Friday, February 15, 2013

MKUU WA MKOA WA RUKWA AAHIDI KUWACHUKULIA HATUA KALI WALANGUZI WA NISHATI YA MAFUTA MKOANI HUMO



Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika kikao cha baraza la ushauri la watumiaji wa nishati na maji nchini na wadau wake walipotembelea Mkoani Rukwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za baraza hilo. Mkuu huyo wa Mkoa alitoa pongezi kwa kazi nzuri wanayofanya na kuahidi kuwachukulia hatua walanguzi wa nishati ya mafuta pamoja na wale wanasimamia kwa kushindwa kufanya kazi yao vizuri. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
 
Mwenyekiti wa baraza la ushauri watumiaji wa maji na nishati nchini Eng. Profesa Katima akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema kazi kubwa ya baraza hilo ni kutetea na kulinda haki za watumiaji wa maji na nishati ambayo ni maji safi na maji taka, umeme, petroli na gesi asilia.
 
Baadhi ya wadau wa mkutano huo ambao ni vyombo vya ulinzi na usalama, Tanesco, EWURA Mkoa wa Rukwa, wawakilishi wa sheli za mafuta na shirika la Maji safi na Maji taka Mkoa wa Rukwa (SUWASA) 
 
Wawakilishi wa baraza hilo Mkoani Rukwa
 
Picha ya pamoja.
(Na Hamza Temba -Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

WAZIRI WA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO ATEMBELEWA NA BRITISH COUNCIL OFISINI KWAKE

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (Mb) akisalimiana na Mkurugenzi wa British Council nchini Sally Robinson (kulia) leo  Ofisini kwa Waziri,alipokwenda kumtembelea na kufanya mazungumzo mbalimbali kuhusu tasnia ya ubunifu wa Sanaa na Utamaduni pamoja na jinsi ya kuwajengea uwezo katika fani mbalimbali za sanaa na ujasiria mali.
Picha ya pamoja
 Waziri wa Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara (Mb)akizungumza na Mkurugenzi wa British Council nchini(kulia) Sally Robinson leo alipomtembelea Ofisis kwake jijini Dar es Salaam na kuzungumza masuala mbalimbali ya tasnia ya Utamaduni,

Rais Jakaya Kikwete Asaini Kitabu Cha Maombolezo na Kutoa Heshima za Mwisho Kwa mwili wa Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT)jana, Alhamisi, kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha kabla ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT)Jana, Alhamisi, kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati nyumbani kwa Askofu mara baada ya kuwa ametoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha jana, Alhamisi, Februari 14, 2013. Picha zote na Freddy Maro-IKULU

JAJI MKUU WA UGANDA MHE. ODOKI AKUTANA NA WAJUMBE WA TUME YA KATIBA

UG CJ 1Jaji Mkuu wa Uganda Mhe. Benjamin Odoki (kushoto) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (alhamisi Feb. 14 2013) kuhusu uzoefu wake katika uandishi na utekelezaji wa Katiba. Jaji Odoki aliongoza Tume ya Katiba ya Uganda iliyoundwa mwaka 1989. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.

UG CJ 2Jaji Mkuu wa Uganda Mhe. Benjamin Odoki (kulia) akiongea na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Jaji Odoki, ambaye aliongoza Tume ya Katiba ya Uganda iliyoundwa mwaka 1989, amekutana na Wajumbe wa Tume leo (alhamisi Feb. 14, 2013) na kuzungumzia uzoefu wake kuhusu uandishi na utekelezaji wa Katiba Mpya.
UG CJ 5.Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Assaa Rashid (kushoto) akimkaribisha Jaji Mkuu wa Uganda, Mhe. Benjamin Odoki (katikati) mara baada ya kuwasili katika ofisi za makao makuu ya Tume hiyo Jijini Dar es Salaam leo (alhamisi Feb 14, 2013) na kulia ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume, Bw. Joseph Ndunguru. Jaji Odoki, ambaye aliongoza Tume ya Katiba ya Uganda iliyoundwa mwaka 1989, amekutana na Wajumbe wa Tume na kuzungumzia uzoefu wake kuhusu uandishi na utekelezaji wa Katiba Mpya

