Evarist Mushi wa Parokia ya Minara Miwili ya Kanisa Katoliki mjini Zanzibar, mauaji yaliyotokea Zanzibar.

Rais Kikwete anawapa pole nyingi na rambirambi za dhati ya moyo wangu Baba Askofu Augustino Shayo wa Jimbo Katoliki, Zanzibar, maaskofu wote nchini na waumini wote wa Parokia ya Minara Miwili kwa msiba huo mkubwa uliowakuta.

Rais kikwete amemwambia Baba Askofu Shayo. ”Napenda kuwahakikishia kuwa tupo pamoja katika kuomboleza kifo cha Mpendwa Marehemu Padri Evarist Mushin a kuwa msiba huu ni wa kwetu sote.”

Ameongeza Rais Kikwete: “Nimeligiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”

“Aidha, nimewaagiza Jeshi la Polisi washirikiane na vyombo vingine vya Usalama nchini na mashirika ya upepelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji haya.”

Amesisitiza Rais Kikwete: “Nataka ukweli wake ujulikane ili kama kuna jambo lolote zaidi liweze kushughulikiwa na kukata mzizi wa fitina.”

Vile vile, Rais Kikwete amewataka waumini wa Kanisa katoliki na wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali inashughulikia suala hili na kuwa hakuna mtu wala watu ama kikundi cha watu kitachoruhusiwa kuvuruga amani ya nchi yetu

TARIFA MPYA KUHUSU KIFO CHA PADRI ZANZIBAR LEO


Taarifa  imeripoti kuwa Padre Mushi aliuawa na watu walipolisimamisha gari la Padre huyo alipokuwa akielekea katika kanisa la Mtakatifu Theresia lililoko eneo la Mtoni, na alipopunguza mwendo ili awasikilize, ndipo alipopigwa risasi kichwani na kusababisha gari alilokuwamo kukosa uelekeo na kuigonga nyumba iliyokuwa jirani. Watu walioshuhudia tukio hilo walimchukua Padre Mushi ili kumwahisha hospitalini katika jitihada za kuokoa uhai wake, lakini alifariki dunia. Waliomwua Padre Mushi bado hawajakamatwa.
-----------------------


Akina mama wakilia kwa uchungu kuomboleza kifo cha ghafla cha kupigwa risasi Padre Evaristus Mushi kilichotokea leo asubuhi muda mfupi kabla ya kuanza Misa ya Jumapili kwenye kanisa la Kigango cha Mtoni, Zanzibar. (Picha na Martin Kabemba via Lukwangule blog)

Taarifa kutoka Zanzibar zikiripotiwa na mwanahabari Donisia Thomas wakati kipindi cha Patapata cha WAPO radio FM kinaendelea, zinasema kuwa Padre Evaristus Mushi wa Kanisa la Parokia ya Minara Miwili huko Zanzibar amepigwa risasi majira ya saa moja asubuhi -na watu wasiofahamika- na kufariki dunia.


Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa na madaktari kutoka hospitalini alikopelekewa katika harakati za kuuokoa uhai wake.


Padre Mushi aliuawa akiwa anashuka kwenye gari lake tayari kuingia Kanisani kwa ajili ya kuendesha misa ya kawaida ya Jumapili katika kanida la Mtoni, mjini St. Joseph. Inaelezwa kuwa gari lisilofahamika lilifika na kufyatua risasi zilizomlenga Padre Mushi sehemu ya kichwani na hivyo kumsababisha majeraha yaliyokuwa yakivuja damu nyingi.


Mwanahabari anasema tukio hilo limezua taharuki kubwa miongoni mwa waumini ambao wamekataa kuahirisha ibada iliyokuwa iendeshwe na Padre huyo na kusema ikiwa kusudio ni kuwaangamiza Wakristo wote, basi na waangamizi wafike Kanisani wawaangamize wakiwa pamoja.


Jeshi la Polisi limeshafika katika eneo la tukio na kuanza uchunguzi.


