Saturday, February 16, 2013

FAMILIA YA NYERERE YAMKANA ANAYEJIITA MAKONGORO NYERERE

Mwalimu Nyerere

 Familia ya Joseph Nyerere, imejitokeza na kusema haimtambui mtuhumiwa wa kesi ya mauaji, anayejitambulisha kwa jina la Makongoro Joseph Nyerere.

Taarifa iliyotolewa na Nuru Nyerere-Inyangete, kwa niaba ya familia hiyo jana, ilisema hadi kifo cha baba yao, Joseph Kizurira Nyerere, mwaka 1994 haina taarifa zozote za kuwa na ndugu yao anayeitwa Makongoro Joseph Nyerere.

“Hadi baba anafariki dunia hatukuambiwa tuna ndugu anayeitwa Makongoro Joseph Kizurira Nyerere …watoto wote wa Mzee Joseph tunafahamiana, lakini kwa huyu ndiyo kwanza tunaambiwa kuwa ni ndugu yetu. Tunauhakikishia umma kwamba hadi kifo cha baba yetu hatukuambiwa juu ya kuwapo kwa ndugu mwenye jina hilo; hii ina maana kwamba hatumtambui,” alisema Nuru.

Naye mtoto mwingine wa Joseph, Matare, alisema, “Tangu kutangazwa kwa habari hizi tunapata simu nyingi za pole. Tunashangaa kwa sababu huyu mtu hatukuwahi kuambiwa kuwa ni ndugu yetu, na wala yeye mwenyewe hakuwahi kuja kwetu kujitambulisha kama ni mmoja wa watoto wa Mzee Joseph.”

Matare aliongeza, “Tumesoma kwa mshituko kwenye magazeti ya Februari 14, 2013 na katika mitandao ya kijamii, kuwa kuna mtu anayejiita Makongoro Joseph Nyerere. Huyu huyu hatumtambui kwa uhusiano, taarifa wala sura. Watoto wote wa marehemu Joseph Nyerere wanafahamika, hakuna mtoto wa marehemu mwenye jina hilo.”
Juzi, Makongoro ambaye ni mfanyabiashara, mkazi wa Dar es Salaam, alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini humo akikabiliwa na mashitaka ya mauaji ya mfanyabiashara mwenzake, Onesphory Kitoli. Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kuunganishwa katika kesi hiyo na mtuhumiwa mwingine mfanyabiashara maarufu, Marijani Abubakari marufu kama Papaa Msofe (50). Kesi hiyo itatajwa Februari 20, mwaka huu.

Wakili wa Serikali, Charles Anindo, alimsomea Makongoro mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi, Agnes Mchome, na kudai kuwa Novemba 6, 2011 huko Magomeni Mapipa, Makongoro alimuua kwa makusudi Kitoli kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.

Anindo alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na aliomba Mahakama iahirishe kesi hiyo hadi Februari 20, mwaka huu, ambako Makongoro ataunganishwa na Papaa Msofe kwenye mashitaka hayo.

Mtuhumkiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Mzee Mwinyi kuzindua kampeni ya uboreshaji wa wodi za kinamama jijini Dar


Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Taasisi ya Africa Youth Cross Cultural Exchange & Environment Conservation inatarajia kuzindua rasmi kampeni za uboreshaji wa wodi za kina mama wajawazito na watoto.
Mratibu wa Kampeni hiyo William Kotta amesema lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha wodi hizo zinakuwa na vifaa vinavyo jitosheleza kwa ajili ya kusaidia kina mama na watoto wanaoteseka na kupoteza maisha hasa wakati wa kujifungua.
Amesema taasisi hii katika kuanza kutekeleza kampeni hiyo, siku ya tarehe 22 Februari 2013 wameandaa chakula cha hisani kwa lengo la kuchangisha fedha na kusaidia upatikanaji wa vifaa hivyo.
Shughuli hiyo kwa heshima kubwa itaongozwa na Mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi rais mstaafu wa awamu ya pili.

Balozi Seif Idd aitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kuhamasishana kuanzisha miradi ya kijamii.


Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Mfuko wa  Jamii (NSSF) Kanda ya Dodoma Bibi Maryam Ahmed akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kabla ya kumsajili rasmi kuwa mwanachama wa Mfuko huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akijaza Fomu Maalum ya kuomba uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii ( NSSF) Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar
 Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) uliofika Ofisini kwake Vuga kumsajili rasmi kuwa mwanachama wa mfuko huo.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kitope Bibi Halima Bushir Abeid mchango wa Shilingi 100,000/- kwa ajili ya ulipaji huduma ya umeme ya kituo hicho mbaleni Jimboni humo.
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Tanzania (NSSF) umeombwa kufanya utaratibu wa kuishawishi mifuko mingine ya Jamii kuanzisha  miradi ya Jamii ili kuongeza pato la wanachama pamoja na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Ombi hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  wakati akijaza fomu maalum ya kuomba kujiunga kuwa mwanachama rasmi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) shughuli ambayo aliifanya Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif amesema Mfuko huo umeonyesha mwanga na matumaini makubwa kwa wanachama wake hasa kutokana na miradi mingi iliyoianzisha ambayo kwa asilimia kubwa inalenga kuwanufaisha wanachama wake hasa wale wenye kipato cha chini.
Amesema NSSF ni chombo cha wananchi kwa vile kinajihusisha moja kwa moja na hatma ya washirika wake ambao wengi wao ni wafanyakazi wenye kipato cha chini.
Balozi Seif aliuahidi Uongozi wa Mfuko huo wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwamba amehamasika ya mfumo wa mfuko huo na kupelekea moja kwa moja kuamua kujiunga ambapo ameahidi kuchangia kila baada ya kipindi cha miezi mitatu.
Mapema Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Dodoma ambao ndio uliopewa jukumu la kuhudumia Viongozi wa ngazi ya Juu Bibi Maryma Ahmed amesema zaidi ya Wabunge 165 wamekubali kujiunga kwa hiari kuwa wanachama wa Mfuko huo.
Bibi Maryam alimueleza Balozi Seif kwamba wabunge hao hupatiwa mafao yao mara wamalizapo utumishi wao wa Bunge sambamba na huduma za matibabu wakati wa kipindi chote cha kazi zao.
Wakati huo huo Balozi Seif akiwa pia Mbunge wa Jimbo la Kitope amekabidhi vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ukamilishaji ujenzi wa Tawi la CCM la Mbaleni liliomo ndani ya Jimbo hilo.
Akikabidhi vifaa hivyo ambavyo ni Mchanga, Matofali pamoja na Saruji Balozi Seif amesema wana CCM lazima waendelea kushikamana kwa lengo la kukiwezesha chama hicho kuendelea kushika dola.
Alifahamisha kwamba amani ya Tanzania itaendelea kuwepo na kuleta matumaini iwapo chama cha Mapinduzi kupitia Serikali zake zote mbili kitaendelea kuliongoza Taifa hili.
Vifaa hivyo kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la CCM Mbaleni Jimbo la Kitope sambamba na ahadi ya Seti moja ya Jezi na Mipira iliyotolewa na Mke wa Mbunge wa Kitope Mama Asha Suleiman Iddi vimegharimu jumla ya shuilingi Milioni  Moja Nukta Tisa (1,960,000/)

IBF Yachukua nafasi ya Katikati Barani Afrika.