SPIKA WA BUNGE ANNA MAKINDA AONGEZEWA ULINZI

SPIKA wa Bunge, Anne Makinda ameongezewa ulinzi pamoja na kubadilishiwa namba za gari analotumia kutokana na vitisho anavyovipata kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe wa simu.
Taarifa ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa Chadema kutoa namba za Spika na kuzigawa kwa wafuasi wake waliofika kwenye mkutano uliofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam hivi karibuni ili wamtumie ujumbe mfupi wa simu.

Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa Spika Makinda amepokea ujumbe mfupi wa simu zaidi ya 400 na kupigiwa simu zinazofikia 200 za kumkashifu na vitisho.

Taarifa zilizopatikana jana zinaeleza kuwa Spika Makinda amekuwa akitumiwa ujumbe mfupi wa vitisho ambavyo inaonyesha kuwa wananchi wana hasira naye na ndiyo maana ameongezewa ulinzi.

Vyanzo vyetu vya habari vimeeleza kuwa gari la Spika Makinda limebadilishwa namba kwa kuondolewa herufi S ambayo humaanisha Spika na kuwekwa namba nyingine ambazo bado hazijajulikana.

“Watu wanaomtumia ‘meseji’ wana hasira, wanaweza kumdhuru na ndiyo maana ameongezewa ulinzi. Hata magari yake aliyokuwa akitumia yamebadilishwa na kupewa mengine tofauti,” kilieleza chanzo chetu cha habari.

Spika Makinda mwenyewe alipopigiwa simu ili kueleza kuhusu suala hilo la kuongezewa walinzi simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah naye simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.Tangu Chadema wagawe namba hiyo baada ya kumtuhumu Spika pamoja na msaidizi wake, Job Ndugai kuwa amekuwa akipindisha kanuni wakati wa kuliongoza Bunge.

Taarifa zilieleza kuwa wamekuwa wakisumbuliwa na kutumiwa ujumbe za vitisho.Wakati hayo yakitokea, tayari Ofisi ya Bunge imesema itawachukulia hatua kali wale wote waliotumia lugha chafu kwa ujumbe mfupi ama kupiga moja kwa moja kwa Spika na Naibu wake.

Katibu Mkuu wa Bunge, Dk Kashililah juzi alisema kuwa kutoa namba si tatizo, bali kuzitumia namba hizo kinyume na taratibu ndiyo haitakiwi, jambo ambalo linaweza kusababisha baadhi yao kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Wote waliotoa lugha za matusi kwa Spika Makinda na Naibu Ndugai watachukuliwa hatua za kisheria.

Tutawatafuta kwa njia zote, hii itasaidia kuwa fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo ambao wanapewa namba kwa manufaa ya wananchi, lakini wanazitumia kinyume chake,” alionya Kashililah.

“Tutawasaka kwa kila hali, tutawabaini tu kwa kushirikiliana na idara mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Polisi ili wachukuliwe hatua kali.”

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alipoulizwa jana kuhusu msimamo wa chama chake baada ya kutoa namba hizo kwa wananchi alisema; “Bunge halijatuuliza ila wakituuliza tutajibu.”

WIVU WA PENZI LA MAINDA WAMFANYA RAY NA STEVEN NYERERE WAKOSANE



MASTAA wawili wenye majina makubwa ndani ya Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wanadaiwa kuwa kwenye bifu zito kisa kikielezwa kuwa ni mwigizaji , Ruth Suka ‘Mainda’, 


Kwa mujibu wa vyanzo makini vilivyo karibu na mastaa hao, hofu imetanda kwamba huenda wawili hao wakazama kwenye ugomvi kama ule wa Ray na marehemu Steven Kanumba.