Wakizungumza kuhusu hilo, raia wamesema hawana imani na Polisi wala Madaktari na hawatarajii jipya zaidi ya ripoti kuwa suala hili ni la uhalifu kwa kuwa tukio kama hili liliwahi kutokea mwishoni mwa mwaka jana kwa Padre Ambrose kupigwa risasi na taarifa zilisema lilikuwa ni tukio la kihalifu na kwamba risasi hazikutumika jambo ambalo halikuwa kweli kwani Padre Ambrose alikutikana na risasi alipohamishiwa katika hospitali ya Taifa, Muhimbili.


Kwa taarifa zaidi, tafadhali fuatilia vyombo mbalimbali vya habari.

SIMBA IMESHADUNGWA MSHALE 1-0 NA LIBOLO FC YA ANGOLA,

S5Mchezaji wa timu ya Simba ya Tanzania Shomari Kapombe kulia akichuana vikali na Maieco Antonio  mchezaji wa timu ya Libolo FC kutoka nchini Angola wakati wa mchezo wa  Klabu Bingwa  Afrika ( CAF) kati ya timu hizo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Timu ya Libolo FC ya Angola inaongoza goli 1-0 dhidi ya Simba ya Tanzania ni kipindi cha pili na mpira bado unaendelea.
S1Waamuzi wa mchezo huo wakiwaongoza wachezaji wa timu ya Simba na Libolo ya Angola wakati timu hizo zikiingia uwanjani tayari kwa kumenyana katika mchezo huo.
S2Wachezaji wa Simba ya Tanzania na Libolo FC ya Angola wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
S3Mashabiki kwa mbali uwanjani hapo wakishuhudia nguo kuchanika wakati timu hizo zikimenyana uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
S4Hizi siyo salakasi il ni harakati za kuwania mpira wakati wa mchezao wa Simba ya Tanzania na Libolo FC ya ambapo Libolo inaongoza goli 1-0  dhidi ya Simba ya Tanzania

TAARIFA YA INSPEKTA JENERALI WA POLISI SAID A. MWEMA KWA UMMA KUHUSU TUKIO LA KUUWAWA KWA PADRE EVARISTI MUSHI ZANZIBAR TAREHE 17 FEBRUARI, 2013


IJPMkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema akitoa taarifa ya jeshi hilo mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya jeshi hilo leo mchana.
Nimelazimika nizungumze nanyi kuhusu tukio la kuuwawa kwa Padre Evaristi Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar lililotokea leo asubuhi tarehe 17 Februari, 2013 eneo la Mtoni mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo watu wasiofahamika walimpiga risasi Padre huyo alipokuwa anaenda kusalisha ibada katika kanisa la Betras. Baada ya tukio hilo kutokea alikimbizwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja, ambapo baadae alifariki dunia. Tukio hili ni baya na la kusikitisha.
 2 Kufuatia kutokea kwa tukio hilo na kujirudiarudia kwa vitendo vya kuwashambulia na kuwadhuru viongozi wa dini na uchomaji wa nyumba za ibada, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tumeanza uchunguzi wa kina wa kuwatafuta wanaohusika na matukio hayo.
 3Hivyo, nimetuma timu ya wataalam waliobobea kwenye masuala ya upelelezi na oparesheni kutoka Makao Makuu ya Polisi, kwenda kushirikiana na timu ya wataalam iliyoko Zanzibar. Hadi sasa watu watatu wananshikiliwa kwa mahojiano.
 Jeshi la Polisi limeimarisha doria maeneo yote hapa nchini na tunafuatilia mienendo na kuakamata watu wote wanaochochea, kufadhili, kuhamasisha na kushiriki katika vitendo vya uhalifu, vurugu na fujo.
 Tukiwa katika kipindi hiki, nawaomba wananchi wote hapa nchini kuwa watulivu wakati suala hili linaposhughulikiwa kuhakikisha kwamba wahalifu hao wanakamatwa na sheria inachukua mkondo wake.
 Naomba nitumie fursa hii pia, kuwasiliana na wananchi wenzangu wenye taarifa zitakazosaidia wahalifu hao kukamatwa kutupa ushirikiano kupitia namba zetu maalum za simu zifuatazo 0754785557 au 0782417247 na namba za makamanda wa mikoa na vikosi, ili kuhakikisha kwamba amani, usalama na utulivu vinadumishwa hapa nchini.
    Nawashukuru wananchi wote ambao wamekuwa wakitupa ushirikiano. 
AHSANTENI SANA.