Upimaji uzito katika mapambano mawili ya IBF yanayofanyika katika majiji ya Johannesburg na Tunis umefanyika vizuri leo.
Mapambano haya yaliyopewa jina la “Barabara ya kutoka Cape Town mpaka Cairo kwa IBF” kutokana na majiji haya kukaa moja kusini na lingine kaskazini mwa Afrika, yanafanyika wakati IBF ikijipambanua vyema katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.
Kusini mwa Afrika, leo imeshughudia mabaondia mawili wanaopambania ubingwa wa dunia kwa vijana walio chini ya miaka 25 wakipima uzito mbele ya mashirika mbalimbali ya habari ya ndani na nje ya Afrika ya Kusini.
Illunga Makabu kutoka Jamhuri ay Watu wa Kongo (DRC) alipima uzito kumkabili Gogota Gorgiladze wa Georgia. Upimaji huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa ulio katika hotel ya nyota tano ya Emperors Palace iliyoko katika jiji la Johannesburg!
Rodney Berman mtu anayeheshimika kwa kuwa promota wa kwanza kuandaa pambano la IBF la dunia katika bara la Afrika mwaka 1990, ndiye anayepromoti pambano hili!
Tayari wadau na mashabiki wa ngumi kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika zikiwamo Namibia, Zambia, Msumbiji, Zimbabwe na Tanzania wameshawasili nchini Afrika ya Kusini tayari kuangalia mpambano huo. Wengine walibaki Afrika ya Kusini wakati wa mashindano ya kombe la Afrika yaliyomalizika wiki iliyoita.
Msimamazi mkuu wa mpambano huu ni Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi aliyesimama pichani na mabondia Gogita Gorgiladze (kushoto) na Ilunga Makabu (kulia)
Kaskazini mwa Afrika,
Bondia ambaye ameshajizolea sifa kemkem Ayoub Nefzi wa Tunisia anayeishi nchini Belgium atapigana na bondia Ishmael Tetteh kutoka nchi ya Ghana kugombea ubingwa wa Afrika, Ghuba ya Uajemi  na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG) katika uzito wa Light Middle.
Mpambano huo uliopewa jina la “Uzuri wa Jasmine” kutokana na jina hilo kutumika katika mapinduzi yaliyomwondoa Rais wa zamani wa Tunisia Ben Ali unafanyika wakati Ayoub Nefzi akijiandaa kugombea mkanda wa juu wa IBF wa mabara mwezi wa tatu nchini Belgium.
Mabondia wote wawili wanatagemea kuonyesha moto mkali katika mpambano ambao tayari mashabiki wa ngumi kutoka katika nchi za Nigeria, Ghana, Libya, Misri, Algeria tayari wameshawasili nchini Tunisia kuangalia mpambano huo!
Tunisia inasifika kama nchi iliyowahi kutoa viongozi wengi wa mchezo wa ngumi katika bara la Afrika.

Fastjet yatoa mafunzo kwa Mtanzania wa Kwanza Mmaasai kuongoza ndege aina ya Airbus.


William Zelothe Stepehen akiwa ndani ya ndege aina ya Airbus A319.
William Zelothe Stepehen akiwa na marubani wa ndege ya Fastjet.
 
William Zelothe Stepehen ni Mtanzania wa Kwanza Mmaasai aliyepewa ithibati ya kuiongoza ndege aina ya Airbus A319 punde tu baada ya kupokea mafunzo ya urubani yaliyodhaminiwa na shirika la ndege la fastjet. Alipata mafunzo hayo nchini Uingereza kwa muda wa takriban miezi miwili na amerudi nchini Tanzania hivi karibuni. William alikulia Olosipe jijini Arusha ambapo ni nyumbani kwa wazazi wake.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIJESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
15 Februari 2013


 
Meli vita tatu (3) kutoka Jeshi la Wanamaji la Urusi zijulikanazo “MARSHAL SHAPOSHNIKOV”, “ALATAU” na “IRKUT” zikiongozwa na Rear Admiral Vladimir Vdovenko, watawasili nchini tarehe 16 February 2013 na kuondoka tarehe 20 Februari 2013 katika bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kufanya ziara ya kirafiki baina ya Jeshi la Wanamaji wa Tanzania na Urusi.
Waandishi wa Habari mnakaribishwa kufanya ‘coverage’ ya tukio hilo
Siku ya Jumatatu, tarehe 18 February 2013 saa 1.00 hadi saa 3.00 usiku.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764 742161
Email: ulinzimagazine@yahoo.co.uk
K U M B U K U M B U
MMJ/JB/
Feb 13
DP ADMN
Kufanya mahusiano na uongozi wa Bandari
1. Kurugenzi ya Habari imefanya zoezi la kuwaita waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari vifuatavyo TBC, ITV, CLOUDS TV, MLIMANI TV, STAR TV, na CHANEL TEN.
2. Uongozi wa Bandari hauruhusu Waandishi wa Habari kuingia kufanya “coverage” kwenye eneo hilo bila taarifa rasmi.
3. Inaombwa mahusiano yafanyike na bandari kuhusiana na mapokezi ya waandishi wa habari watakao hudhuria siku hiyo ili kukwepa usumbufu kwa waandishi hao.