“Ugomvi wa Ray na marehemu ulikuwa mdogo ila ulikuzwa na alipofariki dunia Kanumba kuliibuka mambo mengi sana, naomba marafiki wa dhati wa wawili hawa wakae nao ili kuweka mambo sawa,” ’ alisema mwigizaji mmoja.

Inadaiwa kuwa chanzo cha yote ni pale Steve Nyerere alipoanzisha kampuni ya kazi zake za sanaa akimshirikisha Mainda, jambo linalosemekana kumkera Ray aliyekuwa akifanya kazi na mwigizaji huyo wa kike chini ya Kampuni ya RJ Production.

“Kuna wakati eti Ray huwa hapendi kumuona mtu akiwa karibu na Mainda, mara nyingi huwa anakuwa na wivu kwa kuwa anahisi kuna kitu zaidi ya kazi,” kilisema chanzo kingine na kusisitiza kuwa Ray alimpiga ‘stop’ Mainda kushirikiana na Steve Nyerere huku suala la wivu wa kimapenzi likitajwa.

Ilidaiwa kuwa kabla ya mtafaruku huo, Steve Nyerere na Ray walikuwa ni maswahiba lakini sasa wamegeuka chui na paka na katika kutafuta ‘sosi’ ya yote hayo, ndipo Mainda akatajwa.

Vyanzo hivyo vilifunguka kuwa hali hiyo ilizua tafrani kubwa kwa kuwa tayari filamu ya Steve Nyerere (jina kapuni) ilikuwa imeanza kurekodiwa.


Baada ya kupata taarifa hizi, mwandishi aliwatafuta wahusika, wa kwanza alikuwa Steve Nyerere, alipoulizwa kuhusiana na hilo alikiri kutokea kwa ishu hiyo.

“Ni kweli mimi na Ray ni chui na paka lakini sitaweza kukwambia sababu ya ugomvi wetu kwa kuwa nitaibua mambo mengi sana, kipindi hiki nipo katika kubadilisha maisha yangu,” alisema Steve Nyerere.

Ray alipotafutwa kwa simu ya kiganjani hakupatikana na hata alipofuatwa ofisini kwake Sinza-Mori, Dar hakuwepo.

Kwa upande wake Mainda, simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kuwapata wawili hao ili nao wafunguke ya moyoni mwao zinaendelea.

VAZI LA MBUNGE SHYROSE BHANJI LAZUA UTATA BAADA YA KUKIANIKA "KITOVU" CHAKE




VAZI alilotinga Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji limezua utata kufuatia kuonesha sehemu yake ya tumboni (kitovu). 


Utata huo umekuja mara baada ya picha inayomuonesha mbunge huyo akiwa amejipara  na kuvalia vazi hilo ambalo linamuonesha sehemu hiyo nyeti na kutupiwa mtandaoni.

“Jamani huu ni utata sasa, inakuwaje mheshimiwa anatinga vazi kama hili? Haya mambo bora angewaachia mastaa wadogo, umri wake haufanani na mambo haya!” aliandika mdau mtandaoni

ASKOFU AMANI: TUMEINGILIWA NA SARATANI YA UVUNJIFU WA AMANI

images

Askofu wa Jimbo la Moshi la Kanisa Katoliki Tanzania, Askofu Isaac Amani Massawe amesema kuwa Tanzania imeingiliwa na ugonjwa wa saratani wa kuvunja amani na utulivu na Watanzania wasipobalika na kukubatia amani watajuta.
Amesema kuwa baada ya miaka 50 ya Uhuru, Watanzania sasa wamefungua ukurasa mpya na nchi imeanza kupoteza sifa ya kuwa nchi ya amani na utulivu.
Aidha, amesema kuwa wajibu wa watu kuishi kwa amani siyo wajibu wa Serikali ama wa Dini ama wa Kanisa bali ni wa kila mtu kwa nafsi yake.
Askofu Amani ameyasema hayo leo, Alhamisi, Februari 14, 2013 wakati alipokuwa anatoa neno la shukurani baada ya kumalizika kwa Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Askofu Jimbo la Moshi, Askofu Mstahivu Amedeus Peter Msarikie katika Kanisa Kuu la Kristo Mfalme mjini Moshi.
Askofu amewaambia mamia kwa mamia ya waumini: “Tumefungua ukurasa mpya katika Tanzania. Baada ya miaka 50 ya amani na utulivu sasa tumebadilika. Tanzania ya leo siyo Tanzania ya zamani sasa tumeanza kuongozwa na misingi ya vurugu za kidini na vurugu za kifedha.”