BAADHI YA FAMILIA ZA KOSA MAHALI PA KUISHI BAADA YA NYUMBA ZAO KUEZULIWA NA UPEPO MKALI





                 
BAADHI ya wakazi wa maeneo ya Mafisa mkoani hapa wamekosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa iliyonyesha leo jioni,


Mbali na kuezua nyumba hizo pia upepo huo uliangusha miti mirefu,taa za barabarani  na mabango marefu ya matangazo ya makampuni ya simu ya vodacom na tigo

Miongoni mwa mabango hayo ni bango kubwa la vodacom ambalo liliwekwa eneo la stendi ya mabasi ya Msamvu katikati ya geti kuu la kutokea mabasi eneo ambalo pia madereva wa boda boda huegesha pikipiki zao chini ya bango hilo.

" Ni mungu tu ametunusulu na kifo wakati bango hili linaanguka sisi tulikuwa hapa chini tukisubiri abiria kwa bahati tuliwahi kustuka,na kukimbia mwenzetu mmoja kwenye heka heka ya kukimbia aliiacha pikipiki yake ambayo aliangukiwa na bango hili na kuhalibika vibaya"alisema mmoja wa mabareva hao wa boda boda aliyejitambulisha kwa jina la Jackson Samwel

Hii ni mara ya pili kwa bango la kampuni hizo kuanguka ambapo mara ya kwanza takribani miaka miwili iliyopita bango la tigo lililowekwa katikati ya stendi ya daladala lilianguka na kuharibu daladala mbili ambazo kwa bahati zilikuwa hazina watu ingawa zenyewe zilihalibika vibaya baada ya kuanguliwa na bango hilo.

Pia upepo huo uliovuma jana kutoka upande wa kaskazini ya mji wa Morogoro uliezua nyumba za watu na kuangusha miti mirefu ambapo  hadi mtandao huu unakwenda hewani takribani nyumba 15 ziliezuliwa mapaa hali iliyosababisha wakazi wa nyumba hizo kukosa mahali pa kuishi.

BREAKING NEWZZZ!!!!! PADRI APIGWA RISASI HADI KUFA ASUBUHI HII HUKO ZANZIBAR

Taarifa zilipatika sasa hivi ni kuwa Paroko wa Kanisa la Katoliki Minara Mirefu Zanzibar, Evarist Mushi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi saa 1.00 asubuhi na kufariki kabla hajafika hospitali ya Minazi Mirefu. Paroko huyu amepigwa risasi akishuka katika gari lake wakati akienda kuendesha ibada ya saa 3.00 leo.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwako na vitisho vya wazi wazi dhidi ya wakristu huko visiwani Zanzibar ambapo inaelezwa kuwa jeshi la polisi halijafanya juhudi yoyote kuzuia tishio hili. Kumekuwapo na vipeperushi vinavyodai kuwa kupigwa risasi kwa padre Ambrose sio mwisho wa mapambano. 

Taarifa hizi zimeripotiwa direct toka Zanzibar.
R .I.P
SOURCE WAPO RADIO

Saturday, February 16, 2013

MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO, AZAM YAIFUNGA EL NASIR 3-1

Kiungo wa timu ya Azam FC, Bolou Kipre (kushoto) akitafuta mbinu za kumtoka mshambuliaji wa El-Nasir FC ya Sudan ya Kusini, Abdallmelik Sebit katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao la pili la timu yao lililofungwa na Kipre Tchetche (katikati) wakati ilipoibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya El Nasir ya Sudan ya Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
 Jabir Aziz akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa El Nasir FC ya Sudan ya Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa Azam FC, Brian Umomy akiwatoka walinzi wa timu ya El-Nasir FC ya Sudan ya Kusini, Jacob Osuru na Abdallmelik Sebit katika mchezo wa kombe la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Kikosi cha el Nasir ya Sudan ya Kusini
 Kikosi cha Azam FC
Mashabiki wa Azam

ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE LINDI LEO

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Narunyu, Kata ya Tandangongoro, alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimiana na watoto wa kijiji cha Narunyu, Kata ya Tandangongoro, alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo.
 Mkazi wa Kijiji cha Ng'apa wilaya ya Lindi mjini, akionyesha kadi yake ya matibabu ya Huduma ya Kadi ulkiopo chini ya Bima ya Afya, wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika kijiji hicho, leo Feb 16, 2013. Mama Salma Kikwete alimpatia fursa ya kuzungumza wakati akihimiza umuhimu wa wananchi kujiunga na mpango huo wa matibabu.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amegoma kushuka katika gari lake, kukataa kwenda kwenye mkutano wa ndani wa Chama Kata ya Tandangongoro, uliokuwa umepangwa na viongozi wa kata hiyo kufanyika katika chumba cha darasa la shule ya msingi ya kijiji cha Ng'apa, mkoani Lindi, leo Februari 16, 2013. Hatua hiyo iliwalazimu viongozi kutafuta ukumbi mwingine wa dharura. Mama Salma alisema si sahihi mkutano wa ndani wa Chama cha siasa kufanyika katika chumba cha darasa la shule ya serikali
Umati wa wananchi wa Kijiji cha Ng'apa wakimsiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akilipowahutubia mkutano wa hadhara leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASIMAMIA ZOEZI LA UTEKETEZAJI SILAHA HARAMU JIJINI DAR LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivuta waya kuashiria kufyatua mtego wa kuwasha moto wa kuteketeza Silaha haramu, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika zoezi hilo la uteketezaji wa silaha haramu, Lililofanyika katika Kambi ya Magereza jijini Dar es Salaam, leo Feb 16, 2013. Kushoto kwake ni Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Siro na wa pili kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Perera Ame Silima na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kmataifa, Benard Membe.
 Sehemu ya Silaha hizo zikianza kuteketea kwa moto baada ya Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufyatua waya maalumu wa kuwasha moto huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi, baada ya kusimamia zaoezi la uteketezaji wa Silaha haramu, lililofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam, leo.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Simon Siro, wakati wakipita kukagua sihala hizo haramu kabla ya kuanza kwa zoezi la uteketezaji wa silaha hizo haramu lililofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam, leo.


 Silaha haramu zilizoteketezwa hii leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa zoezi la uteketezaji wa Silaha Haramu, lililofanyika Ukonga Jijini Dar es Salaam leo.
Wimbo wa Taifa, kabla ya kuanza kwa zoezi hilo. 
*******************************************************

DKT. BILAL AWATAKA WANANCHI KUWAFICHUA WANAOMILIKI SILAHA HARAMU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameongoza zoezi la uteketezaji silaha haramu na kuwataka wananchi kushirikiana na serikali katika kuwafichua wanaomiliki silaha hizo mapema kabla athari haijawa kubwa zaidi.

Akizungumza katika zoezi hilo la kuteketeza silaha haramu, ambalo limefanyika pamoja kwa  nchi  wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye viwanja vya Magereza, Ukonga Jijini Dar es salaam Dkt. Bilal alisema  kila mwananchi ni mlinzi wa kwanza wa amani ya nchi yake  na  wanaomiliki silaha haramu ni wazi kuwa siyo raia wenye malengo mema na amani ya nchi zao.

“Naomba kuchukua nafasi hii kuushukuru uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kufanikisha zoezi hili ambalo linalenga kutukumbusha kuwa ili tuwe na Jumuiya bora yenye kupiga hatua, hatuna budi kuhakikisha eneo letu linabaki kuwa salama na kwamba wananchi wetu wanapata nafasi ya kufanya kazi zao za kujiongezea kipato bila kuwa na hofu ya usalama wa maisha yao,”

Alisema ndani ya Jumuiya kumekuwa na migogoro mbalimbali sambamba na matukio ya kihalifu ambayo mengi huchangiwa na uwepo wa silaha ndogo na kubwa ambazo hazimilikiwi kihalali.