 
(KM Mgawe)
Col
DIPR

NEY WA MITEGO APATA AJALI MBAYA YA GARI

Usiku wa juzi kuamkia jana, Rapa Ney wa mitego, alipata ajali mbaya ya gari maeneo ya Oysterbay jijini Dar na mguu wake ukshtuka kidogo, ila rafiki yake aliekuwa nae, ameumia kichwani na jana ndio aliruhusiwa kutoka hospitali

ajali hiyo ilitokea maeneo ya mataa ya St Peters, alipokuwa akitokea masaki kuelekea moroko, na  baada ya mataa yake kumruhusu kupita, alikutana na Lori lililokuwa likitokea Mjini kuelekea Moroko pia, likiwa halina taa na kumvaa kwa nyuma na kupelekea gari lake kuingia mtaroni na kuharibika vibaya

ndinga aliyokuwa nayo Ney ni aina ya Altezza, ina thamani ya shilingi millioni 14, kama angekuwa amelipia bima katika kiwango cha Comprehensive, yaani bima kubwa, angerudishiwa gari ndinga mpya, akini kwa bahati mbaya alilipa bima ya kawaida


Friday, February 15, 2013

MKONO WA ALBINO WAPATIKANA SUMBAWANGA

MKuu wa Mkoa wa Rukwa , Stella Manyanya wa tatu kulia akibubujikwa na machozi jana usiku baada ya ya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa , Peter Ngusa (kulia) akiwa ameushikilia mkono ulionyofolewa hivi karibuni kutoka kwa mwanamke mwenye ulemavu wa
ngozi (hayupo pichani) na kufukiwa poroni kijijini Miangalua wilayani Sumbawanga akiuonesha hadharani mbele ya majengo ya Hospitali ya Mkoa mjini hapa , watatu kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa , Dk John Gurisha

Mmoja wa askari akifungua majani ya mgomba yaliyoufunga mkono ulionyofolewa hivi karibuni kutoka kwa mwanamke mwenye ulemavu wa ngozi (hayupo pichani) na kufukiwa poroni kijijini Miangalua wilayani Sumbawanga ambao akiuonesha hadharani mbele ya majengo ya Hospitali ya Mkoa mjini hapa jana usiku jana Februari 14.

JAJI MKUU WA KENYA, MHE. MUTUNGA AKUTANA NA WAJUMBE TUME YA KATIBA


Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga (katikati) akibadishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) na Mjumbe wa Tume, Dkt. Sengondo Mvungi nje ya ukumbi wa Tume Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume leo Ijumaa (Feb. 15, 2013). Mhe. Mutunga alikutana na Wajumbe ili kubadilishana mawazo na uzoefu katika uandishi wa Katiba Mpya.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani (kushoto) akibadilishana mawazo na Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga nje ya ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume leo (Ijumaa Feb. 15, 2013). Mhe. Mutunga amekutana na Wajumbe wa Tume kubadilishana mawazo na uzoefu wake kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto) akimwonyesha nakala ya Kitabu Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga (katikati) nje ya ofisi za Tume mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na wajumbe wa Tume baina yao uliofanyika katika ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam leo (Ijumaa Feb. 15, 2013). Mhe. Mtungi amekutana na Wajumbe wa Tume kuzungumzia uzoefu wake kuhusu uandishi na utekelezaji wa Katiba Mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba. (PICHA NA TUME YA KATIBA)

JESHI LA POLISI WALIVYOWEKA ULINZI MKALI KUFUATIA MAANDAMANO YA WAFUASI WA SHEKH PONDA

5Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi nje ya jengo la Sukari lililopo mkabala na Makutano ya Barabara za Ohio na Sokoine Driver Posta jijini Dar es salaam jengo hilo ndmo zilimo ofisi za mwendesha mashtaka wa Serikal Dk.Eliezer Feleshi, Ulinzi huo umeimarishwa kutokana na tishio la wafuasi wa Shekh Ponda kutishia kuandamana kwenda kwa Mwendesha Mashtaka huyokushinikiza Shekh Ponda aachiwe huru.