Ameuliza Baba Askofu Amani: “Tumeelimika zaidi ama tumechoka amani? Tumeingiwa na saratani ya uvunjifu wa amani na migawanyiko kwa misingi ya kidini na kifedha na mingine ya aina mbali mbali. Njia nzuri ya kuagana na mzee wetu Askofu Msarikie ni kuishi maisha aliyoishi yeye- maisha ya amani na utulivu. Yeye alikuwa chombo cha amani na anapumzika kwa amani kwa sababu aliishi maisha ya amani.”
Ameongeza: “Kuishi kwa amani na utulivu siyo suala wala wajibu wa Serikali ama wa Kanisa ama wa Dini ni wajibu wa kila mtu kwa nafsi yake na kila mmojawetu anao wajibu wa kusali ili kuombea amani ambayo imedumu katika nchi yetu kwa miaka mingi sana – miaka 50 sasa lakini inaonyesha kila dalili ya kutoweka.”
Amesisitiza: “Ndugu zangu amani hairithishwi, amani hujengwa na hulindwa. Changamoto alichotuachia Askofu Msarikie ni kutafuta na kuilinda amani katika nchi yetu. Huwezi kuwa mtu wa vurugu na mvunja amani na bado ukapata starehe ya milele mbele ya Mwenyezi Mungu. Sasa ni wakati wa kulea taifa letu, kulitengeneza upya na tumwombe Mungu atusaidie katika safari hii ndefu.”

Thursday, February 14, 2013

MAANDALIZI YA NYAMA YA FARASI INAYOLALAMIKIWA KUUZWA KWA WANANCHI UINGEREZA


Wafanyakazi wa Kampuni Spanghero, inayosambaza nyama nchini Uingereza wakiandaa nyama hiyo tayari kwa kupaki katika vifuko kwa kuwauzia wateja wao, ambapo hivi sasa Kampuni hiyo inaandamwa kwa kudaiwa kuwauzia wateja wake nyama ya Farasi badala ya nyama ya Ng'ombe. Imeelezwa kuwa wateja wa kampuni hiyo wamekuwa wakifurahia huduma hiyo wanayoipata kwa bei nafuu tofauti na awali.

RAIS KIKWETE ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA MAREHEMU ASKOFU MSTAAFU JIMBO KATOLIKI MOSHI MHASHAMU AMEDEUS MSARIKIE


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za Mwisho mbele ya jeneza la Askofu Mtsaafu jimbo Katoliki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa misa ya Mazishi iliyofanyika katika kanisa na Kristu Mfalme, mjini Moshi leo.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Askofu Mstaafu Jimbo katoliki la Moshi,Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi leo



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Askofu Mstaafu jimbo Katoloki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi leo. Picha na Freddy Maro wa Ikulu

CHADEMA yawakumbuka wagonjwa siku ya wapendanao

Chama cha Demokrasia na Maendeleo 'CHADEMA' leo katika siku ya wapendanao ''Valentine's Day'' wameiadhimisha kwa kutembelea wagonjwa katika hospitali ya Mwananyamala ambayo iko katik Halmashauri ya Manisipaa ya Kinondoni. Matembezi hayo yaliongozwa na madiwani na viongozi wa jimbo na kata na matawi na wanachama wengine wa CHADEMA.