Alisema takwimu zilizopo zinabainisha kuwepo kwa silaha haramu zipatazo 500,000 (laki tano) katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki hali ambayo inaonesha kuwa kuna kazi kubwa ya kukabiliana na migogoro ya aina mbalimbali ya uhalifu inayojitokeza katika jamii.

Alisema kufuatia raia wasio waaminifu kumiliki silaha haramu kumekuwepo na ongezeko la matukio ya kihalifu yanayotumia silaha na matukio mengi katika ukanda wa Afrika Mashariki yanatokea katika maeno ya mipakani na yale yanayohusisha muingiliano wa watu kutoka nchi moja kwenda nyingine, matukio ya ujambazi,  uvamizi na mengine ya aina hiyo.

Alisema ongezeko la silaha haramu lina athari nyingi katika maisha na maendeleo kwa ujumla na kutaja athari ya wazi kabisa inayotokana na ongezeko la silaha hizo kuwa ni ile inayojitokeza katika sekta ya Utalii ambako watu wameshuhudia kuongezeka kwa matukio ya ujangili unaofanywa katika mbuga za wanyama ambao unahatarisha kwa kiasi kikubwa mafanikio katika sekta ya Utalii.

“Tusipowadhibiti majangili mapema, siku wanyama wakipungua watahamia katika sekta nyingine. Kazi hii itakuwa rahisi kama tukiifanya kama Jumuiya na sio nchi moja moja,” alibainisha Makamu wa Rais.

Dkt. Bilal alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Ujerumani kwa kusaidia Jumuiya ya Afrika Mashariki kukabiliana na tatizo la silaha haramu na hasa Shirika la Maendeleo la Ujerumani GTZ ambalo limesaidia katika kufanikisha zoezi hilo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi wa Ujerumani nchini Klaus Brandes alisema  Serikali ya Ujerumani itaendelea kuisaidia Jumuiya katika kukabiliana na tatizo la silaha haramu ili kuhakikisha eneo la ukanda wa Afrika Mashariki linabaki kuwa na amani na salama.   

Alielezea kufurahishwa kwake na juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika kutatua migogoro kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kwenye Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
Februari 16, 2013

Watanzania tunaitakia kila la kheri Azam FC katika mechi yake ya leo dhidi ya Al Nasir Juba ya Sudan Kusini.


Mashabiki wa soka nchini Tanzania leo wataelekeza macho na masikio yao katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kushudia mechi ya kiataifa baina ya timu ya Azam Fc ikipambana na Al Nasir Juba  ya Sudan Kusini   
Mabingwa hao mara mbili wa Kombe la Mapinduzi Zanzibar Azam Fc leo watakuwa wakicheza kwa mara ya kwanza michuano inayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Africa (CAF).
Katika mechi ya leo Azam itaingia uwanjani kwa lengo la kupata ushindi mkubwa ili kujiweka mazingira mazuri katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Juba.

HATIMAYE SISTA ALIYEFUMANIWA AHUKUMIWA


MAHAKAMA ya Mwanzo mjini Sumbawanga,  imemtia hatiani aliyekuwa mtawa wa Shirika la Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani, kwa kufumaniwa na mume wa mtu na kuamriwa kumlipa fidia ya
Sh 700,000 mlalamikaji.
Katika kesi ya msingi ya madai, mlalamikaji Asteria Mgabo alimtaka Sista Yasinta amlipe Sh milioni 3 baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa, Martin Msangawale (39) ambaye pia ni mkazi wa mjini Sumbawanga.

Sista huyo ambaye ni daktari katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjiniSumbawanga, kwa sasa anaishi nje ya nyumba ya utawa eneo la Kantalamba.
Katika hati ya awali ya madai, inadaiwa mshitakiwa alifumaniwa na Asteria akiwa na mumewe Msangawale wakiwa kwenye nyumba ya kulala wageni  ijulikanayo kwa jina la Chipa iliyopo eneo la Katandala mjini Sumbawanga, Desemba 24  mwaka jana majira ya saa 7 usiku  ikiwa ni siku ya mkesha wa Sikukuu ya Krismas.
Akisoma  hukumu  hiyo juzi, hakimu wa  mahakama  hiyo, Jaffar Mkinga alisema kuwa ushahidi uliotolewa na mlalamikaji ulikuwa mzito wenye kuondoa shaka zote  kuwa mdaiwa alitenda kosa hilo tofauti na utetezi  uliotolewa na mdai kuwa ulikuwa dhaifu.