Baadhi ya wafuasi hao wa Shekh Ponda wamekamatwa katika maeneo mbalimbali wakati wakijaribu kuingia katika eneo la Posta ambapo ulinzi mkali uliimarishwa huku polisi wakitumia Magari, Pikipiki, Mbwahuku makachero wakizunguka kila mahali.
Baadhi ya Barabara zilifungwa ili kuweka eneo hilo katika hali ya usalama zaidi na kuhakikisha linzdhibitiwa na kulidwa kirahisi.
3Poalisi wakiimarisha Doria katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
6Askari Polisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki kam wanavyoonekana wakiranda katika mitaa mbalimbali Posta jijini Dar es salaam.

Lady Gaga Cancels World Tour For Hip Surgery.


Lady Gaga has cancelled the remainder of her world tour after discovering she needs surgery for a hip injury.
The announcement was made on Wednesday, one day after the pop superstar lamented having to delay some of her forthcoming North America concerts.
A news release said Gaga, 26, has a tear in the labrum in her right hip that would require surgery followed by a recovery period.
The labrum is a layer of muscle that helps holds the ball-shaped hip joint in place.

NCCR – Mageuzi yapinga hatua zozote za kutaka kuzuia matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni.

Chama cha NCCR – Mageuzi kimesema kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya Katibu wa Bunge kwa waandishi wa habari juu ya mpango wa kuzuia kurusha matangazo moja kwa moja na badala yake kuyafanyia kwanza uhariri kabla ya kuwafikia walaji.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho Faustin Sungura NCCR – Mageuzi inapinga kwa nguvu zote, hatua zozote zinazotaka kuchukuliwa na mamlaka yeyote za kuzuia matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni.
Amesema wanapinga hatua hizo kwa sababu, hoja na sababu za kutekeleza azma hiyo kama zilivyotolewa na Katibu wa Bunge ni hoja dhaifu na hasi.
Amesema mawazo ya Katibu wa bunge yanakinzana na Ibara ya 18(d) ya katiba ya nchi.(Picha na Maktaba).

Nigerian singer Susan ‘Goldie’ Harvey has died in Lagos.

Nigerian pop singer Susan Oluwabimpe Harvey, popularly known as “Goldie”, has died after a sudden illness.
Her record label said Miss Harvey, 31, had complained of a severe headache shortly after returning to Nigeria from the US where she had attended the music industry’s Grammy Awards.
The star was rushed to a hospital in Lagos, where she was pronounced dead.
Goldie had won several industry awards and appeared in last year’s celebrity Big Brother Africa TV show.

Pope appoints Ernst von Freyberg new Vatican bank head.

Pope Benedict XVI has appointed German lawyer Ernst von Freyberg to head the Vatican’s embattled bank.
Mr Freyburg’s selection is one of the last major appointments of the Pope’s tenure in office.
The bank, officially known as the Institute for Works of Religion, has been dogged by scandal in recent years.
The pontiff, 85, shocked the world’s biggest Christian Church on Monday when he announced his resignation.

AFYA YA MATUMAINI YATENGAMAASHIRIKISHO la filamu nchini(TAFF) limesema, limefurahishwa na taarifa iliyotolewa na madaktari wa hospitali ya Amana kuwa afya ya msanii wa vichekesho Bi.Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’iposhwari na wamemruhusu kurudi nyumbani.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam jana Rais wa Shirikisho hilo la filamu nchini(TAFF) Simon Mwakifamba alisema kuwa wao kama shirikisho wamepokea kwa furaha taarifa hiyo.

"Tunajisikia poa kwa afya ya msanii huyo kurejea kuwa nzuri,  baada ya kuwa ameruhusiwa na madaktariwa hospitali hiyo ya Amana kwa kuwa amerudi nyumbani kwao Kiwalani jijini Dar es Salaam,"alisema Mwakifamba.


Afya ya msanii huyo ilibadilika na alianza kuumwa alipokuwa ameenda nchini Msumbiji na alipokelewa na wasanii wenzake kibao baada ya kutua  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere jijini Dar akiwa hoi kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...