''Siku ya leo CHADEMA tumefanya usafi; kufagia, kufyeka, kukusanya takataka, kusikiliza changamoto zinazowakabiri wagonjwa na wauguzi, pia katika kuonyesha ishara ya upendo katika siku hii tumewaletea wagonjwa vitu mbalimbali ikiwemo mikate, juice, maji, sabuni nakadhalika.'' Alikaririwa mmoja wa makanda














JAMBO TZ Blog Wishes You a Happy Valentines Day


KAMPUNI YA BIA YA TANZANIA (TBL) YATOA BASI KWAAJILI YA TIMU YA TAIFA



Mwanariadha Oscar Pistorius amuua mpenzi wake kwa risasi. “Valentine’s Day surprise that went tragically wrong”.




 Mwanariadha Oscar Pistorius alipokuwa katika mashindano ya Olympic mwaka 2012 mjini London.
Mwanariadha na mshindi wa medali za dhahabu wa Paralympic raia wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, amekamatwa  nyumbani kwake mjini Pretoria kwa kosa la kumuua mpenzi wake baada ya kumpiga risasi moja kichwani na nyingine mkononi , majeraha yaliyopelekea kifo cha binti huyo.

Chanzo cha Pistorius kumsuti mpenzi wake bado hakijaeleweka, japo fununu za awali zinadai uenda Pistorius alijichanganya na kudhani amevamiwa na mwizi/jambazi kutokana na hali mbaya ya uhalifu anayoikabili nchi ya Afrika Kusini.

Binti huyo Reeva Steenkamp, (30) mwanamitindo alilenga kumsuprise Pistorius kwaajili ya valentine.

Msemaji wa Polisi aliliambia shirika la habari la Reuters “tumekuta pisto ya mm9 eneo la tukio, na mtuhumiwa amepelekwa kituoni kwaajili ya utaratibu mwingine”.

Pistorius mwenye miaka 26 maarufu kama “blade runner” amekuwa ni mlemavu wa kwanza kushiriki Olympic mbali na mashindano yao maalum ya Paralympic , hukimbia riadha kwa kutumia vifaa maalum vilivyofungwa miguuni kwake,  baada ya kuzaliwa bila miguu yote miwili.
 
Mpenzi wa Pistorius, Mwanamitindo  Reeva Steenkamp aliyepigwa risasi na kupoteza maisha.
 Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wake   Reeva Steenkamp November 2012.

Zimbabwe kuipigia kura Katiba mpya.


Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai anasema nchi hiyo inatarajiwa kufanya uchaguzi wa bunge na urais mwezi Julai baada ya kupiga kura  maoni juu ya katiba mpya mwezi Machi.
 Alisema hayo  Jumatano baada ya waziri wa maswala ya katiba Eric Matunenga  kupanga tarehe ya Machi 16 kwa ajili ya kupiga kura ya maoni.
 Katika mkutano na waandishi wa habari huko Harare , Matinenga alieleza wasi wasi wake kuwa muda hautoshi na pengine muda zaidi huenda ukahitajika kwa ajili ya uchaguzi wa Machi.
 Baraza la kitaifa la bunge (NCA) ambalo linajumiwsha makundi  ya harakati za kidemokrasia   huko Zimbabwe  limesema  litapinga tarehe  upigaji kura wa maoni  hapo Machi 16 mahakamani .
Katika mahojiano na Sauti ya Amerika mwenyekiti NCA Lovemore  Madhuku amesema kundi lake linataka serikali itoe kipindi cha mdahalo cha  miezi miwili hivi  kabla ya wapiga kura kufanya uamuzi wao juu ya katiba mpya.
 Chama cha Bw. Tsvangirai cha MDC na kile cha  rais Robert Mugabe cha ZANU PF wote wanaunga mkono  mabadiliko hayo mapya.
 Jumuiya ya maendeleo ya Afrika Kusini inataka  katiba mpya  iidhinishwe kabla  ya Zimbabwe kufanya uchaguzi mkuu.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...