Awali katika  utetezi wake  mdaiwa  aliiambia mahakama  hiyo kuwa  kwanza alikuwa hajui kuwa Martin alikuwa  mume wa mtu na kukiri mbele ya mahakama hiyo kuwa alimweleza kuwa hana mke hivyo alimwomba amuoe.
Lakini Hakimu Mkinga alipinga utetezi huo kwa sababu usiku  huo wa mkesha  wa Krismas  mwaka jana, saa saba na robo usiku, mlalamikaji akiongozana na mwenyekiti wa mtaa wakiwa na mashahidi wengine watatu,  walimkuta mdaiwa na Martin wakitoka katika   moja ya vyumba katika nyumba ya kulala  wageni ya Chipa, akasainishwa.
“Kama hukufahamu kuwa Martin alikuwa  hana  mke ilikuwaje ukakubali kusaini karatasi hiyo ya fumanizi  iliyoandaliwa na mwenyekiti  huyo?” alihoji hakimu, akamhukumu kulipa sh 700,000.

Rais Deby wa Chad awafukuza kazi mawaziri wawili, ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kuwasimamisha kazi askari wa jeshi la polisi nchini humo.


Rais Idriss Deby wa Chad amewafukuza kazi mawaziri wawili wanaohusika na masuala ya ulinzi ikiwa ni baada ya wiki iliyopita kuwasimamisha kazi takriban polisi zaidi ya 6,000 kwa tuhuma za rushwa, upendeleo na udhalilishaji.
Katika tangazo lililotolewa katika radio ya taifa, rais Deby amemfukuza Waziri wa Usalama wa Umma Ahmat Mahamat Bachir na Waziri wa Usimamizi dhidi ya Ugaidi Bachar Ali Souleymane.
Kufukuzwa kwa mawaziri hao kunafuatia pia kufukuzwa kazi kwa Mkuu wa Polisi nchini humo, ikiwa ni siku mbili baada ya kulisimamisha kazi jeshi hilo.

Uso mtoto wa Jay – Z Blue Ivy Carter kwa mara ya kwanza waanikwa hadharani.!


Pichani ni Jay-Z na mtoto wake Blue Ivy mwenye umri wa mwaka mmoja kwa mara ya kwanza imewekwa hadharani kuonyesha baba na mwana wanavyofanana.
Blue Ivy akiwa na mama yake.

urais Kenya pamoja na mashitaka yanayomkabili ICC.


Mahakama Kuu nchini Kenya imemsafishia njia mmoja kati ya wagombea urais Bw. Uhuru Kenyata kuwania kiti cha urais wa taifa hilo katika uchaguzi mkuu ujao pamoja na kukabiliwa na mashitaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Ikiwa imebakia muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa Machi 4 mwaka, uamuzi huo umemuweka Kenyatta huru kuwania kiti hicho akionekana kama mmoja kati ya viongozi wanaongoza katika kinyang’anyiro cha urais.
Jopo la majaji watano waliokuwa wanasikiliza kesi hiyo wanasema mahakama kuu ndiyo yenye uwezo wa kuamua kesi hiyo.
Kesi hiyo ilifunguliwa kupinga ushiriki wa watu hao katika uchaguzi wa mwezi Machi, kwa kile walichokiita kukosa uadilifu kwa sababu tayari wamefunguliwa mashtaka ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya ICC.

WABUNGE 47 KIJIUNGA NA JKT, WAMO ZITTO KABWE,HALIMA MDEE,KAFULILA, MBOWE, JOSHUA NASSARI,ESTHER BULAYA,LEMA,NYAMBARI NYANGWINE N.K



 JUMLA ya wabunge 47 kutoka vyama CCM, Chadema na NCCR-Mageuzi, wamekubali kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa ajili ya mafunzo na uzalendo kwa taifa.
Habari za kuaminika zilizopatikana mjini Dar es Salaam jana na kuthibitishwa na Makao Makuu ya JKT, zinasema wabunge hao wametawanywa katika vikosi mbalimbali na wanatakiwa kuripoti kwenye vikosi vyao kunzia Machi mosi, mwaka huu.
Msemaji wa JKT, Meja Emmanuel Mruga, alipoulizwa kuhusu wabunge hao kujiunga na jeshi hilo, alisema mpaka sasa wana orodha ya wabunge 47 kutoka vyama mbalimbali.
Alisema wabunge hao, wametawanywa katika kambi mbalimbali kwa ajili ya mafunzo ambayo yatarajia kuanza mwezi ujao.
Alisema wabunge hao, waliomba wenyewe kwa ajili ya kupata mafunzo ambayo wanaamini yatawajengea uzalendo zaidi kwa taifa lao.
Baadhi ya wabunge ambao MTANZANIA imepata majina yao na vyama wanavyotoka kwenye mabano ni David Kafulila (NCCR-Mageuzi), Zitto Kabwe (CHADEMA), Halima Mdee (CHADEMA), Freeman Mbowe (CHADEMA), Abdulkarim Shaha (CCM), Esther Bulaya (CCM), Twaida Galusi (CCM), Neema Hemed (CCM), Ezekiel Wenje (CHADEMA), Joshua Nassari (CHADEMA), Raya Ibrahim (CHADEMA), Godbless Lema (CHADEMA) na Nyambari Nyangwine (CCM).
Akizungumzia mafunzo hayo, Zitto Kabwe alisema kuanzia sasa anajiandaa kuanza maisha mapya ya jeshi na atapumzika siasa kwa muda wa miezi sita.
“Najiandaa kupumzika siasa, kwa ajili ya kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), nadhani ni hatua nzuri ambayo tunataka kuwaonyesha Watanzania wazalendo na vijana wenzetu,” alisema Zitto.
Naye Mdee, alisema zaidi ya robo tatu ya wabunge wote vijana wa chama hicho, waliomba kujiunga JKT na tayari wamepangwa katika vikosi mbalimbali.
“Si mimi na Zitto, nakwambia karibu robo tatu ya wabunge vijana wa CHADEMA, tumeamua kujiunga kwenye mafunzo ya JKT,” alisema Mdee.
Alisema yeye amepangwa kikosi cha 842 KJ kilichopo Mlale, mkoani Ruvuma.
Alisema wengine ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ambaye amepangiwa kikosi cha JKT Ruvu, Mkoa wa Pwani.
Habari zinasema Mbowe aliomba kujiunga JTK na amepangiwa kambi moja mkoani Tabora.
Akizungumzia sababu za kujiunga na jeshi hilo, Mdee alisema wanataka kujifunza mambo tofauti yatakayowasaidia kutekeleza wajibu wao wa kisiasa na kijamii sawasawa.
“Unajua sisi ni viongozi wa watu, tunadhani mafunzo ya kijeshi yatatusaidia kutekeleza kazi za kila siku, kujifunza ukakamavu, na zaidi kwa vipi tunaweza kujilinda kwa mantiki ya usalama binafsi.
“Kingine ni kujifunza kazi za kila siku za maisha, kiuchumi, kijamii, kilimo na vitu kama hivyo ukizingatia sisi ni viongozi tunaopaswa kuongoza watu, hususani wapiga kura kwa mifano.
Kuhusu kujifunza zaidi uzalendo kama ambavyo imekuwa ikisemwa na viongozi serikalini, Mdee alisema uzalendo ni tabia ya mtu binafsi na kamwe jeshi haliwezi kumfundisha mtu uzalendo.
“Ninakubaliana na suala la nidhamu, jeshi linaweza kumfundisha mtu nidhamu, lakini siyo uzalendo.
“Walioharibu nchi na kuitumbukiza katika ufukara na ufisadi karibu wote wamepitia jeshini, hatuna cha kujifunza kwao kutokana na kwenda kwao jeshini,” alisema na kuongeza:
“Ngoja twende huko tukajifunze mambo ya ziada, naamini tutapata kitu cha ziada kwa ajili yetu na jamii tunayoiongoza”.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...